Jukwaa la Siasa Linapoteza Mvuto Tujenge Hoja, Tuache Taarabu

Soma tena nilichoandika
Kuna sehemu umeona nimeegemea upande?
Huku unapwaya !

Nyuzi za siasa zinapostiwa yes je za aina gani?
refer to your heading umesema watu waache taarabu wajenge hoja plus maneno mengine, how come uite mawazo ya wenzio ni taarabu? hiyo yote ni kwa sababu wameenda kinyume na wewe,,

ok kingine mfano kuna baadhi ya wachangiaji wamesema jukwaa limevamia na chawa wa mama, shida sio kuvamiwa ila wao wanaplay part yao kwa kutoa mawazo yao kichwani na namna wanavyo mu appreciate mtu,,, hatuwezi tukafanana kwenye kufikiri
 
Asante kwa maoni yako sasa fatilia na maoni ya wenzio!
 
Naunga mkono hoja 🤝
Nyongeza tu hatujasema watu wasipandishe mada jukwaani hapana ila basi ziwe mada zenye hoja mada za viwango bora kulingana na hadhi ya jukwaa siasa ni maisha na lazima maisha yawe na msingi mzuri
 
Kusema kweli kuna hoja za maana na zinastahili utulivu ili kujibiwa kwa ufasaha.

Ila kuna hoja ambazo, anavyokuja ndivyo tunavyompokea, tunajaribu kuweka mizani sawa ili huyo anayeleta shallow topics ajipange wakati mwingine aje na mada fikirishi.
Matusi sio suruhusho tujenge hoja haijalishi umekereka kiasi gani
Kuna mdau kasema ni ngumu sana kujadiliana na mtu anayelipwa kutetea ugali wake. Tutawapokea namna wanavyokuja....
Nonsense!
 
Tusubiri kwa miaka 30 mingine🤔
 
Kweli Sasa kama mada zenyewe za kina tlaatlaah na mwashambwa kitu kama watu kutekwa wanashabikia,Kwa nini watu wenye mioyo ya jazba wasiwatukane!ingawa sipendi MATUSI.
 
Matusi sio suruhusho tujenge hoja haijalishi umekereka kiasi gani

Nonsense!
Mkuu,
Hatuwezi kufanana, ukitaka hivyo labda uwaambie mods wafanye sensorship ya mada, na hapo utaondoa dhana ya where we dare to talk openly. Kwa hiyo hata hizo tunazooona mada za hovyo, zinaruhusiwa as ni free forum, wanaoona zinawafaa watajadili, wanaoona zinazingua watatukana au kukaa kimya.

Wengine tutatukana in a very polite language ili kuondoa sumu kwenye ubongo, hatutakaa kimya.
 
Naunga mkono hoja 🤝
Nyongeza tu hatujasema watu wasipandishe mada jukwaani hapana ila basi ziwe mada zenye hoja mada za viwango bora kulingana na hadhi ya jukwaa siasa ni maisha na lazima maisha yawe na msingi mzuri
Sijamanisha pia wasipandishe kabisa labda haujanielewa,maana yangu mada zao ziwe na hii hoja uliyo itoa hapa.
 
Umechelewa ndugu, ni vigumu mno kupata unachotaka kwa sasa......jukwaa limevamiwa na nyumbu, wao thinking imekuwa prohibited hivyo unahitajika kusifia tu.
 
Kwa maoni yangu,
nadhani siasa imevamiwa na jamii ambayo haifahamu vema au haina ufahamu ya kwamba siasa ni sayansi, na sio porojo, mihemko, matusi, uongo, uzushi au mahali pa kutafutia excitements.

na hata hoja ikiletwa jukwaani katika sura nilizozitaja hapo juu, mbobevu katika sayansi ya siasa kamwe hawezi kubabaika wala ku-rate kwamba hoja hii ni ya maana au sio ya maana, bali atatoa mawazo yake mapya na fikra mbdala bora zaidi ya hicho cha maana au kisicho cha maana jukwaani. Kinachoonekana, wengi huenda zaidi ya kitu kinachoitwa siasa.

I think,
mihemko na matusi kwenye mijadala ya kisiasa jukwaani, hua ni ishara ya wazi kabisa kwamba mwenye hali hiyo hana ufahamu wala uelewa wa kutosha juu ya kwamba siasa ni sayansi. Ingawa ni haki yake, lakini pia hayo ndio maoni yake huru, hayapaswi kusababisha jukwaa kukosa mvuto.

Binafsi,
katika siasa naona kila kinachopostiwa JF kwenye jukwaa hili la siasa kina maana. Na ikiwa hakina maana, basi huyo aliona hakina maana inafaa atoe maelezo mujarabu yaliyo bora zaidi ya hicho ambacho anaona hakina maana.

Politics is a mind game. It's all about perceptions. And you can't run away about that truth, because that's the nature of politics. And there are only two constants in politics ie are interests and betrayal. Out of that, I don't know if it can be called politics.

hiyo ya kupoteza mvuto ama laa, sidhani kama inaweza kua ni siasa, unless ni kitu kingine ambacho binafsi sikijui.

Binafsi naona hoja za wadau ni nzuri kulingana na uelewa wao, na ninadhani ni vizuri kuendelea kuenzi hoja na maandko mbalimbali ya kisiasa humu jukwaani kwa kutoa mawazo mapya na fikra mbadala bora zaidi ya hoja zenyewe zinazopostiwa jukwaani. Matusi na vinginevyo, ni maoni huru ya wahusika, but
ni muhimu zaidi vichukuliwe kama fursa ya kujirekebisha, kujisahihisha, kua wastahilivu na wenye subra ili hatimae jukwaa liwe bora zaidi mbeleni.🐒
 
Utazungumza mengi lakini chanzo ni ccm wameua utoaji wa hoja.
Zaidi ukiwapinga kwa hoja utapigwa risasi, utatekwa rejea ya polepole na lissu.
Kwa msingi huo haya ndiyo matokeo yake.
Nini kifanyike kwa mtazamo wangu nature itaamua
 
Kuna mdau kasema ni ngumu sana kujadiliana na mtu anayelipwa kutetea ugali wake. Tutawapokea namna wanavyokuja....
Sahihi kabisa, huwezi kwenda kwenye kijiwe cha wahuni ukaanza kuongea Kiingereza cha Grammar au sheria za nchi, watakuona mshamba. Na huku jukwaani sasa hivi kuna watu wanakuja kwa lengo la kuvuruga mijadala tu, hawana jipya.

Ukijidai unakaa kimya au unajibu kwa upole, wanajiona wameshinda hoja wakati wameandika pumba tupu. Kwa hiyo, mbinu ya kuwapokea kulingana na viwango vyao vya akili ndio kiboko yao. Akileta mada ya hovyo, anapewa za chembe hapo hapo mpaka akili imkae sawa.
 
N
NOOOOOOOOOOONSENSE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…