Uandishi sio mzuri mjitahidi
Kabla ya Julius Nyerere hajawa kiongozi wa TANU na hali ya siasa za Tanzania zilikua kama ifuatayo;-
Changamoto kubwa ya TAA na baadae TANU ilikuwa ni power struggle kila mtu alikua anataka awe kiongozi na hakuna mtu aliyeweza kuunganisha wanachama ambao walikua makundi makundi. Hii ilipelekea TANU kuwa na wakati mgumu sana sababu kama hamna maelewano kabla hata ya uhuru mkija kupewa nchi itakuaje
Hakuna kiongozi wa TANU aliyekua na maono mapana ya kuunganisha nchi kwani wengi wao walidhani wanadai uhuru wa Dar es Salaam, walikua na ufahamu na nchi nzima ili hawakuwapa uzito maeneo mengine ya nchi.
Changamoto lingine ni swala la udini, viongozi wa TANU walitaka nchi kuwa ya kislamu na kuongozwa kislamu kitu ambacho mkoloni alikikataa sababu walitaka mtu atakaye leta usawa kwa dini zote kumbuka kabla ya uhuru waislamu walikua asilimia 35 na wakristo 30 na ndio mara ya mwisho Tanganyika kufanya sensa kujumuisha kipengele cha dini.
Na concern kubwa sana ya mkoloni ni swala la udini sababu kuna kosa alilifanya India na Pakistani hakutaka tena lijirudie Tanzania swala la usawa kwa dini zote alilichukulia kwa uzito mkubwa sana
Mkoloni aliwapa masharti kabla hawajarudi tena ku-discuss juu ya uhuru wawe wamesha-sort out juu ya swala la uongozi kwa sharti la awe mkristo, amesoma na mwanachama hai wa TANU kwa hiyo bila kupenda ikabidi wamchague Julius Nyerere
Nyerere kuwa kiongozi wa TANU ni uamuzi wa kutokupenda kwa wapigania uhuru na ndio the only best choice ambayo ilikuwepo kunauwezekano wako ambao walikua wazuri zaidi kwa kigezo cha elimu na uongozi zaidi ya Julius Nyerere ila wengi wao walikua ni wachungaji na mapadre kwa hiyo ingewawia vigumu kuunganisha nchi
Kwa hiyo Nyerere na mapungufu yake alikua ni mtu sahihi kupewa nchi kwa mazingira ya kipindi kile
Chan...
African Association 1924 hadi TAA 1948 kufikia TANU hapakuwa na power struggle.
Sijui haya umetoa wapi.
Hiyo power struggle ilikuwa kati ya nani na nani?
TAA ilikuwa na nguvu TAA HQ New Street, Dar-es-Salaam na historia yake inafahamika.
Hapakuwa na power struggle.
Halikadhalika hali ilikuwa hivyo TAA Kanda ya Ziwa na TAA Central Province.
Hiyo kila mtu alitaka kuwa kiongozi si kweli.
Uongozi wa wakati ule ulikuwa ni kubeba majukumu hili lilikuwa jambo zito.
TANU haikupata tabu kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja.
Umoja wa Watanganyika ulitengenezwa mwaka wa 1953 Hamza Mwapachu alipotoa wazo kuwa Nyerere achaguliwe kuwa TAA President na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.
Nyerere akawa kiunganisho cha Watanganyika.
Hapa kuna kitu muhimu sana muhimu kifahamike.
Wamishionari walifanikiwa sana kwa kuwaweka waumini wao wengi nje ya harahati za siasa.
Ikawa siasa imetawaliwa zaidi na Waislam.
Kitendo cha Waislam kumchagua Nyerere kuwa Rais wa TAA kulidhihirisha kuwa TANU ina uwanja mpana wa Wakristo kujiunga na kuenea kote.
Hivi ndivyo TANU ilivyomkabili Muingereza kudai uhuru wa Tanganyika.
Tatizo la dini ukipenda tatizo la Uislam likawa limemalizwa.
Nyerere peke yake bila ya msaada wa Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, vijana wenzake Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz na Mzee John Rupia asingefika mbali.
Nyerere hakuchaguliwa kuongoza TAA kwa maelekezo ya serikali ya Uingereza.
Historia ya Julius Nyerere inafahamika kwa ushahidi uliopo katika Nyaraka za Sykes.