Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Chan...Ndo changamoto yake ana-amini ana hatimiliki ya ukweli wengine ni uongo
Hapana sina hatimiliki ya historia hii ila mimi ni sehemu ya historia hii.
Nimeitafiti na kuandika kitabu ambacho kimesahihisha historia ambayo ilidhaniwa ndiyo historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Vipi Chuo Cha CCM Kivukoni itaandika historia ya TANU Abdul Sykes asitajwe?
Baba yake ni mmoja wa waasisi waliosisi African Association na mmoja wa waliojenga ofisi ya chama hicho.
Abdul Sykes ndiye aliyempokea Julius Nyerere na akaishi na yeye alipoacha kazi ya ualimu.
Kadi yake ya TANU ni No. 3, No. 2 ni ya Ally Sykes na No. 1 ya Julius Kambarage Nyerere, Territorial President wa TANU.
Kadi ya Julius Nyerere aliyeiandika ni Ally Sykes.
Usajili wa chama cha TANU wamefanya hawa watu watatu.
Kadi 1000 za kwanza za TANU kanunua Ally Sykes kutoka mfukoni kwake.
Inakuwaje wazalendo hawa hawatajwi katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?
Mnao ukweli kushinda huu?
Mnalo jibu?
Mlango bado uko wazi na mnayo haki ya kuandika ikiwa mnaona historia niliyoandika mimi si ya kweli.
Miaka 25 imepita hakuna aliyeweza kufanya hili.
Kitabu kinakwenda chapisho la nne.
Ally Sykes na Julius Nyerere, 1958