Julius Nyerere alikuwa mtu sahihi kupewa nchi kwa mazingira ya kipindi kile

Mtu amezaliwa Nyerere kastaafu au kashafariki Leo anakuja kumlaumu Nyerere,tatizo litakuwa kwake au kwa Nyerere?
 
Viongozi wa TANU walikua wanataka tanganyika iwe islamic republic of Tanganyika bila kujali uwepo wa wakristo mkoloni akawashtukia
Uwongo,suala la nchi kuwa Islamic ni jipya hasa kwa huku Africa,limeanza miaka ya 80 baada ya watu wengi kwenda kusoma itikadi ya uwahabi Saudi Arabia,wakoloni walitaka kutoa uhuru mapema Ila kila wakiangalia watu wa uhuru ni waislam,ndiyo wakamleta Nyerere aliyeshauriwa na askofu asiwe kasisi,walitaka kumuachia 'mwenzao' kiimani
 
😂😂😂😂😂😂..Hapa mkuu naweza kukusaidi kwa nn waliongezeka kuzidi waislamu? Na kwa nn Tanzania ina watu wana majina ya utata kama unakuta mtu anaitwa Mohamed john .,Agustino Ramadhani ( Huyu ni mchungaji aliachiwa hospital ya teule pale Muheza na wakaloni)...

Ila hii bongo ishu ya udini hakuna kwa sababu licha ya viongozi wa dini kualikwa kweny mambo ya kiserikali ila hawana nguvu... Tanzania hakuna udini wala ukabila kwa tafiti zang kuna mchanganyiko mkubwa na watu wanafuata tamaduni za sehemu husika.

Tanzania baada hiyo sensa basi palikuwa na vukuto ila mpaka kufika 2005 hivi ishu ilikuwa safi.
 
Sioni sababu kubwa ya kumlaumu Nyerere.

Je sasa hivi kuna utofauti wowote?
Africa my Africa.
 

unachekww ww na matope yako kichwani!!

Hamna kiongozi anaeweza kukupa akili

ww kama unavinasaba vya ujinga pole
 
Umeandika nini?..soma tena
 
Chan...
African Association 1924 hadi TAA 1948 kufikia TANU hapakuwa na power struggle.

Sijui haya umetoa wapi.

Hiyo power struggle ilikuwa kati ya nani na nani?

TAA ilikuwa na nguvu TAA HQ New Street, Dar-es-Salaam na historia yake inafahamika.

Hapakuwa na power struggle.

Halikadhalika hali ilikuwa hivyo TAA Kanda ya Ziwa na TAA Central Province.

Hiyo kila mtu alitaka kuwa kiongozi si kweli.

Uongozi wa wakati ule ulikuwa ni kubeba majukumu hili lilikuwa jambo zito.

TANU haikupata tabu kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja.

Umoja wa Watanganyika ulitengenezwa mwaka wa 1953 Hamza Mwapachu alipotoa wazo kuwa Nyerere achaguliwe kuwa TAA President na mwaka unaofuatia 1954 TANU iundwe na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.

Nyerere akawa kiunganisho cha Watanganyika.

Hapa kuna kitu muhimu sana muhimu kifahamike.

Wamishionari walifanikiwa sana kwa kuwaweka waumini wao wengi nje ya harahati za siasa.

Ikawa siasa imetawaliwa zaidi na Waislam.

Kitendo cha Waislam kumchagua Nyerere kuwa Rais wa TAA kulidhihirisha kuwa TANU ina uwanja mpana wa Wakristo kujiunga na kuenea kote.

Hivi ndivyo TANU ilivyomkabili Muingereza kudai uhuru wa Tanganyika.

Tatizo la dini ukipenda tatizo la Uislam likawa limemalizwa.

Nyerere peke yake bila ya msaada wa Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, vijana wenzake Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz na Mzee John Rupia asingefika mbali.

Nyerere hakuchaguliwa kuongoza TAA kwa maelekezo ya serikali ya Uingereza.

Historia ya Julius Nyerere inafahamika kwa ushahidi uliopo katika Nyaraka za Sykes.
 
Changamoto ni kwamba hata wewe umeadisiwa sidhani kama kuanzia miaka ya 1930 mpaka 1950 mwishoni sidhani kama ulikua na akili timamu

Ilipata shida sababu TAA na TANU kilikua ni chama cha kislamu na mkoloni hakutaka kufanya makosa aliyofanya india na pakistani

Angeruhusu ule muundo ukabidhiwe nchi basi watu wa dini nyingine wangekua na wakati mgumu sana baada ya uhuru
 
Kuna darkside ya TANU ambayo hata wewe huwezi kuyataja sababu waliokuadisia hawakukuambia lakin haya niliyoandika kwenye uzi ni ukweli mtupu

Swala la power struggle lilikuwepo
 
Wewe mbuzi unatungatunga tu upupu kichwani mwako
 
Huyu naye watu wanataka uhuru wa nchi yeye anataka uhuru wa kabila lake alikua mbinafsi sana
Ndo mama Hadi Leo wachaga wabinafsi
 
Chan...
Sikuhadithiwa nimesoma historia ya African Association katika, "The Townsman Kleist Sykes," "Modern Tanzanians," John Iliffe, (Ed.), East African Publishing House, 1973.

Historia hii inatoka katika mswada wa kitabu alioandika Kleist Sykes kabla hajafariki 1949.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…