Julius Nyerere: Tunao wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya, heshima yao inauzwa na ina bei (mercenary)

Ni kweli Mkuu? Maana angekichapisha nchi za nje tu. Najua Ben alikuja kuwa adui vibaya sana, ugomvi ukianzia na kubinafsisha na suala la ten percent ya kubinafsisha NBC
Hivi Mzee unamfahamu vizuri Mmakonde au unamsikia ?
Jinsi Mwalimu alivyokuwa, ilikuwa siyo kawaida kuona kitu kibaya kinafanyika halafu yeye anyamaze kimya tu na kukiacha kipite. Hakuwahi kuwa mtu wa hivyo hata siku moja na angeziona kampeni za mwaka 2000 nadhani Mmakonde angeisoma nambaa: Sema bahati mbaya Mzee wetu hakufika.
 
Yaliyosemwa na Baba wa Taifa yanaonekana na yataendelea kuonekana siku zote,
 
Kweli kulikuwa na Mercenaries Congo. Mamluki kwa kiswahili kuna mmoja alikuwa anaitwa Bob Denard huyu alikuwa balaa, mara ya mwisho alikuja km sikosei Namibia sina kumbukumbu vizuri. Lkn alikuja uawa
 
Tunao wanasiasa leo hii, malaya malaya. Tunawajua. Wananunulika wanahama chama kwa pesa. Malaya malaya hawa.

Wapo, naweza kuwaweka hapa chini, wapumbavu hawa, wendawazimu. Malaya watupu hawa.
Mkuu! Malaya huwa anajiuza, hivi na anayenunua hiyo huduma anaitwaje? Sheria ya ukahaba mnunuzi nae si ana kosa?
 
Ila huyu Mzee(Nyerere) alikuwa wa kipekee RIP Mzee Julius
 
So it means we can have mercenary politicians
 
Huwa nafuatilia sana 'usia wa baba' hii hotuba TBC sijui kama waliwahi kuicheza.

Nilichogundua ni kuwa kwa sasa TBC wanacheza hotuba nyingi ambazo hatukuwahi kuzisikia, hapo nyuma walikuwa wanarudia rudia tu hotuba zake.
hii cjui kama ilishawahi chezwa!!inaonekana imeletwa kwa makusudi kutokana na hawa malaya wa kisiasa wanavyolitia hasara taifa za kurudia chaguzi kila siku.
 
Note, asante
 
Mkuu spare yourself some disappointment.
Usipende kuwaamini wala kuwategemea wanasiasa wa Tanzania.
Hasa hawa wa kizazi chetu, ndiyo kabisaaa usipoteze muda sanaaaa.
Mkuu mpaka hapa nilipofikia ktk umri huu sijawai kuwekeza imani yangu kwa mwanasiasa yoyote, wala siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa.
 
Hata mimi nimekisikiliza hicho kipindi....TBC asubuhi....nikatamani wahusika wote wangesikia.
 
huyu mzee alikua na upeo mkubwa sana wa kuona mbali. huyu wetu lit kama angekua japo na robo ya uwezo wa baba wa taifa tungefika mbali. et wanajivunia kukimbiliwa na wapinzani . huku wakiwatisha na kuwanunua. huko mbeleni kuna watu watakuja kuona aibu kubwa sana kujiita wana ccm walioshi kipindi cha JPM
 
hii cjui kama ilishawahi chezwa!!inaonekana imeletwa kwa makusudi kutokana na hawa malaya wa kisiasa wanavyolitia hasara taifa za kurudia chaguzi kila siku.
Nimesikia hotuba nyingi mpya kipindi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…