Mkuu
Nguruvi3 , kwanza niheshimu mtazamo wako, ila sii kweli wamehujumu bali wametumia different approach due to different perspectives, kwenye siasa za pragmatism, you concentrate on what is possible only.
Hii siyo pragmatism ni 'a glass half full' jambo la hatari sana.
Siasa pragmatic ni ile ya ANC na Mandela, kwamba, mwachieni Mandela bila masharti tukae mezani.
Ulinzi wa Mandela ufanywe na Makaburu ili wachukue responsibility kwa lolote au chochote.
Tusiende katika uchaguzi hadi tupate Katiba ya South Africa huru
ACT Wazanzibar hawana hiyo pragmatism, wanategemea mambo kwa 'pleasure' ya Rais kwa vile ni Mzanzibar. Wanatumaini CCM itakuwa loyal kwa SSH bila kuijua historia.
CUF walimwamini Kikwete wakitokea Zanzibar wakaungana na CCM kwenda kudai katiba mpya ya Serikali 3.
Guess what akina Pandu Kificho na Nahodha Vuai ndio walitumika na CCM 'kusafisha' njia ya kuhujumu Katiba
Chadema waliishatoa msimamo kuwa bila katiba mpya hawaingii kwenye uchaguzi!, na wakagomea mazungumzo yoyote kama sio kuhusu katiba mpya!. Sisi washauri wa bure tukashauri
Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!. wakatiliwa ndoana kwenye chambo, wakaingia wazima wazima mazima, wakakubali maridhiano na kukaa mezani, wakalambishwa asali, wakakubali kugawana nusu mkate, ila pia wakataka kuchonga malinga!, mapendekezo yao ya katiba mpya yote yakakataliwa!. Kwa watu pragmatic wanajua muda uliobaki kabla ya June 30, 2025 Bunge linapovunjwa ni less than 2 years!, huwezi kupata katiba mpya mzuri ndani ya muda huo, ila unaweza kufanya mabadiliko ya katiba and that is what is possible!. Mapendekezo yamekataliwa unasusa na kwenda kuwashitaki kwa wananchi, two years ahead of election kwa kutegemea buyu la asali ulilolambishwa na huyo unayemsusia!.
Hapa kuna nusu ukweli na nusu si ukweli.
Ukweli: Ni kwamba pressure ya Katiba mpya ilikuwa kubwa mwanzoni kiasi cha kutafutiwa njia ya kupooza.
SSH akadhani kutumia mkono wa chuma kama JPM itasaidia, akamfunga Mbowe.
Mwenyekiti akiwa magereza pressure ilikuwa kubwa nje kuliko akiwa nje. SSH akajua ' if you can't beat them you join'
SSH akabadilisha mbinu na kumtoa Mbowe Magereza. Akatumia 'ambush' ya kumwita Mbowe Ikulu hata kabla ya kukutana na wanachama wake au viongozi wenzake wa Chama. Mbowe akakurupuka kwenda
This was too low ! ilikuwa kosa ambalo Mwanasiasa mkongwe kama Mbowe hakupaswa kufanya.
Mbowe 'aliambiwa atulie' kwasababu mama ana nia njema, alirudi ndani ya cham akiwa na maridhiano mkononi.
Maridhiano aliyoyaasisi mwenyewe kwa ziara ya masaa machache na mapicha mengi. Too low
Nguvu ya kudai katiba mpya ikapungua kama si kupotea BAWACHA Vhawawezi kwenda kinyume na Mwenyekiti wao
Mbowe akaingia 18 za CCM akakabidhiwa mtaalam Kinana. Mazungumzo yasiyo na mwisho yakaendelea.
Tulimuonya Mbowe hapa JF kwamba hili ni kupoteza muda, kwa mshangao akasema hajitoi mama ana nia njema.
CCM walijua wanafanya nini, sasa hivi wanasema hakuna muda wababidilishe sheria.
Hapa CCM wana advantage, kwamba sheria wanaandika wao na Kule Dodoma vichwa wazi ni ''ndiyooo'' hata kama kama sheria ina kipengelea cha watoto wa kiume wanaozaliwa na Wapinzani wahasiwe saa 24 baad ya kuzaliwa.
Kwa mantiki hiyo sheria itakayopitisha ambayo 'mbumbu ACT Wazanzibar' wanaitegemea itapendelea CCM Zaidi.
Nitakupata scenerio moja inayotengenezwa.
Kwamba Tume ya uchaguzi itakuwa na Wajumbe kutoka vyama vya upinzani, majina yao yatapelekwa kwa Rais atakayefanya uteuzi wa Mwisho.
Kwa maneno mengine, Bw 30th aliyesaidiwa na Msajili atakuwa mjumbe akiwa na akina '' chama cha briefcase'
Dobutwa, Queen Sendega, na wengine 19 waliobeba vyama katika briefcase
Hawa ACT watapewa nafasi ya kupeleka majina, lakini Rais ndiye atachagua ya mwisho.
Kwa maneno mengine Rais atakuwa na uwezo wa kuchagua ' mkate utakaokuwa lain au maharage ya Mbeya''
Kutakuwa na kundi la viongozi wa dini kama Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni mlezi wa jumuiya ya Wazazi ya CCM. Kutakuwa na Maaskofu kama akina mzee wa kupaka na yule wa pale Kawe n.k.
Kutakuwa kundi la Wazee wa dini za asili ambao hawajawahi kushika laki 5 , wakiingia tu allowance ni laki 5 kwa siku hawa utawaambia nini kama siyo CCM mbele kwa mbele.
Halafu matokeo hayatapingwa mahakamani, huko nako kuna wale jamaa wanaosema '' Msitazame sheria inasema nini tazameni mihimili mingine inataka nini'' wakiwa na Mh wa GPA
Uchaguzi ukifanyika Wapinzania watalalamika nini? Hapa watatoa uhalali katika haramu.
'ACT Wazanzibar' wameshiriki chaguzi zote ndogoBara , hawakukushinda hata moja na kila baada ya uchaguzi wanalalamika '' rough and foul '' halafu unategemea mambo tofauti. ACT wanatueleza definition ya Insanity,
I say it unequivocally ACT Wazanzibar is insane
Lakini upumbavu mkuu wa ACT Wazanzibar niwanapotaka sheria zibadilishwe bila kubadili sheria Mama.
Hivi wakishinda halafu Rais akatoa amri ya hali ya hatari kama ilivyotokea kwa Jecha watafanya nini.
Ni afadhali Chadema waliosusia kwasababu wana kesi mbele ya Wananchi ingawaje walisha 'fumble' kuingia maridhiano bila utaratibu , dira wala ratiba.
Wanachokifanya 'ACT Wazanzibar' ni kusema kwa nguvu kwamba '' Nguruwe ni Haramu'' lakini wanaamini kwa dhati kabisa kwamba 'Mchuzi wa nguruwe ukiungwa na mdalasini, vitunguu swaumu na nyanya' uharamu wake unapungua kwasababu huyo si nguruuwe ni '' Pragmatism' anayosema
Pascal Mayalla
JokaKuu Mag3