Juma Duni "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo; ACT Tumefarijika Sana na Rais Samia Kubadili Sheria, Tunaomba Ratiba ya Utekelezaji

Juma Duni "Babu Duni" Mwenyekiti, ACT Wazalendo; ACT Tumefarijika Sana na Rais Samia Kubadili Sheria, Tunaomba Ratiba ya Utekelezaji

Huu unaitwaje ni "pandikizi" au ukosefu wa ubunifu kisiasa? Niliwahi kuandika hivi kuhusu Babu Duni:


Naamini; "Once a system always a system".
 
Naona uko vizuri kuliko hata watumishi wa Mungu wanaoishi kwa kutegemea sadaka.
Ni kweli nimekuwa mwandishi kwa miaka 30, sasa ni msataafu ila naendelea kuandika bure na kuandaa vipindi bure, kwasababu ni kitu kiko kwenye damu, naendelea kufanya uandishi na utangazaji kwa kujitolea.
P
 
Kama ni kusemwa mapandikizi, wengi pia tunaamini wanasiasa waliwahi kushika nyadhifa kubwa serikalini ni mapindikizi kwa sababu tunaamini "once a system always a system" walikula viapo hatujawaona wakifuta viapo vyao, kama kuna uwezekano huo wa kufuta kiapo, sijawahi kusikia.

Naamini OMO alikuwa ni mwanasheria mkuu wa Zanzibar
Nimekupata
P
 
Naamini; "Once a system always a system".
Kwa hivyo ndio kusema OMO ndio hao, kiukweli kabisa kwangu mimi hili ni jema, OMO akisimama 2025 akishinda anapewa, ili kumsitiri na aibu ya kushindwa, nimeshauri Dr. Mwinyi aje huku kumpokea Mama ile 2025 hivyo kule OMO apewe. Ushauri huo nimeutoa hapa Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke nimeshauri
Wanabodi
Hivyo namshauri Mama aendelee na maadalizi ya 2025 kwa kujiandaa yeye kama yeye, lakini pia afanye na maandalizi ya kuisubiria hiyo sauti ya uthibitisho kuwa 2025 yeye Rais Samia ndiye aliyepangiwa na YEYE, kama ni yeye ndiye aliyepangiwa na YEYE, then 2025 ni yeye Samia.

Lakini kama ataisikia hii sauti, sio vibaya kama atajiandaa na kumuandaa mtu wa kumpokea, kwa maoni yangu, Dr. Hussein Mwinyi atatufaa sana, hivyo namuomba Rais Samia akiisikia sauti, amuombe Dr. Hussein Mwinyi, kwa uchaguzi wa urais wa 2025 aje kugombea urais wa JMT, kuimalizia awamu yake ya pili ya Mama Samia kwa yeye kukubali kuwa rais wa JMT kwa awamu moja tuu.

Hivyo hata sauti hii niliyoisikia leo, 2022, kuhusu 2025, usikute hata Mama Samia mwenyewe bado hajui kuwa 2025 sii yeye kwasababu yeye bado hajaelezwa na YEYE kuwa sio yeye, na ndio sababu ni Rais Samia ndiye aliyependekeza 2025 twende na mgombea Mwanamke kumaanisha ni yeye!.

Unaweza kuta aliyepangiwa na YEYE kuwa rais wetu 2025 ni Mama Samia mwenyew, baada ya kuingia by default kuwa rais wa JMT kwa awamu hii ya kwanza, sasa anajipanga kuendelea awamu ya pili, properly kwa kuchaguliwa na kura za Watanzania, ila kugombea kwake ni kupitia ule mserereko wa CCM , huku Dr. Mwinyi akiji set for his second term in Zanzibar kwa mserereko wa CCM na wala hajui kuwa kuna sauti inamtaka yeye ndiye aje awe rais wa JMT, 2025!, hivyo maono kama haya, yanasaidia sana kuwaandaa watu kisaikolojia!.

Hili la Mwinyi kuja huku, sio la sauti, hili ni langu tuu, maana usikute pia ni mpango ya YEYE, kumfanya huyu jamaa Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii maana
wakati nikiandika hayo, Dr. Shein alikuwa hajui, hivyo hata saa hizi ninapoandika hapa, usikute huyu jamaa wala hajajijua kuwa yeye ndiye anapaswa aje awe rais ajaye wa Zanzibar!. Hii nikufuatia dhulma kubwa iliyokuwa ikifanyika Zanzibar kwa miaka na miaka, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda lakini sasa kwavile Samia ni mpenda haki, msema haki na mtenda haki, for the first time in Zanzibar tangu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964, uchaguzi wa 2025 unaweza kuwatendea haki!.
P
 
Ni kweli nimekuwa mwandishi kwa miaka 30, sasa ni msataafu ila naendelea kuandika bure na kuandaa vipindi bure, kwasababu ni kitu kiko kwenye damu, naendelea kufanya uandishi na utangazaji kwa kujitolea.
P
Ni vizuri kujitolea japo ni vizuri zaidi kupata malipo ambayo ungewapa si pesa taslimu wenye mahitaji waliopo kwenye kambi za wazee na watoto, nakazia si pesa taslimu.
 
Ni vizuri kujitolea japo ni vizuri zaidi kupata malipo ambayo ungewapa si pesa taslimu wenye mahitaji waliopo kwenye kambi za wazee na watoto, nakazia si pesa taslimu.
Najitolea kwasababu wahusika hawana mpango huo wa kuandaa vipindi
P
 
Pascal Mayalla, unaayaamini maneno ya mwenyekiti wa ACT Wazalendo aliyoyapokea kutoka kwa mwenyewe wa Chama Cha Mafisadi?
Mkuu Buji, Bujibuji Simba Nyamaume , wengi humu hawamjui Babu Duni, huyu sio mtu wa kulishwa maneno na kuyatapika!. Wanasiasa spoon fed ni wale waliokubali kupiga magoti kujinyenyekeza kuomba na wao wakae mezani kwenye chakula na kumegewa mkate hivyo wakakubali nusu mkate!. Niliwaeleza watu humu, hakuna mkate mgumu mbele ya chai!, mkate hata uwe mgumu vipi, mbele ya chai lazima utalainika!. Kivumbi ni pale ulipokubali kumegewa mkate ukapokea mgao, ukafufuka, ukaanza kujitutumua na kufurukuta kwa kubeza , lugha zisizo za staha, na sometimes matukano!, huo ni ukosefu wa fadhila na ukosefu wa shukrani, karma pia huwashughulikia wakosefu wa shukrani. Siasa za Kijungu Jiko, Penye Uzia, Penyeza Rupia!. Hakuna Mkate Mgumu Mbele ya Chai!, Hata Uwe Mgumu Vipi, Mbele ya Chai/Rupia, Lazima Utalainika!
P
 
Kubadili sheria ni jambo moja lkn kama katiba itabakia kuwa hii hii inayomfanya rais kuwa Mungu mtu hakutakuwa na jipya.
Not necessarily!, ukiomba kingi, au kikubwa, ukikosa, ukanyimwa, lakini ukapewa kidogo, kuwa ni mtu wa shukrani kwa kidogo hicho ili upatiwe kikubwa!.
Katiba mpya iandikwe ili rais apunguziwe madaraka. Asiteue kila kiongozi nchi hii na asiwe bosi wa kila mtu.
Naunga mkono hoja hata mimi niliwahi kushauri humu Je, Bunge letu linaendeshwa kikada? Ili tuwe na Bunge la haki, lenye uwezo wa kuisimamia Serikali Kikamilifu, kuna haja Spika asitokane na vyama?
Sheria nyingi zinavunjwa kwasabb rais yuko juu ya katiba hivyo anaweza kuparaganya kupitia wateule wake na asifanywe kitu huyo mteule kwasbb katumwa na rais aliye juu ya katiba.

Sijui mnanielewa??
Nakuelewa sana and that is what it's purported to be kuwa rais yuko juu ya katiba!. Hakuna aliye juu ya katiba, ila ni kweli kwa Tanzania, rais wetu yuko juu ya katiba!, anaivunja bila kuulizwa chochote na yeyote!, anapotokea mwandishi wa habari brave and fearless kuuliza rais wetu ametumia mamlaka gani?, anajibiwa maana ya jina lake!.
P
 
Kubadili sheria ni kitu kingine na utekelezaji ni kitu ingine kbs!!
Ni kweli kama ilivyo kwenye voting zetu, the determinate of victory is not the votes casted but the votes counted!, hivyo mwamuzi wa chaguzi zetu sio mpiga kura bali ni mwesabu kura!.

Kitu muhimu hapa ni the Political will, kwa jinsi ninavyo muona Rais Samia, ana dhamira ya kweli, tunataka tuione dhamira hiyo 2025!. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
P
 
ACT wako very strategic ila hawana mvuto kwa watu. Ukitaka kujua nenda kaangalie uchaguzi mdogo wa Mbarali, CDM hawashiriki uchaguzi wote umekosa mvuto. Hizo strategic za ACT ndio zilitakiwa impact yake ionekane kwenye chaguzi hizi.
Being strategic ni pamoja na kuzijua strong holds zako, ACT Wazalendo kabla ya ku merge, strong hold yake ilikuwa Kigoma, baada ya ku merge na CUF, strong hold yake ikawa Zanzibar na Pemba, chama chanye chance Mbeya ni Chadema, kingemteua mgombea strong halafu Sugu, Lissu, Heche, Mnowe, MNyika, Msigwa, CCM wangepenyea wapi?.
Hizo strategic za kujipendekeza kwenye mikutano ya kupotezeana muda, ndio hao wanaoandaa hiyo mikutano wanafika na kuwaambia katiba haileti maendeleo.
Jifunze kitu kinachoitwa the politics of engagement and pragmatism!. Mwalimu wa somo hilo ni huyu Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
P
 
Ni kweli kama ilivyo kwenye voting zetu, the determinate of victory is not the votes casted but the votes counted!, hivyo mwamuzi wa chaguzi zetu sio mpiga kura bali ni mwesabu kura!.

Kitu muhimu hapa ni the Political will, kwa jinsi ninavyo muona Rais Samia, ana dhamira ya kweli, tunataka tuione dhamira hiyo 2025!. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
P
Huez jiwekea mtego ili uje ukutege!!
 
Kwa suala la katiba mpya tuwe wakweli tu, kwamba Zitto na ACT Wazanzibar wamehujumu sana jitihada.
Mkuu Nguruvi3 , kwanza niheshimu mtazamo wako, ila sii kweli wamehujumu bali wametumia different approach due to different perspectives, kwenye siasa za pragmatism, you concentrate on what is possible only. Chadema waliishatoa msimamo kuwa bila katiba mpya hawaingii kwenye uchaguzi!, na wakagomea mazungumzo yoyote kama sio kuhusu katiba mpya!. Sisi washauri wa bure tukashauri Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!. wakatiliwa ndoana kwenye chambo, wakaingia wazima wazima mazima, wakakubali maridhiano na kukaa mezani, wakalambishwa asali, wakakubali kugawana nusu mkate, ila pia wakataka kuchonga malinga!, mapendekezo yao ya katiba mpya yote yakakataliwa!. Kwa watu pragmatic wanajua muda uliobaki kabla ya June 30, 2025 Bunge linapovunjwa ni less than 2 years!, huwezi kupata katiba mpya mzuri ndani ya muda huo, ila unaweza kufanya mabadiliko ya katiba and that is what is possible!. Mapendekezo yamekataliwa unasusa na kwenda kuwashitaki kwa wananchi, two years ahead of election kwa kutegemea buyu la asali ulilolambishwa na huyo unayemsusia!. Watanzania ni wapesi kukasirika na wapesi kusahau!, kufikia 2025 buyu la asali limekauka, Bandari inatema, SGR inasongesha, umeme wa JNHPP uko kwenye gridi, mradi wa LNG umeanza, bomba la mafuta on progress, Watanzania wafundishwa civic education kuvikataa vyama vikaragosi!, kuna mtu ataikumbuka Chadema?. Halafu afadhali mtu msemaovyo na anayegomba kama Magufuli, akitibuka analipuka, ogopa sana mtu mkimya dizain ya Putin!, kuna kitu nilitaka kukisema hapa Mama, I'm here to support you, to serve our country. I'm here sio tu kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu, bali pia kuutumia. But... lakini sikukisema!.
Tume huru ya uchaguzi ni upuuzi wa hali ya juu. Zitto na Duni si wanajua Zanzibar kulikuwa na tume huru ikiwa na 50/50 ya wajumbe CCM/CUF. Jecha kama mpini wa Dola aliwapiga chini CUF
Sii kweli Tume huru ya uchaguzi ni upuuzi mtupu!, ila upuuzi mtupu ni kuteua majitu majinga toka chama chao kuingia kwenye tume bila kujua wajibu wao!. CUF walikuwa hawana lolote wala sio chochote mule ni majitu majinga ajabu!. Angalia bandiko hili ni la lini Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee?. Wajumbe wa CUF ndani ya ZEC ni sifuri kabisa!, empty shells!. Sheria ya uchaguzi Zanzibar na huku bara imesema wazi kabisa maamuzi yatafikiwa kwa consensus, Mwenyekiti hapigi kura, yeye ana kura ya Mwenyekiti iwapo kura zitalingana. Sasa walimwachaje Jecha ajigeuze ZEC?. What did they do?!. CUF ina wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, what did they do?!. Niliwauliza humu, Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
Majitu majinga ya hivi ndio yamejaa kwenye vyama, serikalini, Bungeni hadi Mahakamani! Tukiunda Tume huru ya uchaguzi na tukaweka watu makini, tutafanya uchaguzi Mkuu huru na wa haki.
Huwezi kuwa na tume huru wakati sheria kama ya usalama imebadilishwa na kutoa mkono wa chuma.
Usalama wao wana deal na usalama wa nchi, ila pia hawa jamaa zetu wa sasa wengi ni empty shells tuu mule!, mimi ni product ya wazazi wangu wote wawili walikuwa watu wa kule, nimekuja kujua niko darasa la 5, tena kwa kusoma gazetini gazeti la Mzalendo, ile kesi ya mauaji Mwanza ndio kujua!. Hawa jamaa niliwahi kuwazungumza humu, TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Yale majamaa ni magoigoi ajabu!, ile 2014 nilipenyezewe hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli nikawaeleza kitu humu kumhusu mtu huyu, tungekuwa na Idara makini, wala asingefika kote kule lakini hakuna kitu pale!, ila huyu jamaa wa sasa,
View: https://youtu.be/INQFOfDufhk?si=mmczOKwJOfRQCI0I hiki ni kichwa!. Baada ya Apson sasa ndio Idara imepata mtu tena!.

Wale wengine wote kulikuwa hakuna kitu pale!, baada ya yule Blaza kuwa, watu tuna pua za kunusa kama sniffing dogs, tukanusa a danger from very far!, tukawatonya wale jamaa kupitia JF, maana humu wametamalaki!,
- Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?

it's very unfortunately, they couldn't protect him!, wenye kazi zao wakafanya yao na matokeo ndio vile!.
Kwa nguvu za ACT Wazanzibar kama wasingeshirikiana na CCM Katiba mpya ingepatikana hata December.
Kama ni katiba mpya tuu as kitabu kipya cha katiba, hata mimi tuu mwenyewe nakuandikia katiba na kwenda kukuprintia kwenye the best printer in Tanzania, Jamana, nakutolea katiba mpya within 7 days, ila itakuwa ni a constitution book without constitutionality!. Ili kupata katiba bora ambayo ni a constitution with the constitutionality sio bora katiba, it's a process yenye kupitia hatua mbalimbali mwaka mmoja hautoshi hata kwa dawa! Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio hata hivyo hilo la kufanya mabadiliko ya katiba, Mama tumemshauri Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
P
 
Mkuu just a quick question, mama watoto alikua concerned na interview zako you always use one hand. Alitaka kufahamu kama ulipata ajali ya mkono au ni mazoea tu.

Just curious and samahani if it's offensive.
No it's not offensive, its a fact, nina mkono mmoja!. Pascal Mayalla apata ajali.....
Nilipata tatizo linaloitwa brachial plexus injury. Baada ya mwaka mmoja nilipona na kurejea kwenye mic, pia nilitoa shukrani zangu humu JF Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
P
 
No it's not offensive, its a fact, nina mkono mmoja!. Pascal Mayalla apata ajali.....
Nilipata tatizo linaloitwa brachial plexus injury. Baada ya mwaka mmoja nilipona na kurejea kwenye mic, pia nilitoa shukrani zangu humu JF Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
P
Oooh pole sana mkuu, nimekumbuka ule Uzi basi tulivyosikia umetoka salama hatukufuatilia repurcussions.

It could have been worse ila Mungu alikuokoa uendelee kuisaidia jamii. Wish you more life and steady health
 
Pascal Mayalla

Wapi Wazanzibar wanadhulumiwa? Hebu tujadiliane hapa maana kuna matatizo halafu kuna upotoshaji
Kitu kitu muhimu kuliko kitu chochote kwa taifa lolote ni watu wake, na uhai wao, kitu kikubwa kuliko kitu kingine chochote ni katiba yao na , na hitaji kubwa kuliko hitaji lolote ni haki na usawa.
Nimejitolea kuwapiga watu humu darsa la katiba Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani? katiba imetoa haki fulani ambazo Watanzania wamedhumiwa.
P
 
Oooh pole sana mkuu, nimekumbuka ule Uzi basi tulivyosikia umetoka salama hatukufuatilia repurcussions.

It could have been worse ila Mungu alikuokoa uendelee kuisaidia jamii. Wish you more life and steady health
Thanks.
P
 
Mkuu Nguruvi3 , kwanza niheshimu mtazamo wako, ila sii kweli wamehujumu bali wametumia different approach due to different perspectives, kwenye siasa za pragmatism, you concentrate on what is possible only.
Hii siyo pragmatism ni 'a glass half full' jambo la hatari sana.

Siasa pragmatic ni ile ya ANC na Mandela, kwamba, mwachieni Mandela bila masharti tukae mezani.
Ulinzi wa Mandela ufanywe na Makaburu ili wachukue responsibility kwa lolote au chochote.
Tusiende katika uchaguzi hadi tupate Katiba ya South Africa huru

ACT Wazanzibar hawana hiyo pragmatism, wanategemea mambo kwa 'pleasure' ya Rais kwa vile ni Mzanzibar. Wanatumaini CCM itakuwa loyal kwa SSH bila kuijua historia.

CUF walimwamini Kikwete wakitokea Zanzibar wakaungana na CCM kwenda kudai katiba mpya ya Serikali 3.
Guess what akina Pandu Kificho na Nahodha Vuai ndio walitumika na CCM 'kusafisha' njia ya kuhujumu Katiba

Chadema waliishatoa msimamo kuwa bila katiba mpya hawaingii kwenye uchaguzi!, na wakagomea mazungumzo yoyote kama sio kuhusu katiba mpya!. Sisi washauri wa bure tukashauri Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!. wakatiliwa ndoana kwenye chambo, wakaingia wazima wazima mazima, wakakubali maridhiano na kukaa mezani, wakalambishwa asali, wakakubali kugawana nusu mkate, ila pia wakataka kuchonga malinga!, mapendekezo yao ya katiba mpya yote yakakataliwa!. Kwa watu pragmatic wanajua muda uliobaki kabla ya June 30, 2025 Bunge linapovunjwa ni less than 2 years!, huwezi kupata katiba mpya mzuri ndani ya muda huo, ila unaweza kufanya mabadiliko ya katiba and that is what is possible!. Mapendekezo yamekataliwa unasusa na kwenda kuwashitaki kwa wananchi, two years ahead of election kwa kutegemea buyu la asali ulilolambishwa na huyo unayemsusia!.
Hapa kuna nusu ukweli na nusu si ukweli.

Ukweli: Ni kwamba pressure ya Katiba mpya ilikuwa kubwa mwanzoni kiasi cha kutafutiwa njia ya kupooza.

SSH akadhani kutumia mkono wa chuma kama JPM itasaidia, akamfunga Mbowe.
Mwenyekiti akiwa magereza pressure ilikuwa kubwa nje kuliko akiwa nje. SSH akajua ' if you can't beat them you join'

SSH akabadilisha mbinu na kumtoa Mbowe Magereza. Akatumia 'ambush' ya kumwita Mbowe Ikulu hata kabla ya kukutana na wanachama wake au viongozi wenzake wa Chama. Mbowe akakurupuka kwenda
This was too low ! ilikuwa kosa ambalo Mwanasiasa mkongwe kama Mbowe hakupaswa kufanya.

Mbowe 'aliambiwa atulie' kwasababu mama ana nia njema, alirudi ndani ya cham akiwa na maridhiano mkononi.
Maridhiano aliyoyaasisi mwenyewe kwa ziara ya masaa machache na mapicha mengi. Too low

Nguvu ya kudai katiba mpya ikapungua kama si kupotea BAWACHA Vhawawezi kwenda kinyume na Mwenyekiti wao

Mbowe akaingia 18 za CCM akakabidhiwa mtaalam Kinana. Mazungumzo yasiyo na mwisho yakaendelea.

Tulimuonya Mbowe hapa JF kwamba hili ni kupoteza muda, kwa mshangao akasema hajitoi mama ana nia njema.

CCM walijua wanafanya nini, sasa hivi wanasema hakuna muda wababidilishe sheria.

Hapa CCM wana advantage, kwamba sheria wanaandika wao na Kule Dodoma vichwa wazi ni ''ndiyooo'' hata kama kama sheria ina kipengelea cha watoto wa kiume wanaozaliwa na Wapinzani wahasiwe saa 24 baad ya kuzaliwa.

Kwa mantiki hiyo sheria itakayopitisha ambayo 'mbumbu ACT Wazanzibar' wanaitegemea itapendelea CCM Zaidi.

Nitakupata scenerio moja inayotengenezwa.
Kwamba Tume ya uchaguzi itakuwa na Wajumbe kutoka vyama vya upinzani, majina yao yatapelekwa kwa Rais atakayefanya uteuzi wa Mwisho.

Kwa maneno mengine, Bw 30th aliyesaidiwa na Msajili atakuwa mjumbe akiwa na akina '' chama cha briefcase'
Dobutwa, Queen Sendega, na wengine 19 waliobeba vyama katika briefcase

Hawa ACT watapewa nafasi ya kupeleka majina, lakini Rais ndiye atachagua ya mwisho.
Kwa maneno mengine Rais atakuwa na uwezo wa kuchagua ' mkate utakaokuwa lain au maharage ya Mbeya''

Kutakuwa na kundi la viongozi wa dini kama Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni mlezi wa jumuiya ya Wazazi ya CCM. Kutakuwa na Maaskofu kama akina mzee wa kupaka na yule wa pale Kawe n.k.

Kutakuwa kundi la Wazee wa dini za asili ambao hawajawahi kushika laki 5 , wakiingia tu allowance ni laki 5 kwa siku hawa utawaambia nini kama siyo CCM mbele kwa mbele.

Halafu matokeo hayatapingwa mahakamani, huko nako kuna wale jamaa wanaosema '' Msitazame sheria inasema nini tazameni mihimili mingine inataka nini'' wakiwa na Mh wa GPA

Uchaguzi ukifanyika Wapinzania watalalamika nini? Hapa watatoa uhalali katika haramu.

'ACT Wazanzibar' wameshiriki chaguzi zote ndogoBara , hawakukushinda hata moja na kila baada ya uchaguzi wanalalamika '' rough and foul '' halafu unategemea mambo tofauti. ACT wanatueleza definition ya Insanity,
I say it unequivocally ACT Wazanzibar is insane

Lakini upumbavu mkuu wa ACT Wazanzibar niwanapotaka sheria zibadilishwe bila kubadili sheria Mama.
Hivi wakishinda halafu Rais akatoa amri ya hali ya hatari kama ilivyotokea kwa Jecha watafanya nini.

Ni afadhali Chadema waliosusia kwasababu wana kesi mbele ya Wananchi ingawaje walisha 'fumble' kuingia maridhiano bila utaratibu , dira wala ratiba.

Wanachokifanya 'ACT Wazanzibar' ni kusema kwa nguvu kwamba '' Nguruwe ni Haramu'' lakini wanaamini kwa dhati kabisa kwamba 'Mchuzi wa nguruwe ukiungwa na mdalasini, vitunguu swaumu na nyanya' uharamu wake unapungua kwasababu huyo si nguruuwe ni '' Pragmatism' anayosema Pascal Mayalla

JokaKuu Mag3








 
Kama ni katiba mpya tuu as kitabu kipya cha katiba, hata mimi tuu mwenyewe nakuandikia katiba na kwenda kukuprintia kwenye the best printer in Tanzania, Jamana, nakutolea katiba mpya within 7 days, ila itakuwa ni a constitution book without constitutionality!. Ili kupata katiba bora ambayo ni a constitution with the constitutionality sio bora katiba, it's a process yenye kupitia hatua mbalimbali mwaka mmoja hautoshi hata kwa dawa! Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio hata hivyo hilo la kufanya mabadiliko ya katiba, Mama tumemshauri Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
P
Muda upo kwa bahati mbaya kuna nia mbaya ya kupata katiba

1. Hakuna anayeeleza kwanini maoni ya Tume ya Warioba yaliyotumia mabilioni ya pesa kuzunguka nchi nzima hayafanyiwi kazi kama ' Launching pad' ya kutenegeneza Katiba

2. SSH alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kujadili maoni ya Tume ya Warioba, hivi nani yupo katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza mafanikio au matatizo ya Tume ya Warioba kuliko yeye na kwanini haelezi.

3. Kulikuwa na sababu gani za kuunda kikosi kazi, na kiliundwa kwa sheria gani ya nchi na kilifanya kazi kwa wigo gani.
Tunajua kikosi kazi cha Mkandala kilihoji watu wawili watu akina Fatma Karume , Duni ACT Wazanzibar n.k. Hivi hawa ndio Tanzania nzima?

Kama SSH angekuwa na nia njema kungekuwa hakuna haja ya kuunda kikosi kazi.

SSH anafahamu umuhimu wa Katiba kinachomtisha ni suala la Muungano.
Hizi zunguka zunguka ni kuepusha suala la Muungano.

Kwa bahati mbaya sana trick zote atakazofanya hazitazaa matunda.
Anaweza kuahirisha tatizo siku likifumuka hakuna Nyerere wa kulizuia. Tanzani ya leo si ile ya akina Wasira

Kizazi hiki kinahoji si kile cha kumeza tu. Mfano, utawasikia akina Wasira na Mpango wakisem Muungano wetu adimu na adhimu hawaelezi wala kushawishi kwanini tunahitaji Muungano na wala hawana njia za ku address matatizo ya Muungano kwasababu walimeza tu wakati huo na kisha kuamini muungano unalindwa kwa Bunduki na vitisho.
 
Back
Top Bottom