Juma Nature akataa kushiriki Wasafi Festival kisa malipo kidogo ya laki tano

Kwa Sasa necha hana soko Ndio Maana Ngoma zake za sasa haziihit mngekuwa ni wapenzi wa kweli wa mziki wake ungemsaidia kununua Ngoma zake na kuuzulia kwenye show zake
 
Hawawezi kumtangaza bila kukubaliana dau , kuna shida mahala na wala sio hyo 500K
Shida wasanii wanachukuliana poa,
Usikute walimtangaza bila makubaliano, niliwahi kusikia jux akimlalamikia harmonize kuwa kasema atakuwepo kwenye show, wakati yeye harmonize hajaongea chochote na jux.
Na ben paul pia alilalamika juu ya harmonize.
Ikaja baadae kuna msanii akimlalamikia jux kwa kitu kama hicho.
 
Nyie vitoto vya 2000 ulizeni kwanini juma huwa anawekwa wa mwisho ktk show? kuuliza sio ujinga
Kwenye malipo ya show wanaangalia jina kwanza ndio inadetermine value yako sio performance unayoenda kufanya ndio maana Kiba analipwa vizuri kwenye show kuliko Sir nature lakini kwenye performance nature amempita sana Kiba
 
Kwenye malipo ya show wanaangalia jina kwanza ndio inadetermine value yako sio performance unayoenda kufanya ndio maana Kiba analipwa vizuri kwenye show kuliko Sir nature lakini kwenye performance nature amempita sana Kiba
Umewahi kuhudhuria japo show mbili za juma. Kama umewahi utaelewa kwanini inakuwaga hivyo. Kama hujawahi huwezi kuelewa. Bye utanikausha koo bure.
 
Jay mo huwezi kumfananisha na nature hata kidogo kwasababu Jay mo anahit mpaka kwenye kizazi hichi nature soko lake lilikuwa zamani Ndio Maana latest song zake hazifanyi vizuri kwenye kizazi hichi .Waandaaji wanakuvalue kulingana na jina ulilonalo recently sio unaenda kuperform vipi jukwaani Ndio Maana Marioo huwezi kufanana kimalipo na nature Marioo lazima hela yake itakuwa ni kubwa zaidi ya nature
 
Diamond anamjua Nature vizuri. Nature mtoto wa kihuni toka Temeke kwahio masela lazma wawe shazi. Muziki wake unaakisi maisha halisi huwezi kufananisha na miziki ya Big G ya akina Mondi.
Ndio Maana diamond anapesa nyingi kuliko hata huyo asiyefanya mziki wa big G uoni huo utofauti
 
Kwahiyo kwenye matajiri 10 naye yumo? Hizi story sijui mnaziokotaga wapi dah
 
Ndio Maana diamond anapesa nyingi kuliko hata huyo asiyefanya mziki wa big G uoni huo utofauti
Kipindi cha kina Juma Nature hakukuwa na mitandao. Connection za hela zilitegemea ma promoter na baraka za Clouds fm. Bila hivyo huuzi show kwahio wamepitia ugumu kuliko hao kina Mondi.

Halafu Nature hayuko kwenye maagano ya kishirikina kama huyo Domo unaemsifia.
 
Hii sio show ya watu wenye akili sana kwamba watatumia heshima na kumbukumbu kuliko trend, mtu wa kawaida, muuza chips au bodaboda wa Morogoro mwenye miaka 24 unatarajia akiwekwa Jux hapo na akawekwa Juma Nature ataenda wapi?

Nature ana tracks kadhaa miaka hii mitano iliyopita, kuna ngoma yeyote ina viewers hata 200k YouTube? Wakati huo hayupo streaming platforms sasa mashabiki zake wengi wanamsikiliza kupitia wapi? Muda huo tulinganishe na ngoma za wabana pua wanaotrend hawakosi viewers za millions. Sasa kama unaandaa show ya rika hili la kurushiana vumbi unafanyaje hapo. Ushahidi wa kwamba Nature anauza unaupata wapi, unabaki na ushahidi kwamba aliwahi uza na ana fanbase yake ambayo sio hii ya Fiesta au Wasafi Festival.
 
mtaaram unaongea pwent sana.sema kunipqngishq ile salun miez 6 ya mqjaljbio ya biashara ndio umekataa mkuu
 
 
Kwa majukwaani bado sir nature ana uwezo wa hali ya juu mno ambao haujafikiwa na msanii yoyote yule.

Nature ni legend ila kiwango kikubwa cha hadhira ya sasa sokoni hakimpi nafasi ya kuwa na thamani hiyo mnayojaribu kumpa.

Huu ni ukweli wa kibiashara, kama tutaamua kuweka mapenzi na hisia pembeni.
 
Juma nature na watu kama kina inspector kwa mtu wa kale kama mimi tunaweza mtazama na kumlipa akiitisha shoo sababu nyimbo kama ugali, mzee wa busara tulizisikiliza sema ndo hivyo kuna umri huwezi fikiria matamasha na disko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…