Juma Nature kama muziki umekushinda tafuta kazi nyingine, usichafue watu

Juma Nature kama muziki umekushinda tafuta kazi nyingine, usichafue watu

Unawajua nje ndani ukiwa km nani? We Jamaa una akili wewe kweli unamjua Nature nje ndani amekuoa wewe mkewe amekuzalisha?
Jamaa Kila msanii anamjua yeye na maisha yake ,msanii yoyote akiwa upande wa Wasafi anamtetea akitoka Wasafi anakua mbaya anamponda mbayaa
 
We Jamaa huyo mtu usimchukulie poa anamiliki maekari ya mashamba ya KOROSHO huko Ntwara, punguza shobo mtoto wa kiume
Badae aking'atwa mbu muanze kutembeza bakuli la michango
 
Yaani show in endorsement za makampuni 10+ ukijumlisha na hela ya viingilio alafu mje kulipa watu 500k, Hii bongo ya ajabu sana mnapenda kutengeneza watu maarufu wenye majina ila hawana pesa. Huyo kwevo mbona aligombana na mawingu kutokana na suala kama hili la malipo dusko
 
Nature anatuletea....ngebe, ngita.na ghadhabu za jirani yetu mtani..ba mtu mbishi baache kama alivyo.....ajue HILI GAME ,GAME TOUGH
 
Wewe ndio unatakiwa utafute kazi nyingine kuliko hii ya uchawa wa WCB
Muache Legendary Juma Nature aishi maisha aliyo yachagua.
Cha ajabu uchawa wake hautumii vizuri, machawa wa faida kina mwijaku, manala,baba levo, baada afanye mziki alipwe hata hiyo laki tano, au hata kupata jina mjini tu, litakusaidia mbele.
 
Sijui kwanini lawama anapewa huyu jamaa while alie andika ni Rich one. Tuna muonea bure tu huyu mlevi
 
Ingawa wewe Chawa ni mtu wa kupuuzwa ila katika hili la Nature nakuunga mkono. Kuna wapumbavu wanaodai Nature ni legend anatakiwa alipwe zaidi... hawa hawana hoja kabisa. Kwenye biashara ya muziki kinachoangaliwa ni nani anakubalika sokoni kwa wakati huu na sio zilipendwa. Hata kwenye soka kwa sasa huko Ulaya hawawezi msajili Messi au Ronaldo wakati kuna damu changa zipo kasi. Nature anaheshimika ila huu sio wakati wake. Hiyo laki 5 ni nyingi sana kwake pia ni upendeleo. Wengi wenu mnaompinga mleta uzi hamjui ugumu uliopo wa kuandaa tamasha.. huwa hilo jambo lina mambo mengi mno.. huyo Diamond nahisi ni jini kwasababu atakuwa halali kupambania hilo jambo.
 
Ulitaka Akae kimya? Ulitaka Aeleweke vipi na watu Kutuhudhuria kwenye show ulitaka aseme uongo ili kumfurahisha nani? Wakati ufike Watu waache uoga na wauseme ukweli no matter what...
Hata Diamond kipind anaamza alikataa sana show za Laki tano na milion Milion na akafanikiwa kuwepo hapo alipo...
Legend Kama J.nature kumpa laki Tano kwenye show ni Tusi tena kubwa na nakubaliana naye na amesema ili Watu wasije wakamchafua Aonekane hajaonekana kwa na kala pesa za watu....
Nakazia
 
Kwani wee chawa wa WCB, unadhani kila mtu ana msujudia huyo domokayaa wako? Ukimsujudia wee inatoshaaa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hujistukiiii?
 
We Sinza la Masinza Pazuri...

Kwa hiyo njaa za Juma Nature ndiyo afanye show kwa Laki Tano? Unajua show za Sir Nature Kibra vizuri kweli wewe?Au ndiyo umezaliwa kwenye kizazi cha Amapiano

Shida Isiwe sababu ya kumkandamiza mtu...Hata wewe ujifunze kwa Nature...
Hapo sasa.
 
Back
Top Bottom