Juma Nature ndio best storyteller wa muda wote Bongo. Wasanii wachanga mnao-rap jifunzeni kwa Juma Nature

[emoji441][emoji441][emoji443][emoji443]nashangaa!! Nashangaa!! Nikimuonaaaa[emoji443][emoji443][emoji441][emoji441]

Nakumbuka kibwagizo cha nyimbo hii ya juma nature
Lakini nyimbo siikumbuki.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Hii ni Mandojo na domo Ft Nature
 
Umenikumbisha jinsi Nature alivyokamua kibwagizo cha Wimbo wa Zali la Mentali wa Professor Jay...

Nature alikuwa msanii noma sana....
 
Mack D ft Banana - Jumba bovu
OCD - Kazeze
JCee ft Q Chief - Mpiga Debe n.k
 
Ngojea nimalizie kuzisikiliza album ya
Nikki mbishi-sauti Ya jogoo
Mwingi wa habari-Pmawenge
African son-sterio singasinga
Verteller-Dizasta vina
Taleta ushuhuda wa shahidi-wa Dizasta alivyo shuhudia meli ikienda mlama.
 
Jay Moe ndio best story teller wa muda wote.
 
Samahani! Kila msanii afanye singeli au amapiano kwa kuwa ndio inakimbiza!? Kama ni hivyo, nini maana ya ubunifu katika sanaa kama kila msanii atakuwa copy ya msanii mwingine!?
 
Jay Moe ndio best story teller wa muda wote.
Jay mo NI mkali pia wa storytelling nyimbo zake nilizozikubali ni
Story tatu
Mvua na jua
Maisha ya boarding

Lakini unaposema WA muda wote unakosea binafsi professor jay alikua balaa

Ndio mzee
Nang'atuka
Nikusaidiaje
Chemsha bongo
Msinitenge
 
Ukimtaja Nature hunabudi kunegesha stori kwa kumtaja Inspekta Haruni

Hawa miamba ndio waliishusha hip hop chini uswahilini na mtaa wakawaelewa

Ukiachana na storytelling hawa jamaa walikua mafundi wa wordplay
Enzi hizo wanahip hop ulikua unyamwezi mwingi na english lakini hawa jamaa walikua wanacheza na maneno flani hivi ya uswazi ndani ndani na kuleta ladha ya aina yake
Hebu sikiliza Mzee wa Busara remix kasimama Nature na Inspekta utanielewa

Msikilize Inspekta kwenye mtoto wa getikali kisha msikilize Nature kwenye nipo gado alioshirikishwa na zay b
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…