Feisal2020
JF-Expert Member
- Nov 15, 2018
- 1,113
- 2,656
Mkuu sanaa ni pana sana, haiko hivyo unavyofikiria... Huo uandishi na uwasilishaji wa Dizasta una hadhira yake na ndio maana mpaka leo bado anafanya hicho anachokifanya... Dizasta ni moja kati ya MCs wachache ambao uwasilishaji wao umebaki vilevile bila kuyumbishwa na kelele za akina nyie ambao mnapiga mayowe kuwa wasanii wa hivyo wabadirike kufuata soko.Yule ni mwandishi wa vitabu talent yake ipo uko, huu ni muziki uwezi kutuletea manyimbo yana part 1 mpaka part 8 ukimsikiliza kama unaperuzi kurasa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sikiliza maisha ya boarding ya JMo au Mikasi ya Ngwea ukafundishe watunza misingi ni nini storytelling.
Hoja yako ya kusema ngoma zake zina part 1 mpaka 8 ukimsikiliza kama unaperuzi kurasa... Kuna ubaya gani kufanya hivyo? Au ubongo wako mdogo hupendi kuperuzi kurasa? Kwanza inabidi ujue kuwa mziki wa HipHop una nguzo zake, na mojawapo ya nguzo muhimu zaidi ni "Knowledge" nguzo ambayo siku hizi imekua underrated sana kutokana na mziki kuingiliwa na watoto waimba ngono, pombe na mademu sana kuliko maarifa, Dizasta kaamua kubaki huko.
Hiyo style ya kufanya ngoma kwa series sio ngeni kwenye fasihi, asili yake ni Medieval Literature (ya Ulaya) ila kwenye rap game bongo imekua introduced na Dizasta na wadogo zake katika game hawajaiona hiyo kuwa ni mbaya na ndomana Maarifa akatoa series ya MAARIFA YA MAARIFA, Rapcha akatoa series ya LISSA, Young Killer SINAGA SWAGA baada ya kuwa inspired na Dizasta.