DIZASTA VINA ANASIKILIZWA KWENYE WHATSAPP?
Mkuu nisaidie na mimi hapo
Sinaga muda wa kudownload nyimbo ila huwa nazisikia kwenye Tv/Radio na sehemu za starehe
Mfano tuchukulie wana Hip Hop wa zama hizi
Ngoma kama Wapolo, am leaving my life, Si wanataka kubang 😂😂, Maisha na Muziki, na nyimbo za Mcs kibao kama Young Lunya, msodoki nk nk zikitoka tu utazisikia radio na kwenye tv muda wote, ukipanda bajaji au dalala utazisikia, ukienda club ndio usiseme, ukiingia saluni au simu za vijana utazikuta, ukienda youtube unakuta viewers 1m+
Ukija sasa kwa hawa Mcs ambao wanasifiwa sana sana humu JF kama Akina Dizasta, Nikki Mbishi, Rapcha. nk nk nyimbo zao huwa zinapigwa wapi? Hazisikiki radioni au kwa uchache sana ukitoka, huzi sikii club, bajaji, saloon, wala kusikia labda Rapcha ana shows mikoani nk
Ukienda youtube unakuta viewers wachache sana
Cha ajabu ni kwamba wala nyimbo zao hazina matusi sana kama kabda za Lunya
Ukitembelea page zao sasa unakuta wana wafuasi wachache lakini wanavyo wanwagia sifa ni balaa
Na wengi wao kazi yao ni kupost kuponda akina Lunya na wengine wanaokimbiza mainstream
Na wengi wao wanauza nyimbo zao kwa Whatsap
Tatizo ni nini
Nahisi kunatatizo kwa hawa jamaa
Ndio maana wengi tunaona wanasikilizwa Whatsap
Kwa mtu kama mimi ambaye sina muda wa kudownload nyimbo nategemea Media zipige ndio niujue wimbo na kuupenda au la, hawa jamaa hawana nafasi kwangu
Trust me mkuu hivi ndivyo soko la muziki lilivyo........ kuusikia wimbo kwenye media kisha unakua mkubwa
Sisemi kama hawajui kuimba, hapana
Ila post hii wanachakujifunza, Enzi hizo Mcs walikua wasomi au walioishi mbele kama kundi la KWANZA UNITY, Nature alichofanya aka connect na uswazi wake watu wakamuelewa..... alikimbiza vibaya sana
Ni lazima ujue pia hadhira yako inataka nini badala ya kukomaa na culture ambayo hata wamarekani wenyewe imewashinda