JWTZ badilikeni, dunia ya sasa hakuna vita ya kuvunja matofali kwa kichwa!

Vipi kwenye "Special Mission" ....watumie vifaru na mizinga pia??.

Ulipita hata mgambo kweli??

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app

Mkuu special mission ya jeshi la merikani kumteka ama kumua Osama bin Laden, hawakutumia karate, wala uvunjaji wa matofali kwa kichwa, ilihusisha vifaa vya technologia ya kisasa ujuzi na usahihi wa hali ya juu, unao hitaji akili nyingi zaidi ya mabavu.
 
Hakuna technically exhibition imewahi fanya na jw kubwa zaid ya gar za nyumbu ww

wahafidhina wa jwtz wakisikia hivi wanatamani wakutafute wakuuwe.....ila huo ndio ukweli.

nimehudhuria exhibition zote za sabasaba na banda ninalopenda kulitembelea ni la wizara ya ulinzi ambalo ndani yake unawakuta jwtz wakionyesha zana zao mbalimbali na journals zinazozungumzia historia ya jeshi na mafanikio yake.

sijawahi kuona waki exhibit teknolojia yoyote ya kisasa ambayo jeshi limewahi kuivumbua.

kitu unique ambacho nimewahi kukiona kwenye banda la jwtz ni wale makomando wao wawili wakiwa wamesimama huku wamevaa begi kubwa ambalo wao wenyewe wanadai ni zito sana.[emoji16][emoji16][emoji16]
 
kweli teknolojia ilitumika kwa asilimia kubwa kufuatilia nyendo zake zote katika makazi yake ila bado haikutosha ikabidi Marekani wapeleke undercover agents ambao waliendesha zoezi la kutoa huduma ya chanjo kama sikosei mtaa mzima anaoishi Osama ila lengo kuu ilikuwa kuweza ku penetrate ndani kwa Osama na kujua zaidi kuhusu makazi yake
pia baada ya satellite na drone za Marekani kufuatilia kila hatua na kujiridhisha kufanya uvamizi walipelekwa maaskari wa kikosi maalum na wakati wanakaribia wakapata ajali, kufupisha hadithi ni kuwa kikosi maalum ndo kiliingia kwenye makazi ya Osama, kupambana na vikwazo vya walinzi wa Osama na hatimae kumuua na kuondoka na mwili wake pasipo nchi mwenyeji kufahamu.
Nina hakika ingetumika teknolojia pekee kama ilivyotumika shambulio la drone kwa Generali wa Iran inawezekana ingepelekea vita au kutokuelewana baina ya mataifa hayo ila kikosi maalumu kilitumika pasipo kuacha alama yeyote ya ushahidi nyuma hii ndo maana halisi ya "special force"
 
Mkuu iyo teknolojia ya kulinda anga ina uzwa ni fedhaa tu. Ata mwaka jana taifa kubwa la Turkey walinunua mitambo ya warusi .

Cha msingi ni kuwa na elimu iliyo bora
Facts, elimu muhimu sana. Sana sasa kwenye utumizi wa vifaa vya ki military modernized sahi, hadi uwe umeisomea undani hadi nje wa mashine hizo, sio kitoto pale! 🀣
 
Kwa hyo mleta mada unadhan kuna siku TZ itaingia vita na ISRAELI au MAREKANI KWELI?

Adui wa kwanza ni jirani yako,hivyo lzm ujiimarishe kulingana na jirani yako alivyo ie Kenya,Uganda na Nchi nyngne zinazotuzunguka!!
Mmarekani alishambuliwa na Alqaeda wa Afghanistan na Iraq huko, na yeye kwa kujibu kipigo akawafuata kwao kuwachapia home ground hadi leo hii ndio wanatolewa. So military modernization ni muhimu, sio lazma jirani yako awe adui ndio uanze kujihami, No! Hata waweza kuwa unatoa msaada wa kielimu kwa majeshi ya nchi zingine ukiwa wewe uko far kwenye nyanja hiyo, au hata kusaidia kataki peace keeping missions kibao tu ju uko na experience ya kutosha with the new tech in town na uko advanced military wise.
 
Mtu yuko mbali ndani ya container, kambini haswa, anakufwata hadi kwako na kukuachia kombora kutoka kwa drone zile za kisasa alafu hicho kinarudishwa kilipotoka. Wewe huku ushalizwa na hasara juu. Jamaa anaenda kunywa chai sasa, Duh. Technology muhimu
 
Eti alambwe makofi?? Duh πŸ˜πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜­πŸ˜€
 
Ujinga mzigo

Kwa hiyo mfano ukiwa mwanajeshi uko doria mtaani akija akija kibaka kwa nyuma yako akakukaba utabonyeza computer? kuumchomoa kwenye shingo yako kiteknolojia mjinga wewe?
Anaongelea vita na nchi nyingine, sio one on one mkuu! 🀣
 
Mazoezi hayaachwi kamwe popote pale duniani kwenye vikundi hivi. Alafu ujue kuna nchi zilizoendelea mfano Uarabuni hata Uzunguni hao majambazi unasema wanadakwa rahisi kupitia technology tu. Vitu vinatumika toka kitambo mkuu, sio movie! 🀣
 
Vita ya ardhini unafikiri unapigana wapi? MIJINI UTAINGIA mitaani pia.Au uNAFIKIRI VITA NI angani tu ? Unatekaje miji bila kushuka ardhini na kuingia mitaani na vichochoroni kwenye watu wengi?
Hata hivyo vita vya ardhini pia tech inavihusu, kuanzia tanks, mortars, rpg Guided Multiple Launch Rocket System nk vyote hivyo vinaundwa vipya kila kukicha. Huwezi niambia utashinda vita ukiwa na ka bunduki ka kitambo au tank zee, hiyo nayo itakuwa ngumu.
 
Ni kama zile F-22 Raptor walizoundiwa na Lockheed Martin Aeronautics, hizo pia hazikuuzwa nje ya USA. Ilipotolewa F-35 ambayo Israel walinunua pia. Wakati F-22 walinyimwa na urafiki wote huu. Haha chezea tech, muhimu sana kwenye nyanja tofauti tofauti za nchi.
 
At the end of the day, tech wins ata mkipatana head on!
 
Mabomu mabaya yale yanayotoka baharini lile likituwa moja basi magomeni yote flat, likija lingine Ilala yote flat ziko silaha hawa jamaa wakizitumia wanakurudisha miaka 40 nyuma.
Kabisa, alafu unasikia mtu akisema Tech sio muhimu. Haha
 
Physical and mental fitness ni foundation ya lazima ndani ya jeshi. Huko utapitia tu siku utakuwa enrolled. Hapa ni military tech advancement tunajadili.
Umeongelea kurusha bomu la mkono, sasa wewe uko mbali na bomu lako la mkono, mwenzako kule mbali ana Rocket Propelled Grenade (RPG) au zile Advanced Lightweight Grenade (ALG) Launcher, kumbuka hiyo ni tech imetumika kuitengeza kuanzia design yake hadi efficiency yake. Nani anapasuliwa hapo, wewe!



{A soldier demonstrates firing positions on the Mk 47 Striker}

Kuhusu Pistols na tech, ziko zenye kutumia finger print ya mtu mmoja pekee, na hiyo yote ni kuzuia hasara wakati umenyang'anywa bahati mbaya, mhuni hatoweza kuitumia hata aje na ndumba πŸ˜‚, wewe tu ndio unaweza sababu tu ya print yako, hivi hapo hujaokoka maisha yako ama?
{The $400 Intelligun by Kodiak Industries lets you lock and unlock a gun with your fingerprint, the way you’d open an iPhone.}

Kuvuka mito yenye Mamba sio πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, haya bhana, tech iko hapo pia, kuna machine inaitwa armoured vehicle-launched bridge (AVLB), hiyo ni gari na inaweza kuji convert kuwa bridge na magari ya kijeshi hata tanks kupita juu yake na kuvuka pande ya pili, hiyo nayo tech + engineering inahusika hapo.
{A Biber AVLB of the German Army using its own bridge}

{An M60A1 Armored Vehicle Launched Bridge, deploying its scissors-type bridge.}

{An M60 AVLB deploying its bridge on the banks of Lahn RIVER.}

{A Slovak AM-50 laying a fast bridge over the Torysa}


Kuhitimisha ni kwamba, ndo maana unaona nchi nyingi developed, military training yao hawa base sana kwa misuli, ni akili na tech + endurance kwa kila hali, penye kutumia nguvu wanarekebisha na PT nyingi, jamaa wanakuwa physicali all day everyday. Unaweza kuta kijana mwembamba ila hatari kupindukia sababu ana training ya kinyama, akili tech kila kitu ka fundishwa yaani akiingia pahali anasababisha hasara utadhani umevamiwa na kikundi kumbe timu tu ya mtu nne au tano lakini unatoa chenji kwao. Tech ndio future, misuli kiasi ndo usiwe bwege hata kujisaidia uwe unaweza.
{MTU-20 bridge layer}

{EWK-Gillois amphibious bridging vehicle}

{German M3 amphibious bridging vehicles}
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…