JWTZ ifanye uchunguzi dhidi ya tabia na mwenendo wa askari wake Denis Urio

Hiyo ni fursa kwa Mbowe.
Nimejifunza kuna wakati Mungu huruhusu mabaya yakukute ili Ajitukuze kwako.
Naifurahia sana amani ya Mbowe, haonyeshi kujuta, amejaa tabasamu.
Hakika atashinda.
Ushindi mwindi mwingine hukamilishwa na vifungo, vipigo na maonevu.
Yakamilikapo mateso ndipo Shujaa na Mzee wa siku hushuka na kuishangaza dunia.
Yeye hajawahi shindwa.
Huujua mwisho kabla ya mwisho.
 

Sisi sio wanasheria ila tuna logic. Hayo ya kujifanya kuna mbinu za kisheria mnazibeba nyinyi mliotunga hii kesi. Hata kama mkimlazimisha jaji huyu kuwafichia aibu, bado kwenye mahakama ya rufaa itakuwa ni dakika chache tu ukweli wote utawekwa wazi.
 

He is just a victim Kama wenzake in a different side...
 
Mpaka bapa ilipofika ni kuwa Urio anaelekea kupoteza kazi yake. Hakuna namna ambavyo jeshi linaweza kumuaxha salama. Huyu ameshajiharibia.
 
Chadema mnajitahidi sana kupotosha ili gaidi asifungwe lakini hamtafanikiwa.

Denis Urio alipewa ruhusa na DCI aendelee kusbirikiana na Mbowe ili mradi tu awe anatoa taarifa ya kila kitu kinachoendelea.
Personally, Urio na DCI wamewasababishia sana mateso wenzake(makomandoo), hii dhambi haitawaacha salama Daima.

Ivi ilihitaji kuendelea kutafuta watu wa kuwatesa ili wamuwajibishe Mbowe! Kweli?
 
Mpaka bapa ilipofika ni kuwa Urio anaelekea kupoteza kazi yake. Hakuna namna ambavyo jeshi linaweza kumuaxha salama. Huyu ameshajiharibia.
Hii ni Tanzania baba usijekushangaa flani anaagiza apandishwe cheo.
 
Ukute baba yake denis ndiyo baba yake mbowe yaani baba wa taifa
 
He is just a victim Kama wenzake in a different side...
How bro?
Unataka kusema DCI alimlazimisha kula njama baada ya kugundua ana ukaribu na Mbowe?
Kama alilazimishwa, je aliripoti jeshini kwa wakubwa zake?
Kwangu mimi bora uniue kuliko kunilaximisha nimsingizie mtu mwingine.
Na tena ningeusema ukweli wote mahakamani ilovyokuwa regardless yatakayonipata.
Hakuna kitu kibaya kama kuhukumiwa na mahakama ya moyo wako...utakufa kwa sonono.
 
Una matatizo kichwani mwako,issue hapa ni responsibility iliyopo kwa taasisi hizi kufanya kazi zake kwa mujibu wa kisheria,urio ni mwajiriwa wa tpdf ilikua ni wajibu wake kuwasiliana na MI na SIO DCI.Mh.Mbowe issue yake itaamuliwa na judge anayesikiliza case yake,sio wewe ambaye tayari una uamuzi wa Mh.Mbowe eti kakosea,middle class wewe ni sehemu ya tatizo kubwa ambao Tanzania inakabiliana nalo,elimu mbovu matokeo ya shule za ajabu na mfumo ovyo wa kielimu.
 
Shahidi wenu muhimu ni huyu urio na huyu anapuyanga tu hana lolote analolijua sasa nenda na wewe ukapeleke uthibitisho urio hana
 
Mfafanulie hiyo MI kuwa ni Military intelligence huyo kilazzer
 
Sasa hayo unasema wewe.
Nenda wewe Basi kawasiliane na MI.
Hamjiulizi chat,calls,na miamala ya fedha viliingia vipi kwenye simu ya kamanda urio?

Kesi ya msingi ndo ipo hapo.
Sio wapi alikwenda kutoa taarifa.
Mkishajua hivyo vitu vimetendeka vipi ndio mtajua ukweli Kama mbowe alihusika kupanga hyo mipango au ametengenezewa.
Kwa hyo ishu sio kamanda urio amekwenda kuripoti wapi.
Ishu ni kweli mbowe alimtafuta urio? alikuwa anampigia simu?alikuwa anachat naye?
Akipanga mipango yoyotte na urio?
Kesi ya msingi ndipo IPO hapo mtaelimika lini nyie?
 
Mfafanulie hiyo MI kuwa ni Military intelligence huyo kilazzer
Na hiyo ndio inayokusanya zote kutoka URAIANI, nje ya mipaka na ndani ya mipaka. Na ndio unafanya situation analysis ya kuamua wafanye nini
 
Hili jambo limeshughulikiwa na watu wajinga sana.
Kama Mbowe alikuwa na mipango hiyo, wangeendelea kufuatilia mpaka upatikane ushahidi wa kutosha. Wakikosa waliache kimya kimya.
Pia wangeendelea kutafuta watu wenye akili wafuatilie.
 

Usiongee tu kirahisi, haijalishi Ni jeshi gani, we have the same president and one political part "Ccm" Huyu Ni victim tu! Ni WA kuombea wala sio kusimangwa!
 
Tatizo linaloonekana wanakosa huo ushahidi. Labda wamewahi kabla ya kupata ushahidi wa kutosha au wameutafuta kijinga.
 

Hawatafanya lolote kwa sababu inawezekana pia askari wao huyu ametumwa na JW kufanya aliyofanya. Kila taasisi imepangwa kutoa ushahidi wa uongo kwenye hii kesi.

Ni aibu sana jeshi kujiingiza kwenye hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…