Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Hii kesi inayoendelea mahakamani imeufungua macho umma wa Watanzania juu ya tabia ya askari huyo.
Aina ya Ushahidi ambao komando Urio ameutoa mahakamani umeacha maswali mengi sana ya umma juu ya tabia ya askari huyu lakini pia hata kuathiri taswira ya jeshi mbele ya umma.
Kuna haya mambo yafuatayo:
1. Je, jeshi lina taarifa za askari wake Denis Urio kumtafutia Mbowe walinzi ambao yeye Urio anasema walipanga kufanya uhaini? Hata hivyo mahakamani Urio kasema hakuripoti Jeshini bali karipoti kwrnye mamlaka ya kipolisi. Je, hivi ndivyo askari wa JWTZ anavyopaswa kufanya pindi anapopata taarifa za uhaini?
2. Ushahidi wa Urio una matobo mengi, kuna kila sababu ya kudhani kuwa Urio anatoa ushahidi wa uwongo ili kuwaumiza raia wasio na hatia–Hapa JWTZ haina budi kufanya uchunguzi binafsi na kujiridhisha juu ya mwenendo na tabia za askari wake huyu Denis Urio
3. Mbele ya jamii ni vigumu kwa JWTZ kujiweka pembeni katika hii kesi kwa sababu, wananchi wanapata taswira mbaya kuwa JW inatumika kisiasa kuumiza wapinzani. Kwa hiyo ipo haja kwa JWTZ kujisafisha dhidi ya tabia na mwenendo wa Denis Urio kama ulivyothibitika katika ushahidi anaoutoa mahakamani.