Low IQ, Majeshi mengi Duniani hufanya IQ testing kabla ya kuajiriwa Jeshini lkn Tanzania hakuna IQ testing matokeo yake ndiyo hayo Una Jeshi ambalo halijui hata jukumu lake ni lipi, hawajui hata kazi yao katika nchi ni ipi wanaishi kuleta ubabe kwa dala dala kwa raia wakati wamekuwa trained kuilinda nchi.
Mimi nimetembea nchi nyingi hata za Kiafrika hata hapo Kenya tu huwezi kuona Mwanajeshi anazurura mjini ukiona Mwanajeshi mjini wako kwenye gari na wana kitu wanafanya wakimaliza wanatokeamea hawana stori na mtu raia, Tanzania kila siku ugomvi na raia wanagombania wanawake, wakitoka mafunzoni wanaingia mtaani kupiga raia ambao walipaswa kuwalinda …
Tanzania ndio nchi pekee ambayo maswala ya akili hayajapewa kipaumbele.
Angalia tu mfano mdogo wakina Mwijaku na wenzake ambao ndio Machawa.
Hawa ndio wanaokubalika na ndio wenye nguvu kubwa ya ushawishi na serikali ndio inawatumia hawa kwenye propaganda zao.
Mfano leo hii upinzani wakaitisha mkutano Kariakoo kuelezea ubovu wa mkataba wa bandari kupitia vifungu vya katiba.
Serikali inaweza kuwatuma Mwijaku na Babalevo waende Kariakoo hapo hapo kufanya promosheni za kuwasifia Dp Wrld.
Si ajabu ukashuhudia wimbi la watu wengi wakajitokeza kuwatazama kina Mwijaku na Babalevo halafu mkutano wa kupinga mkataba ukakosa wahudhuriaji
Wale watu wote ambao ni conscious huwa hawafuatiliwi, jamii imewatenga wako isolated
Mawazo yao ambayo yanatija hayasikilizwi, ni watu ambao wanapuuzwa na kuchukuliwa poa kirahisi mno.
Kwasababu utamaduni tuliofikia sasa kama nchi ni kuwa watu hawapendi kuumiza kichwa kufanya tafakuri ya vitu.
Na ndio sababu watu hawa wenye akili waliopaswa kuwa asset wamejikuta wamepoteza ushawishi na kushindwa kukubalika.
Njoo kwenye mziki.
Leo hii hata uje na ngoma gani ambayo ni kali na yenye mafunzo lakini raia wataiacha yako watasikiliza "haaniiiiiiii"
Sasa unapokuja kwenye jeshi huko ndio kuna vituko.
Ukiachana na swala la kupeana shavu kwasababu ya undugu lakini jeshini kuna watu wanaweza kuajiriwa kwasababu wamejazia tu misuli.