JWTZ kuwatesa raia wanaovaa nguo za Jeshi ni ukatili

Pana wajinga wanatamani kuajiriwa Jeshini kwa ajili ya kutesa watu na ndio Taifa lilipofikia huko hizi mambo sijui ya usipige picha hapa au mambo ya nguo ni mambo ya kizamani sana...unakuta wanawatesa Raia waliopiga picha eneo lao wakati kila kitu kipo kwenye Satellite ni ujinga sana...
 
Mi nakuunga mkono, sikupingi
 
Hili kundi wengi ni Iron Boy,unakuta hata mtoa tamko ni Iron boy.Unategemea nn?Yaani wanashindwa kudeal na mambo ya msingi wanaangaika na sare eti zimefanana na jeshi.
 
Hili kundi wengi ni Iron Boy,unakuta hata mtoa tamko ni Iron boy.Unategemea nn?Yaani wanashindwa kudeal na mambo ya msingi wanaangaika na sare eti zimefanana na jeshi.
Hujui jeshi wewe...hujawahi kulijua
 
Na yeye kila siku wanakataza alivaa ya nini kujitafutia shida tu, mtu hata mgambo sizani kama alienda waachie wenyewe wayavae.

Avae hata ya polisi au magereza tu
 
Hiyo sababu haihalalishi huu ukatili wa kutesa mwananchi eti kisa wewe ni mwanajeshi, kama kweli wanataka hizo battle wakwende somalia huko wakakutane na maharamia waliopinda akili wapelekeane moto.
 
Haya mambo wananchi wenyewe ndio wanayashabikia,watu wanaona sawa tu askari akifanya hivyo sababu hata ukisikia mtu anavyosimulia unajua kabisa anaenjoy
 
Hivi huyo akifanya kosa halafu raia wakamuona na asikamatwe si watasema ni mwanajeshi? Nakumbuka hata tukiwa tulikuwa hatukatizi kwenye makambi yao labda kama umevaa nguo za shule lakini si vinginevyo
 
Kuna mambo ya ajabu sana yanafanyika hapa nchini...
Sifa za kijinga tu na siungi mkono hili

Ila kwa upande mwingine tujiulize:

Ni kwanini Raia avae nguo za jeshi? Anachotafuta ni nini iihali kuna nguo za kiraia kila kona?

Tangazo lilitolewa na muda walipewa, kwanini wakaendelea kuvaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…