Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jeshi letu linavaa pensi? Unauliza yalipopatikana hayo mavazi kabla ya kuuliza jeshi liliyapotezea wapi hadi watu wakayapataNawapongeza sana hao wanajeshi! Aliyapata wapi hayo mavazi kama siyo jambazi huyo?
[emoji1787][emoji1787]Nenda kalinde mipaka
Nenda vitani huko
Syo nguvu yote unatumia kwa raia
Ova
[emoji1787][emoji1787]Jeshi letu lingeongeza ubunifu kidogo, lingebuni 'sare za jeshi' zinazoruhusiwa kuvaliwa na raia likaziuza kama jezi za Yanga na Simba.
Ukosefu wa ubunifu ndio uliua viwanda kama Urafiki, Sunguratex, Mwatex, Mbeya tex, Musoma tex, Morogoro Canvas nk.
Sahihi sana mkuu, vita kuu ya pili ya dunia boats za raia zaidi ya 850 zilikwenda kuokoa askari wa Uingereza na allies ambao tayari walikuwa wamezungukwa,Jeshi lenye poor training na vilaza wengi huwa linachukia raia na huwa linawanyanyasa, na ndio jeshi huwa linapokea kichapo likikutana na jeshi lenye maadili.
Sifa mojawapo ya nchi zinazoshinda vita ni muunganiko na kuelewana kwa wanajeshi na raia. Mwaka 1973 Israel ilipovamiwa na Waarabu ilikuwa kwenye sikukuu ya Yom Kippur ambayo ndiyo takatifu zaidi kwa Wayahudi na walikuwa mapumziko huku wakizingatia sheria kali za dini. Raia walipojua nchi imevamiwa haraka wakatoa magari yao sababu siku hiyo hakukuwa na safari ni siku takatifu. Watu wakahamasishwa kuachana na sherehe wakapambane, reserves zikatumia magari ya kiraia kufika kambi zao na mambo mengine yakaendelea. Yani bongo tuseme daladala, Abood, Shabiby na makampuni yote yajiamulie yenyewe kubeba wanajeshi kuwawahisha Arusha mfano tumevamiwa na Kenya.
Kwa upande mwingine, jeshi la Uganda kwenye vita ya Iddi Amin lilikuwa linachukiwa kiasi kwamba Tanzania ilikuwa inashangiliwa ikichukua mji. Na hapo kuna support kubwa tulipata kwa Waganda, na raia nchi nzima walilisusia jeshi wakati sisi huku bongo walikuwa wanapewa michele na ng'ombe bure na raia wapate nguvu. Kwanza Waganda walikuwa wanakimbia recruitment, si mnajifanya mna nguvu kapigane wenyewe wakati sisi huku raia alikuwa anakataliwa Mara kwa ubovu wa jicho anapanda basi anaenda kujiandikisha Mwanza ashajua namna ya kukwepa ukaguzi.
Ukishakuwa na wanajeshi wanajiona ni class tofauti na raia ujue kwenye recruitment unabeba vilaza wasiostahili na kwenye training unapwaya.
Yeah. They need to produce armature combat, T-shirts, shorts, bags etc to sell to the general public.hzo nguo hazina tofauti na sanda ukiondoa hayo mabaka mabaka.hazina uspecial wanaozipa wao kiasi cha kuona anayevaa kama sio wao basi ni muhalifu.
Akijibu ni-tagKwanini uvae nguo za jeshi na wanakataza kila siku? Tuanzie hapa kwanza