JWTZ, kwa huu Ufisadi unaoendelea nchini, tukubaliane tu muongoze kipindi cha mpito kulipatia Taifa Katiba Mpya

JWTZ, kwa huu Ufisadi unaoendelea nchini, tukubaliane tu muongoze kipindi cha mpito kulipatia Taifa Katiba Mpya

Umesahau pembejeo na mbolea. Ukiangalia vizuri picha ya pili, hii ITEL inaingiza pembejeo pia. Ndio wanaleta mbolea feki hawa hawa jamaa na kuwaumiza wakulima. Kwahiyo project nzima ya ruzuku za pembejeo sijui nini ni circle hile hile. Dadeeeeek!!!
Hawa washenzi wanalifisadi sana hili Taifa
 
Kaka nakuelewa vizuri sana na kwenye hii comment umetiririka uhalisia mtupu.

Ni kweli kabisa kuongoza nchi inahitaji mtu mwenye uelewa mpana sana kwenye nyanja zote muhimu zinazogusa maisha ya mwanadamu.

Tena kwa taifa kama hili ambalo lina changamoto kibao na idadi kubwa ya watu linahitaji mtu makini sana na ambaye ana akili nyingi aina ya Kagame.

Ila sasa kwa vile tayari tumeshaya kanyaga leo hii tuna mtu kama samia ambaye naye ni kilaza tu pengine kuliko hao maafisa wa JWTZ ni heri tuwape hao JWTZ ambao naamini kuna mambo ya ovyo tunayoyaona kwa samia wao hawatakuwa nayo kama vile kuuza na kutapanya ovyo rasilimali za taifa, kuua watu ovyo wasiokuwa na impact kwenye utawala wao n.k

Kwa tulipofikia ni heri tuachague mbaya tunayomini ina nafuu kuliko kuendelea na mbaya isiyofaa ambayo inazidi kuwa mbaya zaidi kadri siku zinavyokwenda.

JWTZ hata kama watatumia mababvu kuliko akili, ila naamini discipline itakuwepo kwanzia serikalini mpaka uraiani.

Acha tuwape tu kuliko kuendelea kutawaliwa na hawa wauaji... imagine eti wale madogo waliokuwa wanaponda bango la samia, wameuawa sasa ndio serikali gani hii? Samia na ccm yake hapana kwakweli
Hiyo clip ya hao madogo unayo? Imenipita hii..
 
Kampuni yenye mahusiano na mtoto wa Rais Abdul inapewa tenda za kuchimba Maliasili za Taifa kwenye moja ya mkoa masikini zaidi Tanzania.

Kampuni hii inachimba madini ya Makaa ya Mawe kwa kiwango cha kutisha na kuyasafirisha nje ya nchi.

Kampuni nyingine ya swahiba wa Rais Rostam Aziz inapewa kibali cha kuchomba Makaa ya Mawe kwa bei ya kutupa kwenye mkoa huo huo wenye umasikini wa kutisha.

Kampuni ya Mtoto wa Rais pia inapewa tenda ya kuingiza sukari nchini na kuwauzia Wananchi.

Haya yote yanafanyika huku Watanzania wakizidi kuwa masikini. Hawana maji safi na salama ya uhakika. Hawapati madawa hospitalini.


Haya yote yanafanyika huku Amiri Jeshi Mkuu, Mtoto wake na mkwe wake wakiongoza makundi ya kuwateka, kuwapoteza na kuwaua Watanzania wasio na hatia wanaopaza sauti kukataa uovu.

Endapo JWTZ hawatachukua hatua sasa nitaungana na Watanzania kusema kwa sauti moja tuna Jeshi la Kipumbavu haijawahi tokea na ni heri libadilishwe jina na lisiitwe tena Jeshi la Wananchi.
View attachment 3491456View attachment 3491457View attachment 3491458View attachment 3491459
Nakuona bado kuna watu wanatetea
Nashangaa sn
🥲🥲🥲
 
Unaongelea Jeshi as if it's a mythical, divine, and holy being capable of everything, including kupindua nchi. Hichi kitu ni highly prevalent Afrika, kuomba na kuabudu chochote chenye kuonyesha nguvu au power na kutegemea easy and fast results, bila kujali uhalisia ni nini. Ni mindset inayoendelea kututeketeza. Hata wewe mleta mada unaweza ukawa unajiona tofauti na the majority lakini bado uko palepale. I hope you won't take this personally. It's simply an observation.

Binafsi nachukia sana kuabudu, kunanitia hasira sana. It's equivalent to stating or admitting to oneself that you're absolutely powerless and there's nothing to be done. I also hate worshipping the most, for it leads to complacence. Kubweteka.

Jeshi sio one single powerful being bali limeundwa na watu kama wewe na mimi. Watu binafsi wenye maono na maoni tofauti ya maisha. Wana familia, ndugu na jamaa wanaojaliana. Jeshi kwao ni kazi tu kama kazi unayofanya wewe, wapo pale kutafuta na as long as wameridhika basi hawaoni tatizo. Unaweza kushangaa, lakini wengi wao kwa asilimia kubwa nao wana mindset kama yako na ya Waafrika wengi, wanaomba na kuabudu vilevile kwenye chochote wakionacho chenye nguvu.

Taarifa mbaya zaidi ni kwamba wamekuwa conditioned kutii amri za watu ambao wameambiwa ni wakubwa zao, ikiwemo serikali ambayo unaona hatuna cha kuifanya, na kukiuka kutapelekea adhabu kubwa.

Hivyo nao bila shaka wanashangaa kuona mkiwategemea wafanye kitu kikubwa sana kwao, equivalent na kumgeuka na kujaribu kumdhidi nguvu Mungu Muumba na Muweza wa yote.

Kwa maana hiyo tusitegemee jeshi kufanya chochote cha ajabu siku yoyote. There's catharsis in facing reality. Cha msingi ni kutafuta njia nyingine.
 
Back
Top Bottom