Maandamano yoyote yasiyo na kiongozi si rahisi kufanikiwa, na hata yakifanikiwa huwa ni kwa tabu sana na kwa gharama kubwa (mo29)
Maandamano yanahitaji mipango
. Ni lazima kujua yataanzia wapi, yataanza saa ngapi, nani atakuwa mratibu au kiongozi, na yatamalizikia wapi. Pia, ajenda za maandamano zinapaswa kuandikwa kwenye mabango yatakayobebwa na waandamanaji ili kila mtu ajue lengo na ujumbe wa maandamano hayo.
Ni vizuri pia washiriki wakapewa maelekezo ya msingi kabla ya kuanza maandamano ili kupunguza purukushani, ingawa ni kweli kwamba wakati mwingine purukushani hazikosekani ( ukiwa kwenye maandamano kuna mawili)
Kwa upande mwingine, mratibu wa maandamano anaweza kuwasiliana na mamlaka husika kuomba kibali pale kinapohitajika, pamoja na kuomba ulinzi ikiwa kuna ulazima, ili maandamano yawe salama na yenye utaratibu
SWALI LA KUJIULIZA:
Kwa hapa Malawi Ukifata hizo taratibu zote una uhakika utafanikiwa au ujiongeze kwa namna nyingine(hapa utajua wewe sasa)
Tlaatlaah ni kweli atakae toa pua njee kunusa harufu ya wali kwa jirani ataungana na malaika mbinguni?