Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Enzi za kusaidia watu wengine for free nadhani tumwachie Hayati Nyerere.
Kwa sasa kwa sababu tulishaona jinsi tulivyocheleweshwa sababu ya vita ya ukombozi wa ndugu zetu wa kusini mwa Afrika, ni wakati wa kuingia makubaliano maalum na serikali ya DRC, tuwasaidie lakini watupe raslimali za kuendeleza nchi yetu pia kama malipo ya kazi ya kuwasaidia kiulinzi.
Haiwezekani Tanzania iendelee kuwa chini tu siku zote kwa sababu ya usamaria wema!
Na wengi tuliowasaidia hawajui wala kukumbuka mchango wetu wao wanawajua Nkrumah na Mandela tu although they did absolutely nothing for them.
Mubage aliandika kitabu kinaitwa Asante Mwalimu - The unsung hero of Africa. Mchango wa mwalimu unasahaulika pamoja na kujitolea kote. Hatutaki kurudi huko.