JWTZ, tulindieni heshima yetu yalindeni maslahi yetu DRC-Congo

JWTZ, tulindieni heshima yetu yalindeni maslahi yetu DRC-Congo

Ni humu humu nimewahi kuandika uzi miaka minne iliyopita kuwa kandarasi ya kuwamaliza M23 na wenzao ipewe JWTZ tu bila kuwachqnganya na wengine. Ni kazi ya mwezi mmoja tu. Siyo kuwatimuq bali kuwaua.
Nazani hili liko kwenye process sizani kama Tshekedi atapuuza katika kipindi ambapo Rwanda kamzidi kimbinu
 
Jeshi la akiba ndo lende kongo , kila mwaka JKT wakila ugali bure, waende wajue medani za vita, hii ni pomoja na Wabunge wote walioenda jkt kipindi flani
 
Naunga mkona utatuzi wa huo mgogoro. Ila kuliingiza jeshi kichwa kichwa tutapeana gharama tu za mali na maisha ya askari wetu.

Pia inaweza kuhatarisha nchi yetu hawa wahuni wakaanza kutuvizia vizia.

Hatupaswi kwenda kama TZ, ni lazima tuwe na mwamvuli ili tukiwashe vizuri.

Vita inagharama kubwa sana.
 
Kumjua Mfadhili numero uno angalia Congo wanaongea Lugha gani ?
 
Wakongo waweke mzigo mezani au watupe mgodi mmoja wakati wanajeshi wetu wanasaidia, wengine wanachimba madini na ya kuyarudisha home..!!

Miaka hii hakuna cha bure, enzi za mwalimu zilishapita..!! Ss hivi kila mtu ashinde mechi zake.!!
Umenena vema.
Kama huna cha kutulipa bora upigike tu🤣
 
Afande G. Mkunda

Ni muda wako wa kulinda historia na heshima ya muda mrefu iliyowekwa na watangulizi wako

Yanayoendelea DRC hatuwezi kuyaacha yaendelee, Sisi kama MABABU wa ulinzi na ukombozi katika ukanda wa east na south Africa ni fedheha kuona mgogoro huu unaendelea na Sisi tumekaa tuu bila kuchukua hatua.

Pamoja na madhaifu mengi ya jeshi la Congo, inahitaji hatua ya dharura kuokoa maisha ya watu wanaokufa bila hatia na safari hii tuende kimkakati zaidi

1. Kuwe na Mkataba wa muda mrefu wa ulinzi eneo lote lenye mgogoro -kivu, goma nk liwe chini ya ulinzi wa majeshi ya Tanzania Kwa makubaliano maalumu.

2. JWTZ iweke military base katika maeneo hayo.

3. JWTZ ifanye kandarasi ya Ku reshape jeshi la Congo ili Kuwa stabilize jeshi la Congo.

Endapo makubaliano hayo yatafikiwa basi Afande utakua umeweka historia na kudumisha yaliyofanywa na G.

Mwamunyange, akisaidiwa na Wazee wa kazi chafu B.G Mwakibolwa na Lt.G Mella

Licha za faida kiuchumi tutakazopata bado tunahitaji heshima yetu, wananchi wa Congo wanaimani kuwa JWTZ itawakomboa kutoka mkononi wa waasi.

Afande ni muda wako wa kulinda heshima na maslahi ya Tanzania DRC
Mimi ningeshauri afande afanye kila liwezekanalo alinde heshima ya Tz ndani ya Tz tusije tukafikia hali waliyo nayo wacongo..
 
Mimi hapa naweza kuchangia mawili:

-Chanzo cha mgogoro huo mnakijua? Uache ushabiki, utumie akili za kiutu uzima: enzi za kikwete, walifukuzwa wanyarwanda kutoka kanda ya ziwa. Ni kweli wapo waliokuja kiharari, wengine haramu. Walizaliwa wengine mpaka wanafukuzwa, hawajawahi kufika Rwanda. Walipofika, waliwekwa kambini, mpaka walipojengewa na kuanza maisha upya. Chokochoko za kisiasa, huwa chanzo cha kuyumbisha raia tu. DRC, haikuwa na tatizo, lilianza mwaka 1994. Waliouwa watutsi, walilianzisha na kutaka kumaliza kabila lote hata wakazi wa huko. Hivi mfano, huku mtu akisema awamalize wasukuma, patakalika?

-Hayo ni mawazo yako na huenda yakatekelezwa. Ila, kwenye kikao cha umoja wa mataifa(wa mchongo tu), walisema hivi vita vinaweza kuwa vya ukanda. Na kweli inawezekana.
Unadhani waliosema Rwanda anahusika hawana sababu!? Wanaosema Uganda na Kenya zipo upande wa M23 unadhani hawana wanachokijua!? Burundi ina uongozi wa kihutu. Rwanda ni wa kitutsi. Vuta nikuvute zao, unazisikiaga. Unategemea nini?! Unajua kisa cha Burundi kuondoa majeshi yake Kivu kasikazini!?

Je, South Africa na Rwanda unajua mahusiano yao yako vipi?!

Hao wote wanaopigana upande wa DRC, uzuri wote walishasema wana interests zao huko Congo. Hizo interests wanazogombania, M23 haina? Unadhani yenyewe haina wafadhili!?

Vitani hawachezi danadana. Na uache ushabiki. Tanzania ikienda kupigana, unadhani itauwa tu yenyewe haipotezi!? Na uzuri kama ina masrahi, sema. Ila ni wewe si uongozi.
Haya, Congo imevamiwa na wanyarwanda. Kwa sasa, kuna kambi za wakimbizi kutoka DRC, wapo Rwanda. Unaona ni sahihi wao kuendelea kuwa wakimbizi!?
Duniani humu kuna mtu asie na kwao!?
Waafrica tuna akili mbovu, na ndo wanachotuzidi wazungu. Nyie uaneni mtajua wenyewe, madini wachote waende kuendeleza kwao.
Kwa akili hiyo ya kushabikia vita, mwanao nae aje hivo hivo, kuna chochote!? Amani ikizidi ni tatizo. Maisha ya ukimbizi yasikie kwa watu, yasikukute.

Jambo la Rwanda na DRC, historia hiyo inaanza mwaka 1885 au na 6. Anzia hapo then badae uje tena.
 
Mimi ningeshauri afande afanye kila liwezekanalo alinde heshima ya Tz ndani ya Tz tusije tukafikia hali waliyo nayo wacongo..
Kuna watu wanadhani vita ni kama mechi. Congo kuna wezi wakubwa, na hizo M23 na FDLR zipo, lakini uzito upo kwingine. M23 mnadhani ina ubavu wa kumtumbua Chirimwami au Omega!?
 
Unawajua JWTZ ww au unasikia barabarani ..?
Wewe uliwaona wapi!? Wana nini wanachotumia wengine hawana!? Wana mwili gani usioingia lisasi? Wana ujinga gani wa kuingia vita bila sababu? TZ na yo ni serikali, member wa UN. Na japo UN ya mchongo, ila ina masharti inayofuata, usidhani inajiingiza kimhemuko tu.
 
Ni humu humu nimewahi kuandika uzi miaka minne iliyopita kuwa kandarasi ya kuwamaliza M23 na wenzao ipewe JWTZ tu bila kuwachqnganya na wengine. Ni kazi ya mwezi mmoja tu. Siyo kuwatimuq bali kuwaua.
Hivi nikuulize, M23 ni kina nani!? Na wanatafuta nini!?
 
Wakongo waweke mzigo mezani au watupe mgodi mmoja wakati wanajeshi wetu wanasaidia, wengine wanachimba madini na ya kuyarudisha home..!!

Miaka hii hakuna cha bure, enzi za mwalimu zilishapita..!! Ss hivi kila mtu ashinde mechi zake.!!
Umeongea point. Hapo mnapotaka kunyang’anya M23 migodi, na yenyewe inailinda kwa masrahi ya wengine. Ni wekeni mezani mtupe hiki na hiki, mzigo wenu upo. So, mnachowaza JWTZ ipewe, kuna na wengine wanapewa hicho hicho. Je, wapo tayari kupoteza!? Kama mlifatilia, kuna case ya Kampuni ya Apple kutumia madini kutoka DRC, na huku ilikatazwa. Ukija kufatilia huo mlolongo,utagundua kitu. Wenye masrahi DRC ni wengi.

Juzi kwenye mkutano wa UN, mkuu wa MONUSCO Bintou Keita, alisema kwamba Rwanda inatumia GPS jamming system, inayosababisha MONUSCO washindwe kutekeleza majukumu yao.
Je, hiyo mifumo Rwanda imeitoa wapi? Unadhani aliongopa!? Na mpaka Rwanda aweze kujam hizo system, UN unadhani kampuni ya kibongo!? Kuna mikono ya watu wengi sana tena wazito.
 
JWTZ kama iko vizuri isikubali kupigana vita visivyo na maslahi, majeshi yote duniani yanapigana kwa maslahi..!!
Hiyo kujitolea haipo, hatuwezi kupoteza wanajeshi wetu kwa kuwasaidia free.
Waweke mzigo pande zote mbili tufaidike..!!

Hatuwezi kununua kesi bila kufaidika..!!
 
Umenena vema.
Kama huna cha kutulipa bora upigike tu🤣
Wale wanajeshi ni nguvu kazi ya taifa, sasa kupeleka wanajeshi wetu kwenye uwanja wa vita bila maslahi huo ni uwendawazimu.!!

Tushajua kinachogombaniwa mali, sasa kwanini na sisi tusiweke masharti yetu ili tufaidike km wengine??
 
Tanganyika haijawahi kua na maslahi nje y kiuchumi nje ya Tanzania. Nyie endeleeni kuvunja matofali.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Jeshi la akiba ndo lende kongo , kila mwaka JKT wakila ugali bure, waende wajue medani za vita, hii ni pomoja na Wabunge wote walioenda jkt kipindi flani
Mkuu JKT Bado hawajakomaa ki medani Kwa asilimia chache wanaweza kuchukuliwa ila sio Kwa wingi
 
Back
Top Bottom