Afande G. Mkunda
Ni muda wako wa kulinda historia na heshima ya muda mrefu iliyowekwa na watangulizi wako
Yanayoendelea DRC hatuwezi kuyaacha yaendelee, Sisi kama MABABU wa ulinzi na ukombozi katika ukanda wa east na south Africa ni fedheha kuona mgogoro huu unaendelea na Sisi tumekaa tuu bila kuchukua hatua.
Pamoja na madhaifu mengi ya jeshi la Congo, inahitaji hatua ya dharura kuokoa maisha ya watu wanaokufa bila hatia na safari hii tuende kimkakati zaidi
1. Kuwe na Mkataba wa muda mrefu wa ulinzi eneo lote lenye mgogoro -kivu, goma nk liwe chini ya ulinzi wa majeshi ya Tanzania Kwa makubaliano maalumu.
2. JWTZ iweke military base katika maeneo hayo.
3. JWTZ ifanye kandarasi ya Ku reshape jeshi la Congo ili Kuwa stabilize jeshi la Congo.
Endapo makubaliano hayo yatafikiwa basi Afande utakua umeweka historia na kudumisha yaliyofanywa na G.
Mwamunyange, akisaidiwa na Wazee wa kazi chafu B.G Mwakibolwa na Lt.G Mella
Licha za faida kiuchumi tutakazopata bado tunahitaji heshima yetu, wananchi wa Congo wanaimani kuwa JWTZ itawakomboa kutoka mkononi wa waasi.
Afande ni muda wako wa kulinda heshima na maslahi ya Tanzania DRC
Mimi hapa naweza kuchangia mawili:
-Chanzo cha mgogoro huo mnakijua? Uache ushabiki, utumie akili za kiutu uzima: enzi za kikwete, walifukuzwa wanyarwanda kutoka kanda ya ziwa. Ni kweli wapo waliokuja kiharari, wengine haramu. Walizaliwa wengine mpaka wanafukuzwa, hawajawahi kufika Rwanda. Walipofika, waliwekwa kambini, mpaka walipojengewa na kuanza maisha upya. Chokochoko za kisiasa, huwa chanzo cha kuyumbisha raia tu. DRC, haikuwa na tatizo, lilianza mwaka 1994. Waliouwa watutsi, walilianzisha na kutaka kumaliza kabila lote hata wakazi wa huko. Hivi mfano, huku mtu akisema awamalize wasukuma, patakalika?
-Hayo ni mawazo yako na huenda yakatekelezwa. Ila, kwenye kikao cha umoja wa mataifa(wa mchongo tu), walisema hivi vita vinaweza kuwa vya ukanda. Na kweli inawezekana.
Unadhani waliosema Rwanda anahusika hawana sababu!? Wanaosema Uganda na Kenya zipo upande wa M23 unadhani hawana wanachokijua!? Burundi ina uongozi wa kihutu. Rwanda ni wa kitutsi. Vuta nikuvute zao, unazisikiaga. Unategemea nini?! Unajua kisa cha Burundi kuondoa majeshi yake Kivu kasikazini!?
Je, South Africa na Rwanda unajua mahusiano yao yako vipi?!
Hao wote wanaopigana upande wa DRC, uzuri wote walishasema wana interests zao huko Congo. Hizo interests wanazogombania, M23 haina? Unadhani yenyewe haina wafadhili!?
Vitani hawachezi danadana. Na uache ushabiki. Tanzania ikienda kupigana, unadhani itauwa tu yenyewe haipotezi!? Na uzuri kama ina masrahi, sema. Ila ni wewe si uongozi.
Haya, Congo imevamiwa na wanyarwanda. Kwa sasa, kuna kambi za wakimbizi kutoka DRC, wapo Rwanda. Unaona ni sahihi wao kuendelea kuwa wakimbizi!?
Duniani humu kuna mtu asie na kwao!?
Waafrica tuna akili mbovu, na ndo wanachotuzidi wazungu. Nyie uaneni mtajua wenyewe, madini wachote waende kuendeleza kwao.
Kwa akili hiyo ya kushabikia vita, mwanao nae aje hivo hivo, kuna chochote!? Amani ikizidi ni tatizo. Maisha ya ukimbizi yasikie kwa watu, yasikukute.
Jambo la Rwanda na DRC, historia hiyo inaanza mwaka 1885 au na 6. Anzia hapo then badae uje tena.