Kabendera anawezaje kusema Hayati Magufuli alienda na pajama kwa Makamu wake je walinzi wake na Walinzi wa Makamu walikuwa wapi?

Inategemea rais anaishi wapi na Makamu wa Rais anaishi wapi.
Kwa sababu inavyoelekea kwangu mimi siku za karibuni rais haishi Ikulu.
Rais haishi katika Ile nyumba nyeupe tunayoiona katika picha .
Kwa hiyo safari ya kwenda kumsalimu Makamu huku amevaa pyjama,labda alikwenda kwa mguu.
 
Ni kitabu cha kijinga, before you read a book soma publisher.

Kama muhusika alikuwa anatumika na wazungu elewa access (opportunity wanazoweza mpa).

Yaani watu wampe access ya kwenda kufanya Phd chuo kikubwa, na media alizokuwa anaandikia wana multiple publishing firms (part of their group companies) na wameogopa kujihusisha na ule ujinga. Wangechapisha wao wangefanya na marketing pia ya kukiuuza.

Sasa hao waliokataa sio wachapishaji wenyewe ni kuogopa kuziingiza nchi zao kwenye diplomatic row, kwa ujinga ulioandikwa mule wasomaji wao are not that stupid and gullible ata kama hawaijui Tanzania (too childish).

Pili elewa psychology ya mwandishi anapotokea, binafsi wakati nasikiliza interview ya Kabendera asilimia kubwa ya mambo ambayo kayaongea ni vitu ambavyo tayari nilikuwa nishaadika humu JF.

Mengine kwenye interview ni uongo, promotion and self defence tu. Kwa wanasheria makini wakiamua wanamshtaki kwa picha tu aliyotumia; achana na maudhui ya upuuzi alioweka.

Usalama wa taifa ni mchezo wa watu wenye akili (hasa analyst), there is nothing else.

Magufuli hakuwa perfect lakini watanzania wanahitaji social reformer, akili zao bado sana.

Asilimia kubwa ya watanzania hawaelewi decisions za maisha zina consequences na kuna rules of engagement in life. Hii ni shida kubwa sana sio kwa raia wenye elimu ndogo, bali hata viongozi wenye nyadhifa kubwa serikalini.

Kumwelewa Magufuli inataka akili kubwa
 
Kitu pekee kipya nilichojifunza kwa kusikiliza interview ya Kabendera kulikuwa na maafisa usalama kibao jela.

Jiwe alikuwa mwanaume, mara ngapi mimi humu nimekuwa nikiandika wapiga deal wakubwa ni maafisa usalama na ndio wanao haribu nchi.

Kumbe njemba alikuwa ana deal nao kimya-kimya.

R.I.P Magufuli

Predictable
 
Sina hakika na hiii habari ...!
Hivi Kwa jinsi unavyomfahamu Marehemu, hata wewe ndo ungekua Mlinzi wake.....! Ungeweza kusimama kwenye Njia ili asipite...!?
 
Kwani hawezi kwenda na escort ndogo huku amevaa pajamas?
Hebu nawe weka ukweli wako(hauwezi kupinga strongly bila ya kuwa na facts hata kama maelezo unayoyapinga yana walakini) ili tupime kati yako na Kabendera nani ni mkweli na nani ni muongo.
Marehemu alikuwa na machawa wenye IQ ndogo sana yaan wao hata Jiwe angewaambia yeye ni mtume na nabii kesho wangepanga foleni kumuabudu.
 
KABENDERA ANADAI BEN SANANE ALIUAWA NA 'BWANA MKUBWA'!

Mwishoni mwa mwaka 2020, nilipata ujumbe mzito kutoka kwa Rais Magufuli kupitia kwa mtu wake mmoja ambaye jina lake linatunzwa. Rais alimtuma kwangu akiniomba nishawishi Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Tundu Lissu waridhie wabunge wanawake 19 waapishwe kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Nilijitahidi kufurukuta kueleza Rais ajue kuwa sikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wala mimi sikuwa na ushawishi wowote katika jambo lile. Lakini Rais aliamini kuwa Lissu na Mbowe watanisikiliza mimi. Lilikuwa jambo gumu sana kwangu kumshawishi mtu yule aniamini mimi. Ahadi niliyoahidiwa na ambayo pia CHADEMA wangepewa kama 'dili' lile lingefanyika ingali katika kilindi cha moyo.

Nakiri kuwa baada ya ombi la Rais la kunitaka niwashawishi Lissu na Mbowe kushindikana, zoezi la uapishwaji liliendelea na mimi nikajua kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Lakini hoja la andiko hili sio jambo hili.

Mwezi Januari 2021, alitumwa tena kwangu mtu yule yule. Safari hii haikuwa kunishawishi ili niwashawishi Mbowe na Lissu, bali ilikuwa ni kunitisha niachane na harakati, la sivyo basi nilikuwa nachungulia mauti. Nilikuwa nimetoka kuitangazia dunia kuwa maisha ya Mhe. Lissu yalikuwa hatarini na ndipo Ubalozi mmojawapo ukamchukua na kumpeleka nje ya nchi.

Kwa hiyo jibu langu kwake lilikuwa moja tu: "Mwambie Mheshimiwa kuwa akitaka aniue, lakini Askofu hatarudi nyuma"! Vitisho vya aina hiyo niliwahi kupewa na Polisi mmoja nikiwa Central Polisi, Dar es Salaam mwezi mmoja kabla Rais Magufuli hajafariki dunia.

Baada ya majibu yale, yule mtu alitetemeka na ikabidi aropoke mambo mengi sana ambayo sio sehemu ya andiko hili kwani kwa sasa Bado mambo yale ni 'classified information'! Baada ya hapo nikaanza kupata taarifa nyingi ambazo zilinitisha na kunipatia matumaini.

Siku moja nilitafutwa na mtu mmoja ambaye ni mzima na kada wa CCM. Kwa kuwa mtu huyo tunaheshimiana na kwa kuwa aliaminishwa ya kuwa mimi nilikuwa natumiwa na 'mabeberu'; ilibidi nimueleze pia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanamzunguka Rais. Nilifanya hivyo ikiwa kinga yangu kwani nilijua kuwa ataelewa mazingira yangu na hivyo ataweza kupangua hoja dhaifu dhidi yangu akiwa katika 'Pango la Wakilindi'. Aliishia kunikodolea macho na ndipo tukaagana akiwa kama mtu asiyeamini.

Lakini kabla mtu huyo hajaondoka, aliniuliza: "Wewe umejuaje habari hizi'? Nikamjibu kuwa: "Mimi ni mskofu wa mnyororo na pia mimi ni askofu wa kiapo"! Mambo haya yaliaminiwa pia kwangu chini ya kiapo kwa hiyo nisingeyasema hadharani wakati ule na hata sasa. Hapa sio mahali pake kuelezea kisa cha askari aliyeacha kufanya ibada baada ya kushiriki kuwaua watu na baadaye kumbukumbu za watu wale zikawa zinamjia na kuharibu akili yake.

Mambo haya ni ya kitubio na kwa hiyo mtu ye yote atakayemuendea Mchungaji (Padri) au Askofu kwa kitubio, jambo lile linabakia katika kifua cha mtubishaji, anayetubu na Mungu.

Taarifa za kuchapishwa kwa kitabu cha Erick Kabendera zimeanza kusambaa kwa kasi sana mitandaoni siku ya leo tarehe 3 Januari 2025. Kitabu kinaitwa: 'In the Name of the President: Memoirs of a Jailed Journalist'. Nimesikiliza mahojiano ya Erick Kabendera kuhusu kitabu hicho. Nimeanza kufuatilia maudhui ya kitabu. Mengi ya mambo anayojadili ni sehemu ya yale niliyojulishwa kama 'sisi Askofu'! Ila sikutarajia mambo yale yangewekwa hadharani wakati wa uhai wangu. Ujasiri wa Kabendera unaivuka mipaka ya Nshamba na Kamachumu.

Ninaamini watu ambao walinishangaa kwa nini mimi nilijitoa muhanga kwa ajili ya kutetea haki nchini sasa wataanza kuelewa baada ya kuona na kusoma kitabu cha Erick Kabendera. Taarifa nyingi zilizofikishwa katika kilindi cha moyo wangu ziliishurutisha nafasi yangu kuchukua ili kupaza sauti na kutetea pale nilipoweza. Lakini pamoja na uropokaji wangu, mambo ambayo yalitiwa muhuri (sealed) katika moyo wangu yameamriwa na dhamiri iliyo kuu ili yasiyoke.

Kitabu cha Kabendera kitasaidia katika mambo muhimu. Kwamba tukisome na kumjua Rais Magufuli nje ya uelewa uliojulikana. Baada ya hapo, tuone kuwa alikuwa binadamu kama sisi na mwenye mapungufu na kisha tumsamehe. Kikubwa, kama jamii tutafute njia ya kuponya ikiwemo kuondoa vimelea au masalia ya yale aliyoayaasisi ambayo hayakuwa mazuri na hili itawezekana kama tutasoma na kuielewa sura ya mwisho ya Kitabu cha Kabendera.

Kitabu hiki kinaposambazwa na kusomwa ni vizuri tujue kuwa kinayahusu maisha fichika ya Rais Magufuli na sio maisha ya familia na ukoo wake. Hatuhitaji kwa namna yeyote kuwaona ndugu hata familia kama sehemu ya mambo aliyoyafanya kama Rais kwani nao walikuwa ni washangaaji kama sisi.

Mwisho, natoa wito kwa viongozi wa dini walio karibu na familia ya Ben Sanane na familia ya Azorly Gwanda kuzifikia kwa ajili ya huduma ya kiroho. Kupitia kitabu cha Erick Kabendera na mahojiano yake ni rasmi sasa ya kuwa umma umejulishwa kuwa watu hao hawapo pamoja nasi katika maisha haya.

Hekima iliyo ndani ya kilindi cha moyo wa Rais Samia inaweza kumsaidia afanye nini kwa ajili ya familia hizo. Bila shaka, CHADEMA itatafuta namna njema ya kuhitimisha kwa heshima kwa kumkumbuka Ben, mwanachama na Msaidizi maalum wa Mhe. Mbowe. Kadhalika, Gazeti la Mwananchi litaona pia namna ya kulihitimisha l kwa heshima ya Azorly, aliyekuwa mtumishi.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Januari 2025; saa 2:00 usiku
 
Mwamakula ni cray-cray anaandika kama vetted national security agent.

Afisa gani wa usalama ataenda mpa habari za ndani mtu ambae hana clearance ya kupata hizo habari.

Wao wenyewe maafisa usalama wana level of clearance you’d think mambo ya Ikulu ni top level information.

Na kama possibility hiyo ya kupewa hizo habari basi lengo lingekuwa atoe leak. Lakini wakampe siri akae nazo yeye ni nani ndani ya usalama (kwanza angekuwa wao Magufuli angeshajua).

Anajikuza tu taahira mwengine, yaani upewe siri for the sake of it ambazo hazikuhusu.

Askofu anasoma sana JF, angalia movie ya (a beautiful mind) jamaa anaelekea huko. Anaongea vitu ambavyo ni impossible kwa sasa vipo kwenye kichwa chake tu Mwamakula (I see dead people).
 
Back
Top Bottom