Kabla hatuja wafundisha "Wasiomini Mungu" juu ya uwepo wake, basi inafaa sisi "Tunaoamini Mungu" tumalize tofauti zetu

Agnostic na Atheism ni kitu kimoja?
Hivi tunaelewana kweli?

Nimekwambia hao wote hawaamini Mungu/miungu ila wanatofautiana ndio na ndio point yangu kwamba hata wasioamini Mungu pia hutofautiana.
 
Mkuu ningependa unifahamishe tofauti ya takatifu na tukufu.

Kwa lengo la kujifunza tu hii lugha ya kiswahili.
Tukufu ni kilichopewa heshima kubwa. Chenye ukuu.

Takatifu ni kilichotakata, kisicho uchafu.

Kwa hivyo, unaweza kuwa na kitu tukufu kisicho takatifu, na takatifu kisicho utukufu.
 
Hivi tunaelewana kweli?

Nimekwambia hao wote hawaamini Mungu/miungu ila wanatofautiana ndio na ndio point yangu kwamba hata wasioamini Mungu pia hutofautiana.
Unachanganya mambo mawili ambayo hayana uhusiano

Hakuna utofauti kati ya atheist na atheist kama ambavyo tunaweza kuona kati ya theist na theist wakipingana

Ila kuna utofauti kati ya atheist na makundi mengine kama theism, agnosticism, Deism nk.

Muislamu ni theism, mkristo naye ni theism, hawa watu wapo kunfi moja lakini bado wanatofautiana.

Lakini pia sio hiyo tu hata muislam kwa muislam bado pia wanapingana wenyewe kwa wenyewe na humu tunaona namna wanavyo bishana licha ya wote kuwa category moja (theism)

Sasa lini uliona atheist kwa atheist wakipingana kama nyinyi mnavyofanya?

Usinambie agnosticism kwasababu hilo ni kundi lingine halihusiani kabisa na atheism, kumbuka hapa tunatafuta hoja ya watu kupingana wao kwa wao
 
Kwa nijuavyo agnostic sio atheist. Ila ni watu ambao wapo katikati yaani hawana uhakika kama Mungu yupo au hayupo.
 
Twende hivi.

Theists ni wenye kuamini Mungu au miungu, sasa mpaka hapo unaanzaje kutaka kuona hao watu kutokupingana? Sasa tatizo ni wao kupingana au kuwekwa kundi moja hali ya kuwa wanapingana?

Mimi nimewaweka kundi moja Agnostics na atheists kwa hoja ya kwamba wote hawaamini Mungu/miungu ila wewe unasema hayo ni makundi tofauti kutokana na tofauti zao ila kule kwa wenye kuamini Mungu na wenye kuamini miungu wamewekwa kundi moja halafu unashangaa kupingana.
 
Waislamu wanaabudu Mungu au Miungu?
 
Tutakuja huko kwa waislamu, tumalize hapa kwanza kwa theists kupingana.

Waislamu wanaabudu Mungu mmoja.
kwani waislamu sio theists?

Kama wanaabudu Mungu mmoja kwanini wanatofautiana kwa kupingana wao kwa wao?
 
kwani waislamu sio theists?

Kama wanaabudu Mungu mmoja kwanini wanatofautiana kwa kupingana wao kwa wao?
Kutofautiana ni kawaida kwa binaadamu maana hutofautiana uelewa.
 
Kutofautiana ni kawaida kwa binaadamu maana hutofautiana uelewa.
Ndo maana mtoa mada kashauri ni bora mfike muafaka kwa kumaliza tofauti zenu kisha ndio mje kuanza mijadala na atheists
 
Ndo maana mtoa mada kashauri ni bora mfike muafaka kwa kumaliza tofauti zenu kisha ndio mje kuanza mijadala na atheists
Nimekwambia binaadamu hutofautiana uelewa hivyo kupingana si jambo la ajabu, ndio maana pia wapo wenye mtazamo wenye kudai hakuna Mungu na wengine wanaona hakuna uwezekano wa kuweza kujua kuwepo au kutokuwepo kwa huyo Mungu.
Ukiangalia hoja za hao atheists kwanini hakuna Mungu? Utaona pia sababu tofauti tofauti.
 
Hoja zako naona ni rahisi kujibika kwa akili ndogo za kibinaadamu.

Nakushauri ufanye utafiti mdogo tu bila kuangalia superstitions zinazotangazwa na dini kama ndio msingi wa nguvu ya dini husika kwamba inastahili kufuatwa kutokana na superstitions hizo.

Katika dini moja Mungu hawezi kutoa maelekezo tofauti hiyo inafahamika.

Sasa ushauri wangu kwako ni huu:-

Tafuta swali/swala la msingi linalohisiana na imani/maisha ya binadamu.
Mfano: Yesu ni nani katika uislamu/ukristo?

Au: uliza Ndoa ili ikamilike na kuwa ndoa au watu tayari wameoana katika dini ni vitu gani vya msingi vitimizwe?

Ukishapata maswali yako ya msingi sio lazima hayo.

Kila swali tafuta viongozi watano wa dini ya kiislam wakujibu huku ukirekodi majibu, na ufanye vivyo hivyo kwa viongozi wa dini ya kikristo.


Viongozi wa dini moja watakaotoa majibu yanayofanana, nakushauri ifanyie kazi dini hiyo kuifuatilia zaidi. Mana naamini kama Mungu ni mmoja, hakika hawezi toa maelekezo tofauti katika dini moja.

NB: Hakikisha utakaowapata kuwauliza maswali uwe unauhakika na elimu zao za dini zao.
 
Kwenye jambo lenye madai ya kuwa limeshushwa kutoka kwa Mungu halafu ukaona bado watu wanapingana hapo lazima mashaka yawepo

Kwanini kitu kilichokuja kwa muongozo wa Mungu mwnye nguvu zisizomithirika bado kitu hicho kilete matabaka mwa kuwagawa watu?

Anyway nikweli watu tunatofautiana kwenye mambo mengi ila yapo mambo ambayo yametajwa kuwa ni extraordinary na yanajadiliwa kuwa ni ya kweli lakini hapo hapo unaona watu wa jamii hiyo wanapingana, inatia wasiwasi sana
 
Unataka kusema nini au unataka kuhitimisha nini?
 
.
 
Hakuna dini ya kweli inayoelekeza kuwagawa watu, dini zote zinasisitiza udugu baina yetu. Tena zipo zinazoenda mbali zaidi hadi kwa wanyama dunia etc

Ukiona matengano basi ni vile tu tamaa binafsi za wanadamu zipo kazini
 
ila hizi tofauti zinachanganya sana ili kupata uelewa japo kidogo, tu refresh back kipindi hikooo cha akina adam(A.S) then tudondoke mdogo mdogo hadi kwakina Abraham/Ibrahim (A.S) hadi tufike kwa Yesu/Issa (A.S) na hadi tufike kwa Muhammad (S.AW). Then tunaweza kupata kapicha hapa kaukweli japo kwa asilimia chache...
 
Hayo unayoyataka Mungu ayafanye alisha yafanya amemaliza alijifunua kwa manabii zaidi ya laki moja na katika hao manabii 4 amewapa vitabu ili iwe kumbukumbu kwa vizazi viliopo na vijavyo

Sasa kama wewe vitabu vyote 4 alivyowapa manabii wake hauviamini unataka Mungu akusaidieje?

Pia Mungu anataka utumie akili aliyokupa kwanza umjue yeye hayo mengine ni ya ziada hata ndege na wanyama wanayafanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…