Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

Nilikuwa na mpango wa kununua azam ila kwa uzi huu nawaona ni NDOROBO. Bora niendelee na wahindi wangu walionganisha na cable yao kwa elfu 10 kwa mwezi na napata kila kitu wanachopenda vijana wa kileo
 
Nilikuwa na mpango wa kununua azam ila kwa uzi huu nawaona ni NDOROBO. Bora niendelee na wahindi wangu walionganisha na cable yao kwa elfu 10 kwa mwezi na napata kila kitu wanachopenda vijana wa kileo
Nakushauri hiyo budget ya 250,000 wekeza sehemu yoyote. Sisi tunalipa 15,000 bado tunapata local channels na channel za east Africa baaaaaasi
 
Shule/chuo ni kwa ajilii ya kuendeleza kipaji cha mtu alicho nacho,huwezi kuwaondoa hao,ushauri mzuri wajifunze maadili yanayotawala kazi zao,kwa kiasi kikubwa hizo kazi ni kipaji na hubuniwa(sanaa)ukiwaondoa utamuweka nani?
 
Bujibuji said:
Nimetoa ushauri unatoa kashfa.
Au nwenzangu hujui kuwa kuna madishi ambayo hayatumii ving'amuzi vya kulipia? Pia jifunze kuheshimu watu wote unaowafahamu na usio wafahamu.
JF tunatumia majina na utambulisho wa bandia, kuna siku utakuja tukana baba yako, mjomba wako etc.
Labda hajui kama kuna memediacom.
 
TCRA mmeona vitu wananchi wanataka?.kuliko kuwa na ving'amuzi vingi bora kimoja kadi tofauti, unachagua kama simu kadi kupata huduma unazozitaka,pia chaneli za kulipia zijulikane.
 
Kwa kuiondoa ETV Africa kunanifanya nirudi kwenye Startimes ambako nitawaona kina Roman Reign na Dean Ambrose na WWE yao,

Kwa heri Azam TV

Mbc action na mbc2 huwa wanaonesha mieleka up to date, wwe na hata hii wrestlemania ya juzi juzi
 
Nimebahatika kutumia Azam tv. Kuna baadhi ya channel na vipindi ni bora zaidi kuliko local channels.

Tukianza na coverage ya tarifa ya habari, live coverage ya matukio ya kitaifa.

Udhamini wa ligi kuu ya Vodacom umetupa mwanga zaidi kuangalia na kuwafahamu wachezaji wa ndani na hata international football games kama haya mashindano ya CAF.

Azan wana news channel nzuri ila sio zote. Kukosekana kwa cnn, skynews, fox news, msnbc kunazorotesha biashara yao. Kuweka bbc, aljazeera, nhk pekee haitoshi. Mimi ni mpenzi wa news channel hususani za nje ya nchi.

Documentary channel zao ziko vizuri sana. Nimependa sana IDx, visat Nat/His, NatGeoGold, DS sio mbaya. Inaewezekana kuboresha zaidi.

Channel zao za movie hususani MBC(2,3,4 max, action) ni nzuri ila movies ni za zamani. Naelewa kuweka up to dated movies ni gharama ila msiwe mnaweka second generation movies (movies before 2010) na marudio marudio ya movies inaboa sana.

Kutokana na changamoto hizo binafsi nikaacha na azam nikajiunga zuku. Yote ni katika kuexplore na kujua hali ilivyo maana tayari startimes nimeshaipata.

Nilichokikuta zuku well channel nyingi za kenya na uganda, zingine zisizoeleweka.
Sports channel kama fox sports 1&2 , huonesha mechi za mpira za marudio wakati mwingine live hususani Australia, belgium na zingine.. ila unakuta unakosa la liga na mechi zingine kama za epl ambazo huoneshwa kwa nadra sana kwa baadhi ya station za kenya ktn na nbs ya uganda.

Ubora wa channel zao za movies ni mbovu kuliko za azam. Japo zipo English oriented ila ubora wake ni waduni sana pengine zaidi hata ya startimes. Na movies zinazooneshwa aisee ni hatari... ni za zamani mno. Ila juzi kati kupitia channel yao ya zuku max wameanza onesha movie za hivi karibuni.....yani 2009.

Documentary channel zao ni nzuri hususani hizi za viasat. Maana zipo educational and entertaining. Ila hawana tu IDx. Otherwise good

Music channels zao zipo poa na nyingi zaidi kuliko azam na ni njema sana hawa zuku.

Kwenye news channel wamejitahidi maana wanazo zoote kasoro cnn tu.

Otherwise kila kisimbusi kina kasoro yake. Nadhbi bado wanajipanga. Na kasoro kama hizi husaidia wao kujiboresha zaidi na zaidi.

Waweze kuongeza channel nyingi zuri na at least waelewe watz wengi ni english oriented na sio arabic wala Indian

Nawasilisha
 
Mimi nilipia vifurushi vyote lakini NTV Kenya na Uganda na nyingine nyingi ....wansema Access denied...!
 
Mimi nilipia vifurushi vyote lakini NTV Kenya na Uganda na nyingine nyingi ....wansema Access denied...!

unaona upuuzi wao huo? juzi kulikuwa mech ya Rwanda inaonyeshwa Rwanda Tv wakakata matangazo wakati nimelipia!
 
Kiukweli TCRA hawana budi kutoa muongozo haraka. Haiwezekani local channel ziwe zinalipiwa.
 
Back
Top Bottom