Kabla wamisionari hawajaja Afrika na kufundisha kuhusu mbinguni na kuzimu wazee wetu walikuwa wanaenda wapi?

Kabla wamisionari hawajaja Afrika na kufundisha kuhusu mbinguni na kuzimu wazee wetu walikuwa wanaenda wapi?

Sasa hivi ambavyo hufikiri inakusaidia nini kama siyo umauti kutokufikiri?
Acha kufokafoka una stress au? Jadiliana kwa hoja sio kwa mawazo yako kila mtu anaweza kufikiri ila tunazidiana uwezo! Ndiomaana ata tukifanya mitihani kuna alotangulia wengine wakafata! Sasa waafrika wajinga! We muingereza tupe mawazo yako na fikra zako ambazo hujaletewa!
Period!!
 
Watu wote waliokufa kabla injili haijawafikia watahukumiwa na zile sheria walizokuwa wamejiwekea wao wenyewe. Maana nyingi ya sheria za Mungu zimewekwa kwenye mioyo ya watu. Mpaka ulipofika ule utimilifu wa nyakati. Maana hata kama sio mkristo lakin hakuna jamii inaruhusu wizi uongo, au utapeli. Lakin pia kuna wazee wale walioas enzi za nuhu Yesu alishuka kuzimu kuwahubiria habar njema ili watu wote wamjue ile siku na wakahukumiwe kwa haki. Maana ni shart kila kiumbe kimpigie magoti Yesu hata Muhammad.
MBINGUNI AU MOTONI
Wale waliotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria. Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu. Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria. Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea. Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo. (Warumi 2:12-16)

Kabla ya wamisionari kuja Afrika na kufundisha habari za mbinguni na kuzimu, mpango wa Mungu ulikuwa tayari upo na unafanya kazi. Mungu hajawahi kuacha dunia bila mpango wa wokovu, hata kabla Injili haijatangazwa waziwazi. Biblia inasema wazi kuwa baada ya kifo, roho ya mwanadamu haipotei bali inaendelea kuishi. Kuna sehemu mbili kuu: mbinguni, mahali pa raha na uwepo wa Mungu, na kuzimu, mahali pa mateso na hukumu kwa waovu (Luka 16:22-23).

Wakati wamisionari walipofika Afrika, walileta habari njema ya Injili ya Yesu Kristo. Hii haimaanishi kwamba kabla yao hapakuwa na mbinguni au kuzimu, bali watu walikosa ufunuo wa kina kuhusu maisha ya baadaye. Mungu alikuwa na mpangilio wake tangu mwanzo. Katika Warumi 2:14-15, Biblia inasema kuwa hata mataifa yasiyo na sheria ya Musa, Mungu aliweka sheria katika mioyo yao kupitia dhamiri. Kwa lugha nyingine, watu waliokuwa hawajasikia Injili moja kwa moja walihukumiwa kwa namna walivyoitikia sauti ya ndani inayowaelekeza kutenda mema na kuacha mabaya. Hii inamaanisha kwamba mtu aliyeishi kwa uadilifu, bila kumjua Kristo moja kwa moja, Mungu alimwongoza kwa njia yake na kumhesabia haki kwa imani na matendo yake mema.

Hata kabla ya kuja kwa wamisionari, wazee wetu walikuwa na imani kwamba kuna Muumba wa mbingu na nchi. Katika tamaduni nyingi za Kiafrika, Mungu Mkuu aliitwa kwa majina tofauti kama Mungu, Mulungu, Nyame, Katonda, Ruhanga, na mengine. Tatizo lilikuja pale watu walipochanganya ibada ya Mungu na ibada ya mizimu kwa kukosa ufunuo kamili. Lakini yule aliyeishi kwa kumcha Mungu kwa kadiri ya maarifa aliyokuwa nayo, Mungu alimjua na kumpokea. Biblia inasema katika Matendo 10:34-35, “Hakika natambua kwamba Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa naye.”

Kabla Yesu kufa na kufufuka, Biblia inafundisha kwamba kulikuwa na sehemu mbili katika ulimwengu wa roho. Wenye haki walihifadhiwa katika “kifuani mwa Ibrahimu” – mahali pa raha na matumaini – huku waovu wakiwa katika sehemu ya mateso (Luka 16:22-23). Yesu alipokufa, alishuka mahali hapo na kuwakomboa wale waliokuwa wakingoja wokovu (1 Petro 3:19). Kwa hiyo, wazee wetu waliomcha Mungu walihifadhiwa mahali pa raha, wakisubiri kazi kamili ya Kristo msalabani.

Warumi 1:19-20 inaeleza kuwa ufunuo wa Mungu unapatikana kupitia maumbile, na hakuna mtu anayeweza kujitetea kwamba hakuwahi kumjua Mungu. Jua, mwezi, mvua, upepo, na uhai wa kila siku ni ushahidi kwamba kuna Muumba. Wale waliotafuta ukweli kwa moyo wa kweli waliongozwa na Mungu kwa namna ya pekee, hata bila kuwa na Biblia mikononi mwao. Kwa mfano, Ayubu hakuwa Myahudi, wala hakuwa na sheria ya Musa, lakini alijulikana na Mungu na akaishi maisha ya uadilifu.

Kwa hiyo, hata kabla Injili kufika Afrika, Mungu aliwahukumu watu kwa uadilifu. Wale waliomcha Mungu na kuishi kwa haki walihesabiwa haki kwa imani yao, kama Ibrahimu alivyohesabiwa haki kwa imani kabla sheria haijapewa (Warumi 4:3). Wale waliokataa uadilifu na kuishi kwa maovu walihukumiwa kulingana na mwanga waliokuwa nao. Mungu hufanya maamuzi kwa haki na upendo kwa kila mtu.
Kwa Mujibu wa Barua ya Paulo ambayo mnaitumia kielezea hili kwamba wata hukumiwa kwa dhamira zao mbaya....... Je kwa watu ambao walifanya mambo ambayo kwao yalikua na DHAMIRA njemà lakini mbele ya SHERIA mpya za Mungu ni DHAMBI itakuwaje
Kwa MFANO 👇👇👇👇👇

Kuna jamii ambazo kukiwa na majanga wanatoa kafara za kuua watu ili ku-please Miungu yao iwafanyie wepesi.

Kuna jamii zilikua zinaua watoto vilema au kuwatoa KAFARA kwa Mizimu yao zikiàmini ni LAANA na MIKOSI

Kuna jamii zilikua zina ua na kuwala watu wa jamii zingine wakiamini ni BARAKA

Kuna jamii kiongozi akifa alikua "anasindikizwa" na vijakazi waliozikwa hai kama ishara ya UTAKATIFU nk nk

Hawa walifanya kwa DHAMIRA safi kabisa na iliyokubalika na jamii nzima kama ndio njia SAHIHI kwasababu MUNGU muweza wa yote alishindwa kuwapatia sheria zake on time.

Je watahesabiwa wanadhambi au wana haki mbele ya HUKUMU?
 
Ujinga upi mbona unalazimisha unachoamin. Ukiwa unauliza swali subir jibu sio uje na jibu na kuona watu ni wajinga. Nimekuambia watu ambao walikufa kabla ya Yesu kuja humu dunian watahukumiwa na zile sheria zao walizojiwekea wenyewe. Maana kama sheria zao wenyewe walishindwa kuzifuata hata sheria ya Mungu hawawez kuzifuata. Na usisahau sheria za binadam karibu asilimia 80 ni zile zile za Mungu. Yesu aliwashukia kuzimu kuwahubiria roho zilizokataa wakati wa nuhu ili wote tuhukumiwe pamoja. Sio lazima usome bibilia ya king James. Kuna Ethiopian Bible ina maelezo marefu zaid. Ambayo haikupita mikonon mwa mzungu. Pili yale unayoamin usilazimishe watu waamin au usione ujinga ufaham wa mtu kila mtu ana hatima yake. Ndio wazungu wanatuona vilaza. Unauliza swali ukiwa unajibu lako sasa sijui unataka usaidiwe nini.
Ahaa kwahiyo wewe hutaki kulazimishwa ila unataka ulazimishe wewe unachoamini hata kama ni ujinga na tusiuhoji wala kuukosoa eti?
 
Acha kufokafoka una stress au? Jadiliana kwa hoja sio kwa mawazo yako kila mtu anaweza kufikiri ila tunazidiana uwezo! Ndiomaana ata tukifanya mitihani kuna alotangulia wengine wakafata! Sasa waafrika wajinga! We muingereza tupe mawazo yako na fikra zako ambazo hujaletewa!
Period!!
Wewe unajadili kwa hoja na uperiod wako?
 
Acha kufokafoka una stress au? Jadiliana kwa hoja sio kwa mawazo yako kila mtu anaweza kufikiri ila tunazidiana uwezo! Ndiomaana ata tukifanya mitihani kuna alotangulia wengine wakafata! Sasa waafrika wajinga! We muingereza tupe mawazo yako na fikra zako ambazo hujaletewa!
Period!!
Sasa ukiwa mjinga kama huvi ulivyo unataka uambiwe una akili?
 
Iwapo kuna mbinguni na kuzimu wanakoenda Wafrika wakifa je kabla ya wamisionari walienda wapi?
Walioenda kuwa misukule. Wote walikuwa wanakufa Kisha wanaenda kutumika ama kuzalisha sehemu, haswa nyumbani mwa wachawi.
 
Nataka nijibu kwa ujumla hili swala,muamini kuwa hizi dini ni za kuja na tuliingiziwa ili tuzifuate,sijasema kuwa imani yao si ya kweli na nieleweke kuwa kila jamii ina dini yake wakulya,wasambaa,wazungu,waarabu nk, lakini kitendo cha wazee wetu kukubali kuingiziwa imani ya watu wengine na kuikubali walikosea sana na laana ya kutekwa kisaikolojia na kutawalika mpaka sasa! Kwa hiyo wazungu walituwahi kuingiza imani yao kwetu,na laiti tungejua mapema nasi tungewawahi tukawapelekea ya kwetu nao sasa wangekuwa wanalalamika kama sisi, tulizidiwa ujanja na ili wajipenyeze kiurahsi walianza kutuaminisha kuwa dini zetu si za kweli kisha wao wakatwambia zao ndizo za kweli. Wakuu kila dini au imani ya mtu ni ya kweli hivyo tusilazimishane,kama ushakubali kuinizwa mkenge na kuamini muhamadi na Yesu amini hivyo hivyo usimsumbue anaye amini vinginevyo. lakini dini hizi(ukristo & uislamu) si tamaduni za kiafrika tangu kale.
 
Huu ndiyo ujinga wenyewe kwahiyo kuzimu na ahera vimekuwepo au vimeanza baada ya wamisionari kuja Afrika au Mungu kavianzisha baada ya wamisionari kuja Afrika?
Hilo ndio swali
Hao waliokuja kuwafundisha kusoma, kuandika, kuwajengea mahospitali walisukumwa na hiyo hiyo imani unayoikandia.
Alf leo wanachat walikuwa hawajui chochote
 
Hamna aliyesema wanaenda wapi kwa usahihi
Watu wanaeleza Historia

Walikuwa hawajaui , hawajapata hiyo injili ,
Kama hawakupata wangejuaje?
Na wameenda wapi
Je wamechomwa moto au wanaenda mbinguni?
 
Back
Top Bottom