Lwiva
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 22,772
- 32,649
Kuhusu kutenda matendo ya ovyo na kuona sawa ...wewe hujui msingi wa dini ya asili ya kujua mema na mabaya unavyo fanya kazi...hata Kaini alivyo muua ndugu yake aliona sawa.. ila MSINGI WA DINI YA ASILI UNASEMA USIWATENDEE WENZAKO YALE AMBAYO WEWE USINGE PENDA KUTENDEWA ...Dhambi ni NADHARIA tu
Mema, maovu na haki ni MTAZAMO tu
Mfano
Kula nguruwe kunywa pombe ni DHAMBI kwa Waislam lakini sio kwa Wakristo wa RC
Kuoa wake wengi ni Dhambi kwa Wkristo lakini Sahihi kwa Waislam
Bangi ni Kosa OVU Tz lakini ni HALALI Jamaica
Kuna mambo mengi sana ambayo ni KOSA jamii A lakini ni SAHIHI jamii B
Uli unielewe vizuri ni hivi, Kukitokea Janga mfano korona tuliona makanisani na misikitini watu wakifanya SALA za kuomba Mungu atuepushe na janga kwasababu wanaamini na kuona ni SAHIHI......... Zamani kabla ya Dini hizi kunajamii likitokea Janga wanatoa kafara kwa kuua watu tena kikatili ikiwemo kuchomwa moto ukiwa hai ili janga hilo liishe.
Kuna jamii zilikua zinaona ni SAHIHI kabisa kuua mtoto kilema kwasbabu ukimuacha ni LAANA kwenye ukoo
Na mambo mengine mabaya kabisa LAKINI jamii iliamini na kusheherekea kama ni mambo MEMA na SAHIHI.
Je hawa wanahukumiwa vipi?
Sisi tuna bahati sana tumezaliwa kizazi ambacho Dunia imekua CIVILIZED kitambo....... Zama hizo kabla ya hizi dini mpya na civilization watu walikua wanafanya mambo ya HOVYO sana kwa mtazamo wa kizazi hiki na dini mpya lakini wenyewe walikua wanao sawa sawa kabisa
msingi upo hivi
1)USITENDE MABAYA YALE AMBAYO DHAMIRA YAKO YAKUSHUHUDIA KUWA NI MABAYA.
2)TENDA MEMA YALE AMBAYO DHAMIRA YAKO YAKUDMSHUHUDIA KUWA NI MEMA.
3)USIWATENDEE WATU YALE AMBAYO WEWE USINGE PENDA KUTENDEWA .
msingi ni huu ...ukiyaishi haya uwezi kupokea hukumu ya adhabu hata kama ulikuwa una abudu mti kwa sababu unakuwa na jina la WOKOVU NALO NI 👉MTU WA HAKI ...Kuwa mtu wa haki akutegemeo dini zaidi...unaweza usiwe na dini na ukatambulika na Mungu kuwa ni mtu wa haki