Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Maelezo yako ni sahihi kuwa uwekezaji una tija. Ninalopinga kuhusu Mkataba wa bandari ni kampuni ya DPW kuwekeza kupitia mgongo wa nchi yao, Dubai. Mkataba wa IGA, una vifungu vinavyoipa DPW hadhi ya nchi.

Kwa kuwa DPW ina uwezo na uzoefu wa kuendesha bandari, tayari tarehe 28/2/2022 ilikuwa imeingia Mkataba wa Maelewano (Mou) na TPA. Haingii akilini kwa nini DPW haikuendelea na mpango huo, ikajisajiri BRELA kuanza kazi kwa kushirikiana na TPA, badala ya kulazimu Tanzania iingie Mkataba na Dubai, nchi yake, wenye masharti tata km Ibara ya 5(1,4)? Nia ya IGA ni nini wakati kuna makampuni mengi tu km ubinafsishaji wa mabenki wakati wa Mkapa na makampuni ya uchimbaji madini, ambayo naamini hakuna mikataba kati ya Tanzania na nchi zao, kwa kuwa tuna mahusiano ya kidemokrasia.
Mkuu unaweza kuuweka hapa huo mkataba kati ya DP na TPA?
Inaonekan Kuna hatuna nimepitwa.
Ninachojua mkataba huo bado ila utafuata katika Ile mikataba midogo midogo ambayo itakuja baada ya huu wa Tanzania na Dubai.
 
Umeandika mengi ya msingi, lakini mkuu The Boss Kwa nini mkataba hauna ukomo?.

2. Kwa nini mkataba haujajumuisha bandari za Zanzibar?.

3. Kwa Nini apewe bandari zote mtu mmoja, mfano ataendeleza vipi bandari ya mtwara hali yakua anamiliki na bandari ya Msumbiji?.

4. Kwa Nini anaonekana kua na kesi nyingi kwenye bandari za Afrika alizowekeza?.

Hakuna ntanzania yeyote anaekataa uwekezaji, lakini watu wanakataa baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye mkataba. Mfano wewe unaona nisahihi kubadili Sheria za nchi Kwa sababu ya muwekezaji mmoja?.

Kwa Nini apewe aridhi yeyote atakayoomba, na Serikali ndio iwajibike kulipa fidia Kwa wahanga?.

Ushawahi Kwa utashi na akili zako kuona mkataba usio na ukomo?. Nje nahuu wa Aliosaini Tz?.

Tulitunga Sheria kua masuala yote yanayohusu wawekezaji kesi zao zitatuliwe ndani ya nchi, Kwa Nini kwahuyu Serikali ikubali kua yeye kesi yake itakua S Afrika?.

Watanzania wakipindi Cha mkapa sio hawa waleo.

Kheri tubaki na Tanganyika yetu nawao wabaki na Zanzibar yao.
Hapo kwenye kupewa mtu mmoja labda hujuwi mwendeshaji ni mamlaka ya dubai huyo siyo mtu mmoja halafu ana uwezo wa kifedha. Hapo bandarini ni wizi tu unaendelea mifumo zaidi ya 30 na haisomani tunataka tuondoe huu uchafu watanzania msiwe na wasiwasi .mazuri yanakuja
 
Kiukweli sijasoma,siwezi poteza muda wangu kusoma mambo yaliyofanyika nikiwa primary school na secondary school. Ninachojua Samia ni kilaza tena kilaza number moja.
Tulieni mletewe maendeleo zama za kupeleka miradi yote chato zimepita
 
Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika Kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25.

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi.

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa. ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena?

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine?

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.
Wee jamaa Mungu akusamehe bure. Unaongelea kubinafsishwa mashirika ambayo kweli mengi yaliuzwa kiholela na kubinafsishwa vipande vipande vya ardhi tena uwekezaji wa majini kwa kikampuni kimoja huku ukiwa umejifunga mwenyewe kwenye mkataba? Emb Acha ujinga!
 
Nyerere hakuwa Mungu anaejua kila kitu...it's time muanze kuelewa hili..

Serikali haziwezi kuanzisha biashara zikafanikiwa ..ndo maana Kikwete alikuja anzisha Tanzania womens Bank na wakajaribu kuifufua Tanzania Investment Bank na zote zimekufa kabla hazijafikisha hata miaka 7...
Mjifunze na kuelewa
Usikalili kuwa serikali haiwezi kufanya biashara.... mbona uchina na Taiwan wanafanya vizuri tuu. Halotel yenyewe ni campuni ya serikali Vietnam. Usikalili maisha mkuu
 
Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika Kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25.

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi.

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa. ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena?

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine?

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.
DP world kawekeza USA?
Are you out of your mind?
Mwaka 2006 Bunge la Marekani iliwapiga stop DP world.
Acha kuwadanganya watu wewe.
 
Hako ni kakipande kadogo tu ka maongezi yake. Kaongea mengi sana na kudadavua kisheria. Nilipatwa na hasira tu nikaacha kusikiliza maana inatia uchungu.

Sijui tumerogwa na nani sisi 😬😬😬
Niwekee summary kasemaje kama mikataba midogo itataja ukomo ambao yeye anaona ni issue kubwa.
 
Hta
Hizi mada ni za wasomi,
wale wanaopiga makelele ya bandari kuuzwa, wakati wanaishi nyanda za juu kusini mwa mwakaleli na wengine wanazungusha bodadaboda huko nyegezi hawataelewa kitu
Hata boda boda pia inahitaji bandari kwa spare, mafuta hata yenyewe hivyo mkataba unamgusa kila mwananchi na vizazi vinavyokuja, Kwa migogoro na mifumo iliopo mipakani kama Tunduma na Namanga bandari sio kipaumbele kwa sasa.
 
Mkuu unaweza kuuweka hapa huo mkataba kati ya DP na TPA?
Inaonekan Kuna hatuna nimepitwa.
Ninachojua mkataba huo bado ila utafuata katika Ile mikataba midogo midogo ambayo itakuja baada ya huu wa Tanzania na Dubai.
MoU kati ya TPA na DPW umetajwa kwenye mkataba wa IGA (Utangulizi, Kifungu "B", ukarasa 4) ninaoshauri utupiliwe mbali na DPW ipitie TIC kama ina nia ya dhati kuwekeza au ingie ubia na TPA, kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo
 
Yaani nikifikiria Tanesco na Net group solutions, thank God ulikuwa mkataba una muda.Wakabuma wakaondolewa.Sasa huu wa ⏰100 na Dubei ni wa milele.Yaani hata wakivurunda hakuna kuwafukuza.
Pengine ziara za Dubai zitaibua mengine mengi ya hovyo mikataba yote 37 aliyosaini itakuwa na shida tu
 
Kwani hujui propaganda mkuu, watu wanashambulia watu badala ya hoja ili kuhakikisha kila anaepinga aonekane kama muonevu au dhalimu kwa kupitia victimization ya kikundi flani.

Na Mimi ninachoamini kuna kitu kinaendelea chini kwa chini, kwa nini huu mkataba ulio na makosa ya wazi uwekwe wazi tofauti na mingi tu tusioijua.

Mimi nipo na popcorn nikisubiria kuona ni nini kitaendelea
Muda utayafunua mengi sana
 
Huyu jamaa sijui Nyerere alimkosea nini, Kutwa kumuandama tu.
 
Kinachonisikitisha ni kushindwa kufahamu kwamba uendeshwaji wa benki za kibiashara (Commercial Banks) ndani ya nchi, hutegemea sana sheria na sera za uchumi (Fiscal & Monetary Policies) ambazo zinaratibiwa na benki kuu ya nchi ya Tanzania. Mabenki ni makampuni, lakini uendeshwaji wake hauko sawa na makampuni mengine. Mabenki hutumia mfumo wa FRACTIONAL RESERVE BANKING & QUANTITIVE EASING , kusema ni pesa za nje peke yake na wawekezaji ndiyo wametuinia ni kututukana watanganyika.

Hivyo unavyotoa mifano ya CRDB na NMB kufanikiwa, fahamu fika kwamba BOT imefanya kazi kubwa mno hadi hizi benki kusimama. Raisi Mkapa ataendelea kulalamikiwa kwasababu yeye aliziuza hizi benki kiholela jambo ambalo halikuwa sahihi kabisa. Halafu kama umefuatilia vizuri, kuna sababu nyingine kadhaa wa kadhaa, zinazofanya benki ya NMB kufanikiwa, mbali na mitaji ya wazungu au kuwa na wateja wengi. Hapa bado sijazungumzia uwiano mkubwa baina ya THE BANKING SECTOR in relation to other CAPITAL MARKETS.

Nashangaa wewe umeshindwa kung'amua jambo rahisi kabisa ambalo hata mtoto wa chuo angeweza kuling'amua. Mkataba wa bandari na mkataba wa ubinafsishwaji wa mashirika ya ummah kipindi cha Mkapa ni tofauti kabisa. Kwenye mikataba mingi ya Raisi Mkapa, Tanzania bado inamiliki hisa za kutosha ambazo zinaipa nchi nguvu kubwa ya maamuzi hasa kwenye upigaji wa kura. Kubwa zaidi ni kwamba maamuzi ya mwisho ya usimamiz wa hizi benki uko chini ya usimamizi wa BOT na siyo wawekezaji wa nje.

Mkataba wa DP World, unainyang'anya Tanzania haki ya kufanya chochote kile. Tena hata kufikiria walishindwa wakasaini mkataba baina ya Tanzania na DP World ambalo ni shirika binafsi. Kule Djibouti, serikali iliunda kampuni ambalo liliingia ubia na DP World na kumiliki hisa zaidi ya asilimia 60%. Sisi huku tumefanya mambo ya hovyo kupita kiasi, ambapo zaidi ya kukusanya kodi hatuna chetu. Hivyo hata wafanyakazi wa bandari wanaweza kufukuzwa na tusiseme chochote kile.

Kikubwa mkataba huu wa bandari ni LOCK-OUT AGREEMENT, ambapo imewekwa bayana kabisa kwamba mashirika mengine ya ndani au kutoka nje hayataruhusiwa kuja kuwekeza kwenye bandari za Tanzania. Hivyo DP World wamepewa EXCLUSIVE RIGHT OF OWNERSHIP WHICH CREATES A MONOPOLY OVER OUR NATIONAL ASSETS. Mtu yoyote yule mwenye akili timamu na mwenye uzalendo na hii nchi, kamwe hawezi kushabikia huu ufedhuli.

Kule Uingereza ambako haki za binadamu zimeshika hatamu, DP World ilifukuza maelfu ya wafanyakazi wa kizungu wa shirika la P&O Ferries baada ya kulinunua. Sasa huko ni Uingereza, hapa Tanzania unadhani kitawakuta nini wale wafanyakazi wa bandari ? Mambo mengine muwe mnatumia akili nyie watu, siyo matumbo. Sasa hebu nikupashe kidogo:

Mwaka 2020, serikali ya Djibouti ilifunguliwa mashitaka na shirika la DP WORLD kwasababu lilivunja haki yake ya umiliki wa bandari za Djibouti bila kuingiliwa (Breach of Exclusive Rights), kwasababu serikali ilitaka kulipa shirika la China Merchants haki ya kuwekeza kwenye bandari ya Doraleh. Serikali ya Djibouti na China Mechants ziliburuzwa kwenye mahakama za kimataifa na kuamriwa walipe dola za Kimarekani milioni 200.

Ikumbukwe China Merchants ndiyo shirika linalotaka kuanzisha mradi wa bandari ya Bagamoyo, lakini baada ya huu mkataba kupita hiyo haki hawana tena. Unafahamu nini kinaenda kutokea hapa ? Bandari ya Bagamoyo inaweza ikaenda kujengwa nchini Kenya na tusibaki tunaamini chochote hapa. Ikumbukwe mpango wa serikali ya Uchina kipindi cha Raisi Hu Jintao ni kwamba bandari ijengwe kule Kenya lakini wakaamua kujenga Tanganyika. Sasa hapa unadhani nini kitawazuia wakenya kuwaruhusu wachina wajenge Kenya ? Subirini muone...

MWISHO KABISA:
Leo nimemsikiliza Tundu Lissu akichambua kuhusu mkataba wa DP World, ambapo amesema kwamba huu ndiyo mkataba wa ajabu kuwahi kusainiwa na serikali ya Tanganyika tokea mwaka 1920. Mimi nasema amekosea na hajafanya tafiti za kutosha. Mkataba kama huu ulishawahi kusainiwa na serikali ya Muingereza, Mbelgiji na Mfaransa juu ya matumizi ya bandari ya Dar es salaam.

Mkataba ulihusisha makoloni ya Tanganyika, Rwanda, Burundi na Congo DRC na uliitwa THE BELBASE TREATY, ambao ulisema kwamba makoloni ya Rwanda, Burundi na Congo yataruhusiwa kutumia bandari ya Dar es salaam kwa kipindi kisicho na ukomo (Infinitely/Indefinate Time), huku wakilipa kiasi cha paundi 2 za Uingereza kwa serikali ya Tanganyika. Mwalimu Nyerere kawa Waziri Mkuu akaukuta huu mkataba, yeye na Mzee Lusinde akiwa waziri mwenye dhamana waliuvunja huu mkataba bila kufikiria mara mbili kwasababu ulilenga kuiumiza Tanganyika na kuuza uhuru wake.

Hii IGA baina ya Tanzania na Dubai, ina mahadhi hayohayo ya The Belbase Treaty, kwamba waarabu wapewe bandari zetu zote za Tanganyika kwa kipindi kisicho na ukomo. Halafu wakaenda mbali zaidi kusema kwamba "Even in case of state succession, a new state shall be bound by the same treaty." Wakimaanisha kwamba hata leo hii muungano ukivunjika, serikali ya Tanganyika itakuwa imefungwa na huo mkataba ambao umesainiwa na watu watatu kutoka Zanzibar. Sasa kama huku siyo kuiuza Tanganyika ni nini ?

NB 1: Kila siku nilikuwa najiuliza nini kilipelekea wafaransa (The Jacobins) wakachanganyikiwa na kuwa na hasira kiasi cha kumuua mfalme wao Louis IV na familia yake bila huruma, kumbe mambo huwa yanaanzaga hivihivi.

Kule Yugoslavia muungano wao ulikuwa na amani kwelikweli kipindi cha mkomunisti Josep Broz Tito, lakini huwezi kuamini jinsi ambavyo wakristo wa kutoka Serbia walifanya ukatili kwa kuua maelfu wa Waislamu kutoka Bosnia na Kosovo kisa tu hawa waislamu walikuwa wanataka uhuru wao, hivyo wakaanza kushirikiana na mataifa ya kiislamu kama Uturuki ili kuhujumu nchi. Hadi leo Serbia, Bosnia na Croatia ni maadui utadhani siyo ndugu (Slavs) waliowahi kuwa nchi moja.

NB 2: Ukweli tunaufahamu kwamba mbali na kusingizio cha kufungua nchi na kuita wawekezaji kutoka nje, nyuma ya hizi siasa za Raisi Samia kuna kaharufu kakali ka UDINI. Wengi mnamtetea Samia kwasababu tu ni mwenzenu kwenye imani. Hata wengine wanaomponda na kumkosoa wanafanya hivyo kwasababu za kidini, hata kama hapa watapinga. Sasa kama mambo ndiyo yako hivi, siku siyo nyingi Tanzania itakuwa imejaa chuki kubwa mno ya DINI.

Watanzania meingizwa kwenye mtego na ninyi mmejaa mazima.....Nawapa pole!
Big up Sana , UMEONGEA kizalendo Sana na sio KISHABIKI.
Tufike MAHALI , WA Tz tuachane Kabisa na utani ama ushabiki katika masuala ya kisiasa. Tunapoikumbatia tabia hii ndio inachochea zaidi maadui WA Taifa yaani Udini, Ukabila, ukanda , n.k . KUAMKA na kutuangamiza vibaya mno.
 
Back
Top Bottom