Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika Kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25.

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi.

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa. ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena?

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine?

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.
Umeandika mengi lakini nje, kuna msemo wa kilatini tafsiri ya ni "Run very well but outside the tracks"

Shida ya watangányika sio kuletwa DP World, shida ni huo mkataba wao, fullstop. Sasa wewe unaongea meeeengi, hujaelewa tatizo la wanaopinga ni nini?

Kila mtu mwenye akili timamu na exposure hawezi katalia ujio wa DP World (Nikiwemo mimi) tunachokatalia ni terms za huo mkatabamkataba. Umesema DP World wapo hadi china, sawa, tuletee mkataba wake na china af tuwekee na mkataba waliotupa sisi. Ukifanya hivo nikakuta terms ni zile zile walotupa sisi mods mnipige ban la maisha
 
Kwa akili yako umeona hoja yeyote hapo?
Watanzania ni wapumbavu sana, yaani ni sawa na mbuzi wanaopelekwa machinjoni, na hawaoni shida ni kuswagwa tu mbuzi kabisa!!

Nchi ya mataahira, unaweza hata kujuta kuzaliwa nchi iliyozaliwa mbuzi kama nyie!!
 
HGA inaweza kuwa kinyume na intergovernmental agreement iliyopitishwa na Bunge? Kwanini kuwe na intergovernmental agreement tena iliyopelekwa bungeni isiyoainisha kiasi cha uwekezaji na faida zake ili HGA zipate muongozo sahihi?
Iwe kinyume kivipi wakati IGA imesema mambo yote yatawekwa kwenyr HGA?
 
Kinachonisikitisha ni kushindwa kufahamu kwamba uendeshwaji wa benki za kibiashara (Commercial Banks) ndani ya nchi, hutegemea sana sheria na sera za uchumi (Fiscal & Monetary Policies) ambazo zinaratibiwa na benki kuu ya nchi ya Tanzania. Mabenki ni makampuni, lakini uendeshwaji wake hauko sawa na makampuni mengine. Kusema ni pesa za nje peke yake ni makosa ilhali tunatumia mfumo wa FRACTIONAL RESERVE BANKING.

Hivyo unavyotoa mifano ya CRDB na NMB kufanikiwa, fahamu fika kwamba BOT imefanya kazi kubwa mno hadi hizi benki kusimama. Raisi Mkapa ataendelea kulalamikiwa kwasababu yeye aliziuza hizi benki kiholela jambo ambalo halikuwa sahihi kabisa. Halafu kama umefuatilia vizuri, kuna sababu nyingine kadhaa wa kadhaa, zinazofanya benki ya NMB kufanikiwa, mbali na mitaji ya wazungu.

Lakini mwisho kabisa nashangaa wewe umeshindwa kung'amua jambo rahisi kabisa ambalo hata mtoto wa chuo angeweza kuling'amua. Mkataba wa bandari na mkataba wa ubinafsishwaji wa mashirika ya ummah kipindi cha Mkapa ni tofauti kabisa. Kwenye mikataba mingi ya Raisi Mkapa, Tanzania bado inamiliki hisa za kutosha ambazo zinaipa nchi nguvu kubwa ya maamuzi hasa kwenye upigaji wa kura. Kubwa zaidi ni kwamba maamuzi ya mwisho ya usimamiz wa hizi benki uko chini ya usimamizi wa BOT na siyo wawekezaji wa nje.

Mkataba wa DP World, unainyang'anya Tanzania haki ya kufanya chochote kile. Tena hata kufikiria walishindwa wakasaini mkataba baina ya Tanzania na DP World ambalo ni shirika binafsi. Kule Djibouti, serikali iliunda kampuni ambalo liliingia ubia na DP World na kumiliki hisa zaidi ya asilimia 60%. Sisi huku tumefanya mambo ya hovyo kupita kiasi, ambapo zaidi ya kukusanya kodi hatuna chetu. Hivyo hata wafanyakazi wa bandari wanaweza kufukuzwa na tusiseme chochote kile.

Kikubwa mkataba huu wa bandari ni LOCK-OUT AGREEMENT, ambapo imewekwa bayana kabisa kwamba mashirika mengine ya ndani au kutoka nje hayataruhusiwa kuja kuwekeza kwenye bandari za Tanzania. Hivyo DP World wamepewa EXCLUSIVE RIGHT OF OWNERSHIP WHICH CREATES A MONOPOLY. Mtu yoyote yule mwenye akili timamu na mwenye uzalendo na hii nchi, kamwe hawezi kushabikia huu ufedhuli.

Kule Uingereza ambako haki za binadamu zimeshika hatamu, DP World ilifukuza maelfu ya wafanyakazi wa kizungu wa shirika la P&O Ferries baada ya kulinunua. Sasa huko ni Uingereza, hapa Tanzania unadhani kitawakuta nini wale wafanyakazi wa bandari ? Mambo mengine muwe mnatumia akili nyie watu, siyo matumbo. Sasa hebu nikupashe kidogo:

Mwaka 2020, serikali ya Djibouti ilifunguliwa mashitaka na shirika la DP WORLD kwasababu lilivunja haki yake ya umiliki wa bandari za Djibouti bila kuingiliwa (Breach of Exclusive Rights), kwasababu serikali ilitaka kulipa shirika la China Merchants haki ya kuwekeza kwenye bandari ya Doraleh. Serikali ya Djibouti na China Mechants ziliburuzwa kwenye mahakama za kimataifa na kuamriwa walipe dola za Kimarekani milioni 200.

Ikumbukwe China Merchants ndiyo shirika linalotaka kuanzisha mradi wa bandari ya Bagamoyo, lakini baada ya huu mkataba kupita hiyo haki hawana tena. Unafahamu nini kinaenda kutokea hapa ? Bandari ya Bagamoyo inaweza ikaenda kujengwa nchini Kenya na tusibaki tunaamini chochote hapa. Ikumbukwe mpango wa serikali ya Uchina kipindi cha Raisi Hu Jintao ni kwamba bandari ijengwe kule Kenya lakini wakaamua kujenga Tanganyika. Sasa hapa unadhani nini kitawazuia wakenya kuwaruhusu wachina wajenge Kenya ? Subirini muone...

MWISHO KABISA:
Leo nimemsikiliza Tundu Lissu akichambua kuhusu mkataba wa DP World, ambapo amesema kwamba huu ndiyo mkataba wa ajabu kuwahi kusainiwa na serikali ya Tanganyika tokea mwaka 1920. Mimi nasema amekosea na hajafanya tafiti za kutosha. Mkataba kama huu ulishawahi kusainiwa na serikali ya Muingereza, Mbelgiji na Mfaransa juu ya matumizi ya bandari ya Dar es salaam.

Mkataba ulihusisha makoloni ya Tanganyika, Rwanda, Burundi na Congo DRC na uliitwa THE BELBASE TREATY, ambao ulisema kwamba makoloni ya Rwanda, Burundi na Congo yataruhusiwa kutumia bandari ya Dar es salaam kwa kipindi kisicho na ukomo (Infinitely/Indefinate Time), huku wakilipa kiasi cha paundi 2 za Uingereza kwa serikali ya Tanganyika. Mwalimu Nyerere kawa Waziri Mkuu akaukuta huu mkataba, yeye na Mzee Lusinde akiwa waziri mwenye dhamana waliuvunja huu mkataba bila kufikiria mara mbili kwasababu ulilenga kuiumiza Tanganyika na kuuza uhuru wake.

Hii IGA baina ya Tanzania na Dubai, ina mahadhi hayohayo ya The Belbase Treaty, kwamba waarabu wapewe bandari zetu zote za Tanganyika kwa kipindi kisicho na ukomo. Halafu wakaenda mbali zaidi kusema kwamba "Even in case of state succession, a new state shall be bound by the same treaty." Wakimaanisha kwamba hata leo hii muungano ukivunjika, serikali ya Tanganyika itakuwa imefungwa na huo mkataba ambao umesainiwa na watu watatu kutoka Zanzibar. Sasa kama huku siyo kuiuza Tanganyika ni nini ?

NB 1: Kila siku nilikuwa najiuliza nini kilipelekea wafaransa (The Jacobins) wakachanganyikiwa na kuwa na hasira kiasi cha kumuua mfalme wao Louis IV na familia yake bila huruma, kumbe mambo huwa yanaanzaga hivihivi.

Kule Yugoslavia muungano wao ulikuwa na amani kwelikweli kipindi cha mkomunisti Josep Broz Tito, lakini huwezi kuamini jinsi ambavyo wakristo wa kutoka Serbia walifanya ukatili kwa kuua maelfu wa Waislamu kutoka Bosnia na Kosovo kisa tu hawa waislamu walikuwa wanataka uhuru wao, hivyo wakaanza kushirikiana na mataifa ya kiislamu kama Uturuki ili kuhujumu nchi. Hadi leo Serbia, Bosnia na Croatia ni maadui utadhani siyo ndugu (Slavs) waliowahi kuwa nchi moja.

NB 2: Ukweli tunaufahamu kwamba mbali na kusingizio cha kufungua nchi na kuita wawekezaji kutoka nje, nyuma ya hizi siasa za Raisi Samia kuna kaharufu kakali ka UDINI. Wengi mnamtete Samia kwasababu tu ni mwenzenu kwenye imani. Hata wengine wanaomponda wanafanya hivyo kwasababu za kidini, hata kama watapinga. Sasa kama mambo ndiyo yako hivi, siku siyo nyingi Tanzania itakuwa imejaa chuki kubwa mno ya DINI.

Watanzania meingizwa kwenye mtego na ninyi mmejaa mazima.....Nawapa pole!
Huyu The Boss kapotea njia.

Nimemwambia hata mimi, shida huo mkataba. Atuwekee hapa mkataba wa DP world na china au usa kisha tuulinganisha mkataba wao na Tanzania.

Af mtu na akili zako kweli unaweza linganisha situation ya banking sector na hii issue ya port? Kwa aina hii ya watanzania bado tuko na safari ndefu, no hatuna safari tena coz tushashindwa hio safari
 
Sisi wengine tulikuwepo wakati Rais Mkapa (1995-2005)anatukanwa kila siku kuwa "anauza nchi Kwa makaburu".....ilifikia wakati hadi nyimbo zilitungwa zikimuimba naukumbuka wimbo mmoja .."Kama sio juhudi zako Nyerere, Mkapa angeuza nini"???..Mkapa alikuwa anatukanwa kisa ni kuleta wawekezaji wa kampuni zisizo zaidi tano kutoka Afrika Kusini..
Walikuja kuwekeza
1.TBL
2.. NBC
Zingine nimezisahau....Leo...

Uwekezaji wa NBC ulipelekea Serikali kuanzisha NMB ambayo nayo waliletwa Waholanzi kununua hisa zisizozidi asilimia 5..waka provide management baadae waholanzi wale wakashangaa jinsi soko lilivyo kubwa wakaomba kununua hisa zaidi now nasikia ni asilimia 25.

Mabadiliko ya sekta nzima ya Benki aliyoyasimamia Rais Mkapa kipindi kile Leo yamepelekea tuwe na sector ya bank kubwa inayofanya kazi Kwa ufanisi.

NMB Leo ni kubwa kuliko Zanzibar GDP..na bank zote 3 kubwa Tanzania.. NMB, NBC na Crdb ni kubwa kuliko Uchumi wa Burundi...

Haya yote yasingewekana kama Rais Mkapa angeogopa "kuitwa fisadi anaeuza nchi Kwa Makaburu"...kipindi kile usingeweza kumuelewa Mkapa ...since watu waliokuwa wanaompinga walikuwa Wana influence ya kutosha ..tukianzia na Mwl Nyerere.....Na Magazeti ya Jenerali Ulimwengu yaliyokuwa Yana influence kubwa Sana Kwa jamii ya wasomi na wakosoaji wakubwa. ungeweza fikiri nchi inauzwa kweli ukifatilia mijadala...

Leo hizo banks zote 3.. NMB na Crdb zinamilkiwa na watanzania asilimia 70 NBC pia Serikali bado ina hisa za kutosha na zote hizo serikali inapokea gawio la kutosha...wale waliokuwa wanasema Mkapa anauza nchi Kwa makaburu wamenyamaza kiimya na sasa wamehamia kwenye "Samia anauza nchi Kwa waarabu" as if nothing happened...wala hawajawi jiuliza walichokuwa wanapinga kipindi kile na Hali ikoje leo? Walikuwa sahihi??

Kama hawakuwa sahihi kwanini wasiombe hata radhi in public hapo hata waliokuwa washauri wa Mkapa ambao bado wako hai wafarijike??...kama Mkapa aliuza nchi Kwa makaburu, hii nchi wanayosema anauza Samia ni ipi tena?

Itoshe kusema TBL ilienda kuwa kampuni inayolipa Kodi kubwa kuliko kampuni zote Tanzania Kwa miaka mingi Sana kama sio mpaka Leo ninavyoandika hapa....lakini shukran pekee aliyoambulia Rais Mkapa ni kuitwa "fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu"...

Na wale watukanaji wakubwa Hadi Leo hawajawi kusema "hatukuwa sahihi" tulikosea ...Sana Sana wamevamia basi jipya "la Samia anauza nchi Kwa waarabu" Kwa nguvu mpyaa kabisa ...wazungu wanasema "ignorance is bliss"..

Mtu mjinga ana faida ya kutojijua ujinga wake...anaweza ita hata watu werevu wajinga hadharani bila woga...'ignorance is bliss ".....ungemueleza nini Mtanzania wa kawaida kuwa Mwalimu Nyerere hayuko sahihi ..wakati CEO wa Crdb wakati ule anaenda Hadi Butiama kumuomba Nyerere anunue hata hisa kidogo za Crdb kama kushawishi jamii iamke na Ku embrace"mabadiliko ya uchumi "na Nyerere ananjibu waziwazi mbele ya Tv kuwa hakuna cha mabadiliko wala nini ..ni ubepari na wizi tu kubinafsisha mabenki"...

Kwa watanzania Wengi Nyerere ni close to God ... hawezi kuwa hayuko sahihi..huwa najiuliza kama kipindi kile mwaka 1996 kama Babu yangu angekuwa na Uwezo mdogo Tu na akanunua hisa nyingi Crdb mwaka 1996 mfano hisa zenye thamani ya hata ya milioni 2 mwaka 1996 Leo ingekuwa ni utajiri kiasi gani?but watanzania Wengi hawakuwa na uelewa na waliokuwa wanaopinga mabadiliko ndo hao kina Nyerere na Rais anaeongoza mabadiliko anatukanwa kama "anauza nchi Kwa makaburu"...miaka 17 later ... tunamtukana Rais Kwa kuleta nchini moja ya kampuni 3 kubwa duniani Kwa shughuli za Bandari... Dpworld... kampuni imewekeza kuanzia China Hadi USA Kwa mabingwa wenyewe wa uwekezaji..Hadi Kwa wajerumani mabingwa wa ubaguzi duniani......

Kampuni CEO mmarekani lakini tunaambiwa inakuja "kueneza Uislam"... kampuni imewekeza UK lakini tunaambiwa huko kote imewekeza "fair " Ila kwetu ndo "imeuziwa nchi"...hata serikali inaposema mkataba wa uwekezaji bado kusainiwa hatutaki kuelewa...

Watu unao fikiri Wana uelewa wanatokwa na mapovu kuongea with certain "hatari kubwa Sana " iliyo mbele yetu akija "huyu mwarabu"...na wimbo mpya wa Samia anauza nchi Kwa waarabu ndo unazidi kupandishwa chati Kwa nguvu kubwa... maandamano uchwara yanachochewa na Viongozi wa dini ambao unajiuliza ni Bandari tu au kuna agenda ingine?

The more things change the more they stay the same....
Walio muita Mkapa fisadi anaeuza nchi Kwa makaburu..sasa wanafanya miamala banks zile zile na pengine kununua hisa na kunywa Safari lager huku washasahau "matusi " yote waliyomtwisha Mzee Mkapa...angalau wajitokeze waombe radhi japo hata washauri wa Mzee Mkapa wafarijike...kabla hawajapanda hili basi lingine la "Samia anauza nchi Kwa waarabu"...

Pengine wanaweza wasiwe hai ikitokea haya yote yanayozungumwa Leo yakathibitika kuwa ni uzushi , upumbavu na propaganda za wanasiasa wanaotaka Mama Samia "awapishe kwenye kiti mapema".....ili waombe radhi...Bora kwanza waombe radhi hili la Mkapa ambalo limethibitika bila Shaka kuwa "kelele za Mkapa kuuza nchi Kwa makaburu" ilikuwa uwongo, upumbavu,upeo mdogo kuhusu uchumi na uwekezaji na kudandia mabasi ya propaganda ambayo hujui dereva wake nani.
Tafuta Data ndio uandike kama % za hisa za hizo benk na umiliki wake hujui
 
Privatisation ya rais Mkapa haiwezi kuwa success story ya kuleta wakati mashirika mengi yalikufa, viwanda viligeuka magofu nchi ikaanza upya.

Mbona tunataka kugawa lango la uchumi kwa competitor wetu katika bandari?

Hatupaswi kuwa wajinga kiasi hicho all the time.

Yaani inasikitisha mno mno na bado watu wanaleta hoja za ajabu ajabu zisizoeleweka sijui tatizo ni elimu au ni utindio wa ubongo!!

Hakuna sehemu watu wamewakataa hao DPW, watu wanakataa mkataba mbovu usifaa kwa nchi!! Kweli karne ya leo utaingiza nchi kwenye mkatba mbovu namna hii? Kweli?
 
Saga la NBC in the long run limeiyumbisha sana Tanzania kuliko tunavyoweza kufikiri hasa kiuchumi.
Ilikua ni matakwa ya IMF kuiua NBC ili sekta binafsi ya kibenki iweze furukuta lakini kilichoipata NBC leo hamna mpambe anataka kizungumzia. Sekta ya benki imekua Yes... je implication yake kwa uchumi wa nchi ikoje ukilinganisha na nguvu ya NBC ya wakati ule? Je why benki nyingine zisingekuja kupambana na NBC?

Mkapa amekiri mara nyingi hadharani na kwenye kitabu chake kuwa ubinafsishaji kwa sehemu kubwa alikosea maana 80% ya mashirika ya umma yaliingia mifukoni mwa matapeli!

Hoja zile sile waliosimamia watu juu ya uwezo na aina ya mikataba ya hovyo ya ubinafsishaji ndizo zilikuja kuonekana wazi kweli waliopinga walikua na hoja tena kubwa sana.

Vipi NET group Solutions? ATCL? TRL?
Meremeta? Na mengine?

Shida yetu kubwa tunakimbilia sana kwenye petty issues when it comes to analysis

Mfano huu mkataba wa Tanzania na DP World ni wa hovyo usioelezeka! Hoja si kubinafsisha bandari Hoja ni mkataba wa hovyo!

Madini hadi leo yametufikisha wapi ukitulinganisha na Botswana na SA? Mbona kwao pia kuna sector binafsi?
HOJA sio ubinafsishaji hoja aina ya mikataba ya kishenzi ambayo nchi zetu zinaingia.
Uko vema baharia 💯💯💯
 
Iwe kinyume kivipi wakati IGA imesema mambo yote yatawekwa kwenyr HGA?
Kama HGA ndio kila kitu kulikuwa na umuhimu gani wa IGA? Unajua kwanini IGA na tena kupelekwa bungeni? Kwanini wasingeingia direct agreement TPA and DPW! Why tempering with our President and Parliament? ultimate authority!
 
Kama ni hivyo umuhimu wa IGA ni nini? Unajua kwanini IGA tena kupelekwa bungeni? Kwanini wasingeingia direct agreement TPA and DPW! Why tempering with our President and Parliament? ultimate authority!
Kuna mkataba umeingiwa kuhusu TPA?

Ukielewa tofauti ya IGA na HGA basi hutakuwa na haja ya kuandika haya yote
 
Fanyeni utafiti kwanza,dar port ina berth 7 ya 8 ni ile oil terminal,kwa mujibu wa serikali hapo dar port pekee DP kapewa berth na 6 na 7 tu ambazo ni za cotainer terminal hivi angepewa kuendesha bandari yote ingekuaje!
Sio kwa mujibu wa serikali, nenda kasome mkataba ujionee waarabu walichopewa, wacha ujinga.
 
Kuna mkataba umeingiwa kuhusu TPA?

Ukielewa tofauti ya IGA na HGA basi hutakuwa na haja ya kuandika haya yote
Huo mkataba ni kuhusu bandari and its related economic corridors. Hii ndio IGA iliyopitishwa na bunge. Kama haihusu bandari confirm hapa.

Msidanganye wananchi kuhusu HGA ili wapuuze IGA hii ya ovyo ambayo ndio mkataba mama na umehalalishwa bungeni!
 
Saga la NBC in the long run limeiyumbisha sana Tanzania kuliko tunavyoweza kufikiri hasa kiuchumi.
Ilikua ni matakwa ya IMF kuiua NBC ili sekta binafsi ya kibenki iweze furukuta lakini kilichoipata NBC leo hamna mpambe anataka kizungumzia. Sekta ya benki imekua Yes... je implication yake kwa uchumi wa nchi ikoje ukilinganisha na nguvu ya NBC ya wakati ule? Je why benki nyingine zisingekuja kupambana na NBC?

Mkapa amekiri mara nyingi hadharani na kwenye kitabu chake kuwa ubinafsishaji kwa sehemu kubwa alikosea maana 80% ya mashirika ya umma yaliingia mifukoni mwa matapeli!

Hoja zile sile waliosimamia watu juu ya uwezo na aina ya mikataba ya hovyo ya ubinafsishaji ndizo zilikuja kuonekana wazi kweli waliopinga walikua na hoja tena kubwa sana.

Vipi NET group Solutions? ATCL? TRL?
Meremeta? Na mengine?

Shida yetu kubwa tunakimbilia sana kwenye petty issues when it comes to analysis

Mfano huu mkataba wa Tanzania na DP World ni wa hovyo usioelezeka! Hoja si kubinafsisha bandari Hoja ni mkataba wa hovyo!

Madini hadi leo yametufikisha wapi ukitulinganisha na Botswana na SA? Mbona kwao pia kuna sector binafsi?
HOJA sio ubinafsishaji hoja aina ya mikataba ya kishenzi ambayo nchi zetu zinaingia.
Tatizo, raisi analindwa na katiba, hawezi kushtakiwa. Ingekuwa tuna uwezo wa kumshitaki raisi unadhani angeweza kufanya haya? Tatizo kubwa ni Katiba ya nchi.
 
Nchi iliyojaa mashimo ya migodi huku ikiendesha kampeni za kuongeza madawati mashuleni na kujenga vyoo..

Nchi iliyopo kwenye great lake region na mipaka mikubwa ya bahari lakini kupata clean water tu ni mtihani

By the way

Ulichoongelea ni sawa na wanaopinga pia wapo sawa, instead ya kuwashambulia watu, ungeshambulia hoja.
Hakuna anaekataa mkataba Ila watu wanaomba mkataba uwe na maslahi kwa nchi kwa kufanya amendments kwa vifungu baadhi,

Ungefanya la maana sana kama ungeonesha ubora wa mkataba na sio kuchukua successful story ndogo ya mkapa kwenye privatization kuhalalisha kinachoendelea sasa..

Tusigombee fito na tunajenga nyumba moja ,pinga hoja kwa hoja🙏🏽🙏🏽
what a great lecture!
Mkuu, haya ndo madhara ya kuishi kwenye ilani za vyama na siasa za kukimbizana ikulu, na kuacha mpango wa maendeleo wa taifa pamoja. Raia wamebakia kuuziwa haki zao kwenye majukwaa ya kisiasa kila uchao
 
Mimi nadhani Mama Samia asonge mbele. Akiwasikiliza wanaopinga atachelewa sana kuwaletea watanzania maendeleo
Maendeleo ya watanzania hayawezi kuletwa na chama wala Rais yeyote madarakani, maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe kwa kujitambua, kuwa macho na nyendo za ubadhirifu dhidi ya rasilimali za taita na kupigania haki za kiraia wakati wote.
 
Privatisation ya rais Mkapa haiwezi kuwa success story ya kuleta wakati mashirika mengi yalikufa, viwanda viligeuka magofu nchi ikaanza upya.

Mbona tunataka kugawa lango la uchumi kwa competitor wetu katika bandari?

Hatupaswi kuwa wajinga kiasi hicho all the time.
Yaani nikifikiria Tanesco na Net group solutions, thank God ulikuwa mkataba una muda.Wakabuma wakaondolewa.Sasa huu wa ⏰100 na Dubei ni wa milele.Yaani hata wakivurunda hakuna kuwafukuza.
 
Maendeleo ya watanzania hayawezi kuletwa na chama wala Rais yeyote madarakani, maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe kwa kujitambua, kuwa macho na nyendo za ubadhirifu dhidi ya rasilimali za taita na kupigania haki za kiraia wakati wote.
Na maendeleo ya CHADEMA yataletwa na nani?
 
Back
Top Bottom