Kabla ya kumkosoa Rais Samia, tumuombe radhi kwanza Hayati Mkapa na familia yake na washauri wake

Watanzania tunawapa watu wenye uwezo mdogo kutuongoza matokeo yake ipo siku watatupeleka shimoni na kutuingiza kwenye machafuko makubwa sana.
Viongozi wakizidiwa hoja badala ya kukiri kukosea au kukaa kimya wanatafuta wakuwaunga mkono aidha kwa kupitia dini zao au ukanda walikozaliwa.
Hili la bandari hoja iliyoko mezani ni mkataba kuwa na mapungufu makubwa sana badala ya hizo hoja kujibiwa tayari imegeuzwa kuwa chuki ya udini na uzanzibar.
Inafika kipindi mtu unajiuliza hivi hizi akili za dini na ukabila tunazitoa wapi au tumechoka kuishi kwa amani na upendo.
Wahusika wangejikita kwenye vipengele vinavyohojiwa kwenye mkataba ingekuwa vizuri sana kuliko sasa wanavyoanza kujifichia kwenye dini na ukabila.
 
ukumbuke wakati NBC inabinafsishwa watumishi wangapi waliondolewa kwenye ajira?haya hiyo CRDB niambie riba zao za kinyonyaji ambazo zimewatesa watumishi mpaka leo hii.mtu anakopa 10m na analipa 17m wewe unaona ni sahihi?haya ukienda kwenye TBL ajira zilikuwa zinatolewa kwa ubaguzi lkn wewe hujayaona hayo au sababu na wewe pia ni mnufaika wa hizo dili?hakuna aliyesema bandari imeuzwa shida sisi watz ni wagumu wa kuchakata taarifa.watz hawautaki huo uwekezaji.MOU ni makubaliano ya awali tu lakini kinachofuata sasa ni mitataba ambayo wengi hawajui itakuwa na content na intent gani.kama hayo makubaliano ni halali kwa nini serikali inawalazimisha watz tena kwa kutumia nguvu kubwa?kwani huyo huyo mkapa hakulalamikiwa kuchukua mgodi wa kiwira na baada ya kelele za wadau akautema?mambo si yalianza hivyo hivyo.haya nikukumbushe kampuni ya sigara unajua nini kilitokea pale baada ya kubinafsisha.tuna historia na haya mambo.wewe umezaliwa wakati wa mkapa sisi tuko tangu enzi za mwl na tunaielewa sana hii nchi.
 
Mkumbushe leo aende benki yoyote ya NBC akaone kuna nini kule kama siyo kijiwe tu.hakuna mteja na imeporomoka jumla au halioni hilo?
 
Hizi mada ni za wasomi,
wale wanaopiga makelele ya bandari kuuzwa, wakati wanaishi nyanda za juu kusini mwa mwakaleli na wengine wanazungusha bodadaboda huko nyegezi hawataelewa kitu
Kwakua wengine ni watanzania kuliko wengine.
Huo usomi wenu (wa kukariri makaratas na kujibu maswali) umelisaidia nini taifa hili?
 
Indapo ikifanyika hayo yatawekwa kwenye HGA
HGA inaweza kuwa kinyume na intergovernmental agreement iliyopitishwa na Bunge? Kwanini kuwe na intergovernmental agreement tena iliyopelekwa bungeni isiyoainisha kiasi cha uwekezaji na faida zake ili HGA zipate muongozo sahihi?
 
Kwenye hili suala la bandar nimekua observer mzuri sana.Sijaegemea popote mpaka sasa na ni ngumu sanankujua nani yuko sahihi na asiye sahihi.
Wengi wa watu wanao ongea wanatumia hisia zaid facts hakuna kama sio chache...
Uzur ninacho amini (sjjui kwanini), serikali haiwez ikawa imeweka kila taarifa (hasa za kimkakati) hadharani (kwasabau za kiushindani dhidi ya majirani).
Hivyo nasukumwa kuamini kuwa hiki tunachopigizana nacho kelele ni sehemu tu ya ishu nzima but kuna miamba lazima itakua imejifungia somewhere huko kupambania maslahi mapana kwenye hili sakata.

Sidhani kama serikali imekurupuka.
Huwez pewa wewe mwananchi (tundu lissu. Au mbowe au zitto) ishu nzito kama hizi.
 
POKEA MAUA YAKO MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…