Kabla ya kupeleka gesi yetu Kenya tutafakari kwanza kuhusu haya yafuatayo

Kabla ya kupeleka gesi yetu Kenya tutafakari kwanza kuhusu haya yafuatayo

Hao AFDB ndio wanamwaga tu bila kuangalia uwezo wa nchi kulipa deni? Kama mahindi tu kuvusha yana mizengwe ndio itakuwa gas?
Kama una uwezo hata kidogo kufahamu potential ya uwepo wa viwanda Kenya kwa uchumi KIKANDA na matokeo ya ukuaji wa uchumi kutokana na matumizi ya gesi viwandani..hizo usd 1.1 billion kupeleka bomba la gesi Kenya hata benki za ndani Kenya ukiacha AfDB zinaweza kutoa kwa sababu deni litalipwa hata kabla ya miaka 5..
 
Watanzania tuna ugoigoi katika kutekeleza na kufanikisha yale tunayoyafikiria, tunayoyapanga na hata yale tuliyoamua kuyatekeleza. Mfano, hata wimbo wa kuhamia dodoma uliimbwa kwa miaka mingi sana kabla ya kutekelezwa'

Siku ambayo gesi yetu itafika Kenya, kesho yake tu asubuhi nishati ya gesi hiyo

1. itasambazwa kwenye viwanda vyote vya uzalishaji kuzalisha bidhaa zenye bei nafuu ambazo zitakuja kuuzwa tanzania kwa bei nafuu kuliko zetu.
2. magari yao yote yatatumia gesi hii nafuu
3, kaya zao nyingi zitapikia gesi wakati sisi tukiendelea kupika na mkaa na kuni.
4. Watajenga kiwanda kikubwa cha mbolea wakayotumia kwenye kilimo chao na nyingine kuja kuuzwa tanzania na kwingine.
5. Vifaa na vipuli rahisi, imara na bora vya vifaa vinavyotumia gesi vitajaa kenya na kuingizwa Tanzania pia kuuzwa.
6. Gesi ya kupikia majumbani itatoka Kenya.

Sisi kwetu pamoja na kuwa na gesi kwa miaka mingi lakini tuna umeme ghali, tunapikia kuni na mkaa, na tunaagiza mbolea kutoka ng'ambo.

Watatuchekaaa saaaana, watatuimbaaa saaaana na watatuona mazombie.

Tukazane sisi kupata matunda ya gesi kabla yao badala ya kuongea sana bila vitendo.
Mambo ya maana sana haya..
Lakini kwa utawala wa ccm sahau hayo kabisaaa!
 
Usionyeshe kama una matatizo ya akili kijana..lini mikataba iliwahi kuwekwa hapa ukasoma? Unashindwa kutafsiri maana ya badiliko la muundo wa umiliki kutoka Barrick kwenda Twiga una gani..sawa, faida moja, kugawana mapato kwa asilimia zilizokubaliwa ikiwemo ile 16% ya lazima ya umiliki wa rasilimali zote chini ya ardhi..sambamba na mrahaba na kodi zote, pili kushiriki kwenye maamuzi yanayohusu uendeshaji mgodi..kufahamu mikopo kama ipo na riba zake..faida au hasara, kiwango cha gharama za uendeshaji mgodi nk, yote hayo hayakuwepo kabla. Narudia tena mikataba si misahafu inaweza kubadilishwa..labda km unataka kuleta ubishani wa simba na yanga ambao unaweza amua kuwa mjinga hata kama ukweli unaujua.

Nasema hivi, unachokiongea hapa ni ulichoambiwa na hao waongo, huna uhakika wa nini hasa wanalosema, labda kama umeamua kukabidhi akili yako kwa watu waongo. Sasa hilo sio kosa langu ni lako.
 
Kama una uwezo hata kidogo kufahamu potential ya uwepo wa viwanda Kenya kwa uchumi KIKANDA na matokeo ya ukuaji wa uchumi kutokana na matumizi ya gesi viwandani..hizo usd 1.1 billion kupeleka bomba la gesi Kenya hata benki za ndani Kenya ukiacha AfDB zinaweza kutoa kwa sababu deni litalipwa hata kabla ya miaka 5..

Leo ni 2022. Tuombe Mungu atupe uzima ndani ya miaka mitano kama utaona lolote litakalofanyika kuhusiana na hilo bomba la gas. Nitauvuta uzi huu kama tutakuwa hai ili uniprove wrong.
 
Nasema hivi, unachokiongea hapa ni ulichoambiwa na hao waongo, huna uhakika wa nini hasa wanalosema, labda kama umeamua kukabidhi akili yako kwa watu waongo. Sasa hilo sio kosa langu ni lako.
Huu ndio ubishi wa simba na yanga unauleta hapa..mabadiliko haya Barrick wenyewe waliandika kuwaeleza shareholders wao, wewe ndio bado una ujinga kutegemea taarifa za upande mmoja ambao hata huuamini.
 
Hakuna gas inapelekwa Kenya boss, zile ni porojo za kisiasa za miaka yote. Kuna makubaliano ya kuanzisha sarafu ya pamoja ya east Afrika, toka enzi Mwai Kibaki na Mkapa wakiwa maraisi, lakini hakuna lolote limetekelezwa hadi sasa! Kupeleka Gas Kenya haitapungua $2t, nani ana hizo pesa sasa hivi wakati hata gas yenyewe mikataba yake haieleweki?

Zile zilikuwa ni porojo za kufurahisha genge ili viongozi wapige imprest vizuri. Inshort ogopa story za viongozi matapeli.
Binafsi naombea ibaki kuwa porojo hivyo hivyo
 
Huu ndio ubishi wa simba na yanga unauleta hapa..mabadiliko haya Barrick wenyewe waliandika kuwaeleza shareholders wao, wewe ndio bado una ujinga kutegemea taarifa za upande mmoja ambao hata huuamini.

Nimecheka kwa nguvu.
 
Kwa hiyo usipowauzia Kenya hiyo gesi ndio utakuwa umefaidikaje?

Si hata hizo bidhaa utazikosa au kuagiza nchi ya mbali kwa bei ghali zaidi?
Na je Watanzania wamepigwa marufuku kutumia hiyo gesi?

Una mentality ya kichawi sana, yaani kwa kuwa wewe umeshindwA kutumia maji kulima unakataa kumuuzia jirani yako ili wote mfe njaa??
Hao watanzania wataenda kujipimia gesi wenyewe,ndio maana mnaambiwa serikali ijenge miundo mbinu ya watanzania kuipata hiyo gesi itakapojitosheleza ndio uende kokote mnapotaka
 
Wewe ulikatazwa kuwasabotage? Una uwezo mdogo Sana wa akili huku ulijifanya unazo 😁😁..

Kwa hiyo ulivyokaa na gas yako ndio umeshawazidi hao Kenya au?

Hata ungekuwa na kila kitu kwa akili zako Za kindezi hizo hakuna kitu utafanya..

Eti Kenya ndio mshindani wako,kwani Uganda sio mshindani? Zambia sio mshindani?

Gas unayo peke yako? Toa akili za mgando wa matongotongo haziwezi kukutoa hapo ulipo..uza mali Jenga uwezo.
Sasa uwezo wako kufikiri na hao wenzako ndio umefikia hapo na hasa kwa kujali matumbo yenu pasipo kufikiria vizazi vijavyo,gesi hapa kwetu imejitosheleza hadi iende nje?si kwa matumizi wa umeme,viwandani na hata majumbani hapa kwetu bado ovyo,halafu unauliza kama naweza kuwasabotage wakenya,nitawezaje while ndugu zako walio kwenye madaraka wasio wazalendo kama wewe ndio wanaoshirikiana na wakenya kuua biashara za TZ kwa maslahi yao
 
Tungeenza kujua tulie nae ana elimu ya uchumi au ABC za uchumi au degree ya ustawi wa jamii kufanya COUNSELING.

RUTO ni mfanyabiashara wa kwetu MBOBEZI wa nini?
 
Sasa wewe umekatazwa kufanya hayo? Ni serikali ya Kenya ndio itazalisha hizo bidhaa?

Wewe umejenga kiwanda ukangimwa gas?

Ujinga na hofu za kipuuzi kama.hizi ndizo zinafanya hii Nchi iwe Mkiani kwenye Kila kitu licha ya kuwa na kila rasilimali..

Changamana na wenye uwezo Ili unifunze kwao vinginevyo ukijifungia utaishia kurithisha ujinga Kwa vizazi na vizazi..In fact tunatakiwa kufuta viza hapa EAC Ili tuweze kujifunza kwa wenzetu kuwa aggressive kwenye biashara nk badala.ya ulalamishi na mentality za kutegemea serikali.
Umeongea upuuzi, yaani wewe kama una mke asiyejua kutandika kitanda utamwambia aende akachangamane na wanawake wanaojua kutandika vitanda vyao huko majumbani kwao ili ajifunze kutandika kitanda chako kama wao.
 
Tuna miradi ya bwawa la umeme $3.5, na SGR ya $7.5t na hakuna uliofika hata nusu. Kenya hapo ananuka mzigo wa madeni, ni wapi tutapata $2+ kujenga bomba la gas boss? Hebu nitajie wapi tutapata hizo pesa za kujenga bomba, sisi au Kenya, au wote kwa pamoja?
Mkuu viwanda vingi vya Kenya ni mali ya wawekezaji kutoka Uingereza na Marekani, hivyo kupata pesa ya kupeleka gesi Kenya ni dakika sifuri TU.
 
Hao watanzania wataenda kujipimia gesi wenyewe,ndio maana mnaambiwa serikali ijenge miundo mbinu ya watanzania kuipata hiyo gesi itakapojitosheleza ndio uende kokote mnapotaka
Wametaka kununua wakanyimwa? Dangote si ana kiwanda chake na anauziwa gesi?
 
Kinacho tusumbua waTanzania wengi ni ujuaji tunapenda saana kudeal na vitu vilivyo nje ya uwezo wetu wa kifikira

Dunian nchi zote zinazozalisha nishati huuza nje ya nchi kwaajir ya kujipatia fedha za kigeni na mapato kiujumla sasa kuna shida gani Tanzania kuiuzia gesi kenya? Au kuna nchi gani dunian inayozalisha gesi kisha ikawa haifanyi exportation ya hyo gesi?

Swala la kenya kunufaika na gesi kuliko Tanzania pale itakapofika kenya hiki ni zaid ya kichekesho ni sawa na kusema Tanzania tunanufaika na mafuta kuliko muuzaji wetu Saudi Arabia,Unahitaj akili ndogo tu kuelewa kuwa muuzaji wa gesi ndio anaeamua bei ya kuuza na katu hawez kuuza bei sawa na ya ndani ya nchi hivo ni swala lililowaz kuwa bei ya gesi kenya itakuwa kubwa kuliko tz hivo kenya haiwez kuwa na advantage kwenye gharama za uzalishaji.

Kenya kutuuzia gesi ya kupikia kutokana na gesi yetu huu pia ni utoto sababu iko waz gesi inayoenda kuuzwa kenya ni gesi ya kawaida ambayo haijasindikwa hivo haiwez kutumika kwa matumiz ya kupikia bali kuendeshea mitambo na labda kuzalishia umeme pili unasahau kuwa plant kubwa ya kusindika gesi ambayo ndo hutumika kwa kupikia inajengwa Tanzania Lindi na kenya hakuna project kama hyo wala hawez kuwa nayo sababu initial cost yake ni kubwa saana na huwez kujenga hyo plant kama wewe sio gas producer na hata wakiforce kuijenga gesi yao itakuwa expensive kuliko yetu na hivo haitoweza kuuzika sokon hii ni sawa na kulangua ndizi bukoba Dsm afu ukaziuze tena Kagera.

Watanzania tuache uoga usiokuwa na sababu zozote za msingi kenya na Tanzania ndio superpowers wa East Africa hakuna namna yenye tunaweza kukwepana katika kufanya biashara pamoja, uchumi wa kenya ni advantage kubwa kwa uchumi wa Tanzania ni lazma tufaidike na soko la kenya kama ambavyo wao wananufaika na soko la Tanzania moja ya bidhaa ambayo ni game changer kwetu ni gesi na nilazma tuiuze kenya hatuna haja ya kuhangaika na masoko ya mbali wakati tunayo masoko ya jiran.
 
Kakaeni vizuri na msoga atawambia aliemkabidhi gas
Ndo ajue kwann Ruto alifanya kikao na Mzee wa Mgaso ndo wakatoa statement Abt gas.

Nchi inahitaji Overhaul kama tunataka Kutoka hapa tulipo.

Tuiue kabisa CCM na Serikali na Katiba iliyopo tuanze UPYA.

Ameeen.
 
Tangu lini mna gas? Hiyo ina wenyewe
 
Back
Top Bottom