Kabla ya maisha kuwapiga Watu wengi Knockout, wengi walifikiri wakifika miaka 30 wangekuwa na nyumba na Gari


Sio kwamba sikuelewi, nakuelewa sana lakini tusichokubaliana ni kuonesha kuwa kila result, mtu ndio anaamua iweje

By the way wewe si unajua marketing vizuri tu, unapofanya marketing plans na kufanya analysis, je, huwa huangalii other factors beyond your products and customers dynamics ili uweze kubashiri peformance yake ?...

Kama upo a hundred percent sure, kwa nini usiangalie product yako na mteja wako then ukaipush sokoni?...

Okey ngoja nikuulize, Leo hii umeme unasumbua, kuna mtu aliweka kuku na nyama kwenye friji vikamuharibikia na mtaji ukakata. , je, huyu unamuweka katika category gani ?.. Kwamba kashindwa kutengeneza results

Nakuelewa sana sana maana na mimi ni mtu ambaye huwa nachukua full responsibility of my failures regardless of the reasons behind.. Na pia sitaki nikubasilishe msimamo wako maana ni Mzuri sana sanaa lakini kwenye uhalisia, kesho inatabirika ila hakuna mwenye control nayo, sote tunaitengenezea mazingira iwe vile tunavyotaraji ila si mara zote huwa tunavyotaka..

Hizo efforts ulizotaja ndio kutengeneza mazingira ili results zije vile tunavyotaraji kama nilivyosema. Ila hatuna control over them
 
Kachapika kweli kweli now.
Nawaza nimkumbushe ile story tukiwa dom nahisi tamuumiza.
Anaendesha bodaboda kazi ambayo hata mtu asiyejua maana ya neno PEOPLE anaweza kuifanya
Huyo jamaa yako hana uthubutu ni watu ambao wanataka mafanikio yawafuate

Ni kweli Mungu anapanga future yetu ila bila kuwa na uthubutu utakshia kumlaumu Mungu ndo maana iman lazima iendane na matendo ambayo ni ujasiri na uthubutu

Una-degree unaendesha bodaboda fahamu kuna kitu mtu umekosa cha kwanza ni ujasiri na kutokujua thamani yake

Wako wanafanikiwa kwa kupata connection out of nowhere, wako wanaofanikiwa kwa bahati na wako wanaofanikiwa kwa ujasiri na uthubutu
Ndo mwingine unatakiwa uwe jasiri ili urithi Baraka za Mungu tofauti na hapo utaishia kumlaumu Mungu kila siku maisha yetu hayafanani
 
Mkuu kuna kipindi hicho kwenye maisha, kila unachogusa kinaenda hadi unajihisi last born wa Mungu halafu kuna hicho kipindi. Unaweza hisi dunia imekutenga

Na unakuta Cv na uwezo ni ule ule na nafasi unazopambania ni zile zile.. Ipo hivyo
 
Si sahihi kusema hivyo kwa sababu hata wawekezaji wanakopa na mitaji inakufa. Mungu mwenyewe huwapa watu wake. Pia tukiwa wawekezaji wote nani atanunua kwa mwingine?
 
Kuna vitabu vingi vinavyofundisha "how to be rich" ila ukianza kusoma Biblia itakufundisha zaidi kuliko hivyo vitabu vingine
Mfalme suleiman kwenye biblia anatufundisha kuwa "mshike sana elimu usimuache aende zake

Ni point kubwa sana kila jambo unalolifanya linahitaji upate elimu ili ufanikiwe bila maarifa hauwezi kupata chochote hata uwe mlokole vipi

Pia tunamuhitaji msaada wa roho mtakatifu ili uweze kutufanyi a miujiza katika shughuli zetu uwezi kupata mafanikio bila elimu ukihitaji msaada wa roho mtakatifu

Soma yohana 14 :16
16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote. 17 Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini hawawezi kumpokea.

Soma yohana 15:5
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote.

Nahitimisha kwa kusema mafanikio sio bahati wenzetu ngozi nyeupe ili walishafahamu muda mrefu kabla hajaanzisha jambo tayari elimu sisi waafrika tumejikita kwenye upambanaji kutaka kupata pesa kwa kitu usichokijua kwa mapana yake




Siyo sahihi kuaminisha watu kwamba wanaofanikiwa ni wale wa Mungu tu

Wakati na bahati huwapata wote

Na kuna maelfu ya walokole ni Masikini wa kutupwa

Kufanikiwa ni jitihada na bahati
 
Mkuu kuna kipindi hicho kwenye maisha, kila unachogusa kinaenda hadi unajihisi last born wa Mungu halafu kuna hicho kipindi. Unaweza hisi dunia imekutenga

Na unakuta Cv na uwezo ni ule ule na nafasi unazopambania ni zile zile.. Ipo hivyo
Yeah nikweli mkuu, kuna muda Mungu tu anaamua kusimama upande wamtu, nahio ndio tunaita bahati tu.
 
Mafanikio madogo madogo yanahitaji jitihada, elimu sahihi na fursa sahihi

Lakini yale mafanikio makubwa makubwa YANAHITAJI BAHATI
 

Msaada wake kwako hautegemei unamuomba au humwombi. Unamtambua au haumtambui.
Ukishatimiza alichokuletea imeisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…