Kabla ya vita USD 1 ilikuwa sawa na Rubles 77, sasa hivi ni sawa na Rubles 55. Tunajifunza nini kutokana na hali hii kama Taifa huru?

Ni aibu na fedhea kwa nchi zetu za kiafrica. Tuna rasilimali za kutosha ila tunategemea vitu ving kutoka kwa watu wanao beba rasilimali zetu.

Sisi africa tumekali u dini tu. Kucha kutwa ni kuangaika na dini zilizoletwa na wao wenyewe.

Tanzania tuna chuma ya kutosha huko liganga ila mpka leo hatujaanza kuvuna na chuma imegundulika toka karne ya 17. Sasa inawezekanaje sisi mpka leo tushindwe kuchimba chuma kama walivyochimba karne ya 17
Soma hii article kama una uwezo wa kuelewa na itakufungua macho.
 
Tarehe 1 January 2022 dola moja ya Marikani (USD) ilikuwa sawa na Rubles 77 za Russia. Baada ya vita kati ya Russia na Ukraine mwezi Februari 2022, Russia iliwekewa vikwazo (sanctions) lukuki za kiuchumi na dunia inayoongozwa na Amerika na nchi za Ulaya. Lakini leo nchi hizi zilizoweka vikwazo zinalia kwa njaa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kutokea tangu dunia hii iumbwe. Nchi hizi sasa zinabadili USD 1 kwa Rubles 55 ili kupata chakula na nishati kutoka Russia. Mara nyingi zinalazimika kupata vitu hivi kupitia kwa nchi janja za China na India.

Hii ndiyo maana ya nchi kumiliki rasilimali asili zake. Nchi zetu nyingi zimeshindwa kufanya hivyo. Utakuta nchi kama Nigeria yenye rasilimali kubwa ya mafuta ya petroleum, mafuta yake yote huenda ughaibuni na yenyewe kulazimika kuagiza mafuta yake kutoka Uarabuni kama sisi. Gesi ya LNG inayovunwa Mozambique yote huenda ughaibuni na wao kuambulia kiduchu. Yote haya yanatokea kwa sababu nchi hizi siyo wamiliki wa rasilimali hizi kufuatana na mikataba waliyowekeana na hizo nchi tajiri za ughaibuni.

Sisi mambo yakoje? Jee huo mkataba wa mradi mkubwa wa LNG unasemaje? Jee tumejipangaje kulisha dunia kwani tuna ardhi tele na mito tele ya umwagiliaji? Ardhi yenye rutuba na malighafi tele ya kutengeneza mbolea.
Imebidi nikaangalie, nimekuta kweli.

Dunia inamuinamia Russia.
 
Nimejifunza kuwa tuwapinge mashoga wote wakiongozwa na USA tukifanya hivyo thamani yao itashuka na yetu itaongezeka
 
Hiyo sasa ni speculation. Proven natural gas reserves zetu ni nothing ukilinganisha na za Russia na Ukraine.

Hatufanya utafiti wa kutosha kwa sababu ya kukosa uwezo. Miaka yote kuanzia 1970 utafiti umejikita Songosongo na maeneo ya karibu na Songosongo huko Lindi na Mtwara. Hivi karibuni utafiti mdogo huko Zanzibar ulionesha gesi hiyo inayoanzia Mtwara na Mozambique inafika hadi visiwa vya Zanzibar na Pemba. Bila shaka hadi bahari ya Tanga.

Hivi majuzi rais wetu amesema anakusudia kuliongezea uwezo shirika letu la TPDC ili longer kasi ya tafiti hizi ambazo gharama zake ni za gharama kubwa sana.
 
Tarehe 1 January 2022 dola moja ya Marikani (USD) ilikuwa sawa na Rubles 77 za Russia. Baada ya vita kati ya Russia na Ukraine mwezi Februari 2022, Russia iliwekewa vikwazo (sanctions) lukuki za kiuchumi na dunia inayoongozwa na Amerika na nchi za Ulaya. Lakini leo nchi hizi zilizoweka vikwazo zinalia kwa njaa na mfumuko mkubwa wa bei ambao haujawahi kutokea tangu dunia hii iumbwe. Nchi hizi sasa zinabadili USD 1 kwa Rubles 55 ili kupata chakula na nishati kutoka Russia. Mara nyingi zinalazimika kupata vitu hivi kupitia kwa nchi janja za China na India.

Hii ndiyo maana ya nchi kumiliki rasilimali asili zake. Nchi zetu nyingi zimeshindwa kufanya hivyo. Utakuta nchi kama Nigeria yenye rasilimali kubwa ya mafuta ya petroleum, mafuta yake yote huenda ughaibuni na yenyewe kulazimika kuagiza mafuta yake kutoka Uarabuni kama sisi. Gesi ya LNG inayovunwa Mozambique yote huenda ughaibuni na wao kuambulia kiduchu. Yote haya yanatokea kwa sababu nchi hizi siyo wamiliki wa rasilimali hizi kufuatana na mikataba waliyowekeana na hizo nchi tajiri za ughaibuni.

Sisi mambo yakoje? Jee huo mkataba wa mradi mkubwa wa LNG unasemaje? Jee tumejipangaje kulisha dunia kwani tuna ardhi tele na mito tele ya umwagiliaji? Ardhi yenye rutuba na malighafi tele ya kutengeneza mbolea.
Viongozi wa Africa 95% wamelaaniwa na Mungu
 
Hatufanya utafiti wa kutosha kwa sababu ya kukosa uwezo. Miaka yote kuanzia 1970 utafiti umejikita Songosongo na maeneo ya karibu na Songosongo huko Lindi na Mtwara. Hivi karibuni utafiti mdogo huko Zanzibar ulionesha gesi hiyo inayoanzia Mtwara na Mozambique inafika hadi visiwa vya Zanzibar na Pemba. Bila shaka hadi bahari ya Tanga.

Hivi majuzi rais wetu amesema anakusudia kuliongezea uwezo shirika letu la TPDC ili longer kasi ya tafiti hizi ambazo gharama zake ni za gharama kubwa sana.
Tafiti za kupiga pesa tupu
 
America wamebugi sana kwenye hii vita, wangekuwa na akili wala wasingetaka kui-prolong iendelee kupiganwa kwa muda mrefu kwa kuendelea kuwapa silaha Ukraine.

Walitegemea kuidhoofisha Russia, lakini mambo yamekuwa kinyume, ruble inazidi kupanda thamani na uchumi wa Russia kuimarika, mfumko wa bei kwenye nchi magharibi ni wa kutisha, yaani kila kitu kimeparaganyika kwa sasa. Kwa jinsi wamarekani walivyo wabinafsi watataka hali iendelee hivyo tu kwa sababu ya interests zao.
Hii mentality mbaya sana, kwahiyo Ukraine ivamiwe tu watu wake kimya kisa kuokoa uchumi wao binafsi?? Kwa akili kama hizi unadhani Mandela angepigania uhuru wa watu weusi South Africa maana kwa wakati ule uchumi wa Sauzi ulikua juu sana kuliko wa sasa and in fact waafrika Wana maisha magumu sasa kuliko hata kipindi wanabaguliwa tofauti ni uhuru tu ila umaskini umezidi.

So kwa ushauri wako huu Mandela angeacha kupigania uhuru sababu tu uchumi ulikua mzuri Sauzi sio??
 
Tembo Tena kuwanyofo pembe zao hpn utapigwa Vita na dunia nnzima
Mbona huyo OBC huko Loliondo anafanya trophy hunting? Mbona uchumi wa Rwanda unategemea sana mauzo ya trophy wanazozipata kutoka kwetu kwa kificho? Shida ni kuua tembo, kunyofoa trophy zao kitalaam under anesthesia by qualified wildlife veteran doctors.
 
Hata sisi tukitaka leo tunaweza kuipandisha shilingi kwa dola. Ila kwa kufanya hivyo tutaumiza mno wananchi wetu. Tukiweka interest rate asilimia 30 pesa zote zitarudi benki na mahitaji ya kununua pesa za nje yatapungua mno maana tuitakuwa hatuagizi chochote toka nje.

Uzalishaji utashuka na unemployment itaongezeka.

Uchumi sio rahisi hivyo kama mnavyoona eti kisa rubble imepanda. Rubble imepanda kwasababu Putin kachukua hatua kali kali, Kuuza rubble sasa unakatwa tozo asilimia 30.

Hivi leo Tanzania waseme kuuza shilingi pesa za nje unakatwa tozo asilimia 30, kuna mtu atauza tena shilingi?

Interest rate isn’t a controlling factor. Interest rate ya Tanzania haijawahi kuwa chini in recent history, yet kuporomoka kwa thamani ya shilling hakujawahi kukoma!
 
Hatufanya utafiti wa kutosha kwa sababu ya kukosa uwezo. Miaka yote kuanzia 1970 utafiti umejikita Songosongo na maeneo ya karibu na Songosongo huko Lindi na Mtwara. Hivi karibuni utafiti mdogo huko Zanzibar ulionesha gesi hiyo inayoanzia Mtwara na Mozambique inafika hadi visiwa vya Zanzibar na Pemba. Bila shaka hadi bahari ya Tanga.

Hivi majuzi rais wetu amesema anakusudia kuliongezea uwezo shirika letu la TPDC ili longer kasi ya tafiti hizi ambazo gharama zake ni za gharama kubwa sana.

Sawa, lakini hii sio justification ya madai kwamba Tanzania ina natural gas nyingi kuliko Russia and Ukraine, combined!
 
Uchumi gani urusi umeimarika? Wakati mamilionea na matajiri na wafanyabiashara maelfu na maelfu wanatoroka kila siku kwasababu hali mbaya ya kiuchumi. Acheni ushabiki hali ya maisha urusi sasa hivi ni mvaya ba inazidi kuwa mbaya.
 
Interest rate isn’t a controlling factor. Interest rate ya Tanzania haijawahi kuwa chini in recent history, yet kuporomoka kwa thamani ya shilling hakujawahi kukoma!
Leo hii BOT ipandishe interest kwa asilimia 10 utaona kama shilingi haitapanda. Ila sasa maumivu kwa raia itakuwa balaa. Hiyo mikopo mtu analipa laki mbili kwa mwezi, atatakiwa kulipa laki nne.

Interest rate ni factor mojawapo ya ku control thamani ya pesa. Ukishusha interest thamani ya pesa inapungua kwasababu pesa nyingi zinakuwa mitaani. Ukipandisha interest pesa nyingi zinarudi bank na hivyo thamni yake inapanda.

Of course kuna factors zingine pia.
 
Back
Top Bottom