Freddie Matuja
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,479
- 2,877
Waingereza wanasema "they all serve her pleasure".Katika hotuba yake Rais SSH alisema atafanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kumteuwa na kutengeneza safu ya watu wanaoweza kufanya naye kazi. Kwasababu wengine wanamkwamisha.
Baraza jipya limetangazwa na Mawaziri walioachwa ni wanne. Kwahiyo tafsiri yake ni kwamba hawa wanna ndiyo walikuwa sumu ktk serikali yake, yaani Kabudi, Lukuvi, Kitila na Mwambe.
Na ukiangalia kinachoitwa mabadiliko si mabadiliko bali ni uhamisho wa watu walewale kuzurura kutoka wizara moja kwenda nyingine.
Nimesoma haya kutokana na kauli ya MH. SAMIA kwamba kuna mawaziri hawako naye, pengine wanawaza uchaguzi 2025.
Nini maoni yako!
Na kwa katiba yetu Rais halazimiki kufuata ushauri wa yoyote anapoamua kufanya maamuzi.
Uteuzi ni bahati, kudra za mwenyezi Mungu, na mwenye mamlaka ya kuteua at any point akiamua kumwondoa yeyote anamwondoa.
Labda, pia walikuwa na maandalizi ya 2025, hii itabaki labda; je ni wote walikuwa na maandalizi? Muda ukifika (2025) tutajua kama kweli walikuwa wanajiandaa au "walisingiziwa"
Niweke record, sio kila kitu Rais au mkuu wa nchi anacholetewa mezani ni cha kweli. Huenda kuna vingine wanachomekewa.
Ukisoma biblia kulikiwa na serikali, na kuna wakati mfalme Dario aliwahi kuchomekewa kupitisha sheria bila kujua ilikuwa umelenga Daniel ambae alikuwa "Jambe la ukweli" kwa mfalme.
Yusuf aliwahi kusingiziwa na mke wa mkuu wa walinzi Farao, kuwa Yusuf alikuwa na nia ya kumbaka, na akatiwa lupango.
Kiufupi, Rais anapata taarifa nyingi sana na toka watu wengi sana, kama wakubwa wa zamani waliwahi kuchomekewa, bila shaka hata zama hizi mkulu anaweza kuzugwa na akafanya maamuzi then baadae akaja kujua kumbe alikuwa mislead.
Mungu ibariki Tanzania, hongereni wateule, bila shaka mtamsaidia madam SSH kuwatumikia Watanzania.