Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Majina kweli yanafanana. tujaribu kuchimba zaidi. huku tukijikumbusha na kupata dondoo zaidi.

 
Mkuu hili Kanisa Katoliki linafundisha uwongo sana. Hakuna ushahidi wowote hata wa kihistoria tu unao onesha kuwa Mtume Petro aliwahi kuishi Roma. Hakika kabisa Kanisa hili ni adui namba moja wa UKRISTO duniani.
Duuuh!!
Hapa Imani, chuki na Upinzani.
Aluta continua [emoji91]
 
Hawawezi kukuelewa
 
Hujajibu hoja yangu. Sanasana unaleta ubishi wenye chuki ndani yake. Kanisa katoliki ni mama wa madhehebu yote ya kikristo unayoyafahamu wewe, pamoja na ufahamu wako finyu sana wa masuala ya dini
 
Wewe unaonekana ni msabato bila ubishi.Kama unamwamini Petro nadhani alikozikwa sio jambo la msingi sana.Ni kama Krismasi wasabato hawaadhimishi hii sherehe.Ila wanakubali Yesu alizaliwa japo hawana tarehe yao ya kuzaliwa.
Kuwa msabato siyo dhambi ndugu yangu, kuishika SABATO siyo dhambi. Dhambi ni kuzivunja amri za MUNGU, na katika amri kumi za MUNGU moja wapo ni kuishika SABATO, soma KUTOKA 20:8-11.

BWANA YESU alisema sikuja kuitangua Torati bali kuitimiliza, soma MATHAYO 5:17-19, utaona BWANA YESU, anasisitiza kuwa "mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi....... "

BWANA YESU hakuifuta Sabato bali aliitimiliza Sabato pale aliposema; "Je!, ni halali siku ya sabato kutenda mema au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza"? LUKA 6:9. Hapa tunaona alichokisema BWANA YESU ni kwamba siku ya sabato ni siku ya kutenda "mema", hivyo sabato inabakia kama ilivyo isipokuwa inakuwa ni siku ya kutenda mema badala ya kukaa tu na kupumzika. Siku hii ya sabato unaweza ukaitumia kwenda hospitali kuwapa pole wagonjwa, au kwenda kuwasaidia watoto yatima, au kwenda magereza kuwatembelea wafungwa au kutenda mema yoyote yale kuliko kukaa na kufanya mambo yako mwenyewe kwa faida yako binafsi. Soma ISAYA 58:13 "Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza kwa kutokufanya njia zako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo".

Soma; LUKA 4:16, WAEBRANIA 4:9, MATENDO 17:2, EZEKIELI 20:20, ISAYA 56:4-7, UFUNUO 14:12

Biblia imesisitiza sana katika kuitunza siku ya sabato na BWANA YESU alifafanua zaidi nini kifanyike siku ya sabato. Kuna watu huwa wanakejeli kwa kusema "utashikaje sabato kwani wewe ni Myahudi?".

Watu hawa wamesahau au hawaijui ahadi ya BWANA MUNGU kwa watu ambao siyo Wayahudi wanaoishika sabato. Imeandikwa hivi; "Na wageni walioandamana na BWANA ili wamhudumu na kulipenda jina la BWANA kuwa watumishi wake kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu, nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu ya zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote". ISAYA 56:4-7
 
Hivyo vitabu viliandikwa kwa nia ya kupotosha UKWELI. Ndiyo maana viliposomwa havikukubaliwa kujumuishwa kwenye Biblia. Biblia haikujumuishwa na mtu mmoja tu, walikaa watu tofauti wakakubaliana kipi kiwemo na kipi kisiwemo ndani ya Biblia.
 
Mimi adui yangu siyo "Wakatoliki", adui yangu ni "Ibilisi" anayelitumia kanisa Katoliki kufundisha UWONGO? Mimi napingana na uwongo unaofundishwa na Kanisa Katoliki lakini sipingani na waumini wa Kikatoliki. Lengo letu sisi ni waumini hawa wanaodanganywa wafunguke macho na waione KWELI.

Naomba nikuulize swali, hivi Kanisa Katoliki linapowafundisha waumini wake kusali na kumwomba Mama Mariamu badala ya kusali na kumwomba MUNGU; hiyo wewe unaona ni sawa kweli?

YESU KRISTO alifundisha nini kuhusu kusali na alisema tukisali tumwombe nani??

Musa alikuwa mtu pekee ambaye aliongea na MUNGU uso kwa uso ingawa hakumwona MUNGU lakini aliisikia sauti yake mubashara kabisa, tena alikaa mlimani akiwa anaongea na MUNGU kwa siku arobaini, lakini haijawahi kutokea wana wa Israeli wakasali na kumwomba Musa awaombee kwa MUNGU. Sasa inakuwaje leo hii Kanisa Katoliki linawafundisha waumini wake kuwaomba "wafu" wawaombee kwa MUNGU kwa kisingizio kuwa hao wafu ni watakatifu, Je! ni kweli hao wafu ni watakatifu?? Hata kama hao wafu ni watakatifu, Je! ni nani ambaye anajukumu la kuwaombea wanadamu kwa MUNGU? Siyo YESU KRISTO PEKEE??

Wewe huoni kama uwongo huu wa Kanisa Katoliki unawafanya waumini wa kanisa hili kumkosea BABA MUNGU na BWANA YESU kwa kwenda kinyume na mafundisho yake? Wewe huoni kama kanisa katoliki linawaabudu sana wafu linaowaita watakatifu, linamwabudu sana Mama Maria, linaabudu sana sanamu na kuacha kumwabudu MUNGU BABA??

Tukiwa kama WAKRISTO tukiona ndugu zetu wanapotea, Je! hatuna haki na wajibu wa kuwasahihisha? Je! NENO la MUNGU linasema nini katika kukemea maovu?

Hayo yote wewe unaona ni sawa tu yaendelee kufanyika wakati NENO la MUNGU limeyakataza kabisa, au unataka nikuandikie hapa mstari kwa mstari kutoka kwenye Biblia ndiyo uamini? Mimi sitaandika mistari ya kwenye Biblia, ila nakuomba uchukue Biblia yako, ukae chini uisome na utajua kuwa Kanisa Katoliki linafundisha "UPOTOVU" wa kiwango cha juu sana.
 
Hv umesoma ukichoandika Sasa kama hizo barua kanisa katoliki wamezizuia unasemaje tena waongo
Kuzizuia haina maana kwamba hakuna watu waliowahi kuzisoma. Kuna watu wamezisoma na wanazijua vizuri. Zimezuiwa kusambazwa kwenye public.
 
Nitaorodhesha hapa hapa JF "uwongo" wote wa kanisa katoliki kwa faida yako mkuu ili uijue KWELI. Kaa mkao wa kula mkuu.
 
Mabaki ya Petro yamepatikana Jerusalemu, hii ina maana kuwa alifia Jerusalem. Hata kama Biblia haisemi ni wapi alipofia lakini Biblia imesema wazi kabisa kuwa Petro hakufika Roma. Hilo halina ubishi.

Paulo aliandika kila kitu alipokuwa Roma, kama Petro alikwenda Roma; iweje Paulo aandike vyote lakini asiandike kabisa habari za Petro akiwa Roma??

Iweje Petro mwenyewe asiandike kabisa waraka kuhusu Roma?? Hivi kweli inakuingia akilini, Mtume kama Petro akae Roma kwa miaka 24 AKIWA PAPA asiandike chochote kile kwa ajili ya vizazi vijavyo??

Hivi ninyi Wakatoliki mnapodanganywa akili zenu huwa hazifikirii kabisa au mmeleweshwa na mvinyo ya yule kahaba aliyenenwa katika UFUNUO 17:1-6
 
Kuzizuia haina maana kwamba hakuna watu waliowahi kuzisoma. Kuna watu wamezisoma na wanazijua vizuri. Zimezuiwa kusambazwa kwenye public.
Nani amezisoma wewe Ellen g white au [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hizo story unazoleta ni za club za gongo na chimpumu
 
ta
Wewe unaonekana ni msabato bila ubishi.Kama unamwamini Petro nadhani alikozikwa sio jambo la msingi sana.Ni kama Krismasi wasabato hawaadhimishi hii sherehe.Ila wanakubali Yesu alizaliwa japo hawana tarehe yao ya kuzaliwa.
Hahaha, tarehe alisahau Mama E. G. White kuwaambia.
 
Musa na Eliya ambao Petro aliwaona wakiwa na Bwana Yesu kule mlimani ni Musa yupi?

Ule muujiza wa harusi ya kana watu wale walipitisha maombi yao kwa nani kabla ya Bwana Yesu kuufanya ule muujiza?




 
Musa na Eliya ambao Petro aliwaona wakiwa na Bwana Yesu kule mlimani ni Musa yupi?

Ule muujiza wa harusi ya kana watu wale walipitisha maombi yao kwa nani kabla ya Bwana Yesu kuufanya ule muujiza?
Acha kuniuliza maswali ya kitoto wewe. Tatizo hii JF sasa hivi imejaa vitoto ambavyo haviwezi kusoma na kuelewa hoja zinazozungumziwa.

Sikia dogo chukua Biblia yako na uisome vizuri kisha utapata majibu yote uliyoniuliza. Ukiona kuna mahali kwenye Biblia umeambiwa sali na umwombe Mama Maria, sawa fanya hivyo. Na ukiona kuna mahali Biblia yako inakuambia uwaombe wafu wakuombee, pia ni sawa fanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…