Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Majina kweli yanafanana. tujaribu kuchimba zaidi. huku tukijikumbusha na kupata dondoo zaidi.

Mkuu hili Kanisa Katoliki linafundisha uwongo sana. Hakuna ushahidi wowote hata wa kihistoria tu unao onesha kuwa Mtume Petro aliwahi kuishi Roma. Hakika kabisa Kanisa hili ni adui namba moja wa UKRISTO duniani.
Duuuh!!
Hapa Imani, chuki na Upinzani.
Aluta continua [emoji91]
 
mafundisho ya The Roman Catholic yanatoka katika vyanzo vikuu vitatu. Biblia Takatifu, Roho Mtakatifu na Mapokeo.

kuna vitabu vingi sana kwenye maktaba ya kanisa ambavyo vinamafunzo na taarifa nyingi muhimu ila haviko kwenye mjumuiko wa vitabu vya biblia. vitabu hivi RC wanaviita mapokeo. vitabu hivi havikujumuishwa kwnye biblia kwa sababu mbalimbali. ikiwamo kutoendana na maudhui na mafundisho ya kanisa japo vina taarifa muhimu sana za historia na maisha ya mitume na wakristo w kwanza.

makanisa mengi yalioibuka juzi na kukuta biblia tayari imeshaundwa, hawawezi kuwa na access na baadhi ya taarifa. nao wakabaki kutegemea biblia pekee iliyokusanywa na kanisa katoliki kama chanzo pekee cha mafundisho.
Hawawezi kukuelewa
 
Biblia ni ushahidi tosha kuwa Petro hakufika Roma. Paulo ndiye alikuwa Mtume kwa ajili ya watu wa mataifa na Petro alikuwa Mtume kwa ajili ya Wayahudi(waliotahiriwa). Soma Biblia yako vizuri utaelewa. Tukichukua ushahidi wa Biblia na kujumlisha na ushahidi wa mifupa iliyopatikana Jerusalem, tunajihakikishia kabisa kuwa Petro hakuwahi kabisa kufika Roma.

Kanisa Katoliki limedanganya na linaendelea kuwadanganya ninyi msiotumia akili zenu katika kulisoma NENO la MUNGU.
Hujajibu hoja yangu. Sanasana unaleta ubishi wenye chuki ndani yake. Kanisa katoliki ni mama wa madhehebu yote ya kikristo unayoyafahamu wewe, pamoja na ufahamu wako finyu sana wa masuala ya dini
 
Wewe unaonekana ni msabato bila ubishi.Kama unamwamini Petro nadhani alikozikwa sio jambo la msingi sana.Ni kama Krismasi wasabato hawaadhimishi hii sherehe.Ila wanakubali Yesu alizaliwa japo hawana tarehe yao ya kuzaliwa.
Kuwa msabato siyo dhambi ndugu yangu, kuishika SABATO siyo dhambi. Dhambi ni kuzivunja amri za MUNGU, na katika amri kumi za MUNGU moja wapo ni kuishika SABATO, soma KUTOKA 20:8-11.

BWANA YESU alisema sikuja kuitangua Torati bali kuitimiliza, soma MATHAYO 5:17-19, utaona BWANA YESU, anasisitiza kuwa "mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi....... "

BWANA YESU hakuifuta Sabato bali aliitimiliza Sabato pale aliposema; "Je!, ni halali siku ya sabato kutenda mema au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza"? LUKA 6:9. Hapa tunaona alichokisema BWANA YESU ni kwamba siku ya sabato ni siku ya kutenda "mema", hivyo sabato inabakia kama ilivyo isipokuwa inakuwa ni siku ya kutenda mema badala ya kukaa tu na kupumzika. Siku hii ya sabato unaweza ukaitumia kwenda hospitali kuwapa pole wagonjwa, au kwenda kuwasaidia watoto yatima, au kwenda magereza kuwatembelea wafungwa au kutenda mema yoyote yale kuliko kukaa na kufanya mambo yako mwenyewe kwa faida yako binafsi. Soma ISAYA 58:13 "Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza kwa kutokufanya njia zako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo".

Soma; LUKA 4:16, WAEBRANIA 4:9, MATENDO 17:2, EZEKIELI 20:20, ISAYA 56:4-7, UFUNUO 14:12

Biblia imesisitiza sana katika kuitunza siku ya sabato na BWANA YESU alifafanua zaidi nini kifanyike siku ya sabato. Kuna watu huwa wanakejeli kwa kusema "utashikaje sabato kwani wewe ni Myahudi?".

Watu hawa wamesahau au hawaijui ahadi ya BWANA MUNGU kwa watu ambao siyo Wayahudi wanaoishika sabato. Imeandikwa hivi; "Na wageni walioandamana na BWANA ili wamhudumu na kulipenda jina la BWANA kuwa watumishi wake kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu, nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu ya zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote". ISAYA 56:4-7
 
mafundisho ya The Roman Catholic yanatoka katika vyanzo vikuu vitatu. Biblia Takatifu, Roho Mtakatifu na Mapokeo.

kuna vitabu vingi sana kwenye maktaba ya kanisa ambavyo vinamafunzo na taarifa nyingi muhimu ila haviko kwenye mjumuiko wa vitabu vya biblia. vitabu hivi RC wanaviita mapokeo. vitabu hivi havikujumuishwa kwnye biblia kwa sababu mbalimbali. ikiwamo kutoendana na maudhui na mafundisho ya kanisa japo vina taarifa muhimu sana za historia na maisha ya mitume na wakristo w kwanza.

makanisa mengi yalioibuka juzi na kukuta biblia tayari imeshaundwa, hawawezi kuwa na access na baadhi ya taarifa. nao wakabaki kutegemea biblia pekee iliyokusanywa na kanisa katoliki kama chanzo pekee cha mafundisho.
Hivyo vitabu viliandikwa kwa nia ya kupotosha UKWELI. Ndiyo maana viliposomwa havikukubaliwa kujumuishwa kwenye Biblia. Biblia haikujumuishwa na mtu mmoja tu, walikaa watu tofauti wakakubaliana kipi kiwemo na kipi kisiwemo ndani ya Biblia.
 
Wala hakuna sehemu ya Biblia iliyotaja dini ya ukristo sasa kwanini wewe unajiita mkristo? Vivyo hivyo kwenye Biblia hakuna neno au dhehebu la katoliki, je ukristo ulipatikana vipi? Kumbuka kila mtu aliyekubali mafundisho ya Yesu aliitwa mkristo yaani mfuasi wa mpakwa mafuta lengo ni kurahisisha kujua watu fulani ni waumini wa imani fulani a.k.a dini/ dhehebu, mfano unaposema dini ya kiyahudi tunaelewa inamaanisha nini japo Ktk Bible hakuna dini ya kiyahudi. Vivyo hivyo katoliki limetokana na mtazamo uleule wa ukristo hii inathibitika kwa maana ya neno katoliki lenye maana ya mahali pote pote kwa yeyote yaani ukatoliki ni ukristo usio na mipaka wala ubaguzi kwahiyo ukatoliki haukufanyi wewe usiwe mfuasi wa kristo wala kukutenganisha na kristo. Documents nyingi za kiimani na mafundisho ya mitume yalitunzwa na wakatoliki na vyanzo vya madhehebu yote ya kikristo yalitokana na ukatoliki. Kifupi tu niseme mtu wenye matunda mazuri daima utaendelea kupopolewa na mawe. Wamisionari wa kikatolki ndiyo wameujenga na kuutetea ukristo hivyo ukatoliki unahitaji heshima yake siyo kebehi, inawezekana kuna mapungufu ktk ukatoliki kwakuwa ni wanadamu nasiyo malaika. Yesu alishaweka jiwe moja tu la msingi kila mkristo aweke tofali hapo sasa wengine wanakwenda kujenga sehemu nyingine ambapo Yesu hakuweka jiwe hapo. Binafsi sijawahi ona mafundisho yoyote ya kikatoliki yakipinga waprotestanti wakiwamo wasabato wala kuwakebei kwakuwa wanajua hadui yao mkuu siyo hao
Mimi adui yangu siyo "Wakatoliki", adui yangu ni "Ibilisi" anayelitumia kanisa Katoliki kufundisha UWONGO? Mimi napingana na uwongo unaofundishwa na Kanisa Katoliki lakini sipingani na waumini wa Kikatoliki. Lengo letu sisi ni waumini hawa wanaodanganywa wafunguke macho na waione KWELI.

Naomba nikuulize swali, hivi Kanisa Katoliki linapowafundisha waumini wake kusali na kumwomba Mama Mariamu badala ya kusali na kumwomba MUNGU; hiyo wewe unaona ni sawa kweli?

YESU KRISTO alifundisha nini kuhusu kusali na alisema tukisali tumwombe nani??

Musa alikuwa mtu pekee ambaye aliongea na MUNGU uso kwa uso ingawa hakumwona MUNGU lakini aliisikia sauti yake mubashara kabisa, tena alikaa mlimani akiwa anaongea na MUNGU kwa siku arobaini, lakini haijawahi kutokea wana wa Israeli wakasali na kumwomba Musa awaombee kwa MUNGU. Sasa inakuwaje leo hii Kanisa Katoliki linawafundisha waumini wake kuwaomba "wafu" wawaombee kwa MUNGU kwa kisingizio kuwa hao wafu ni watakatifu, Je! ni kweli hao wafu ni watakatifu?? Hata kama hao wafu ni watakatifu, Je! ni nani ambaye anajukumu la kuwaombea wanadamu kwa MUNGU? Siyo YESU KRISTO PEKEE??

Wewe huoni kama uwongo huu wa Kanisa Katoliki unawafanya waumini wa kanisa hili kumkosea BABA MUNGU na BWANA YESU kwa kwenda kinyume na mafundisho yake? Wewe huoni kama kanisa katoliki linawaabudu sana wafu linaowaita watakatifu, linamwabudu sana Mama Maria, linaabudu sana sanamu na kuacha kumwabudu MUNGU BABA??

Tukiwa kama WAKRISTO tukiona ndugu zetu wanapotea, Je! hatuna haki na wajibu wa kuwasahihisha? Je! NENO la MUNGU linasema nini katika kukemea maovu?

Hayo yote wewe unaona ni sawa tu yaendelee kufanyika wakati NENO la MUNGU limeyakataza kabisa, au unataka nikuandikie hapa mstari kwa mstari kutoka kwenye Biblia ndiyo uamini? Mimi sitaandika mistari ya kwenye Biblia, ila nakuomba uchukue Biblia yako, ukae chini uisome na utajua kuwa Kanisa Katoliki linafundisha "UPOTOVU" wa kiwango cha juu sana.
 
Hv umesoma ukichoandika Sasa kama hizo barua kanisa katoliki wamezizuia unasemaje tena waongo
Kuzizuia haina maana kwamba hakuna watu waliowahi kuzisoma. Kuna watu wamezisoma na wanazijua vizuri. Zimezuiwa kusambazwa kwenye public.
 
We unaongea kimbea sasa usiseme vingi vinatumiwa ujawahi sali catholic ebu tupe kimoja tu kama ukijui basi tafuta la kufanya ndo nyie mnaoamini mchungaji wenu kua mti ya kivuli ni mikosi kwel kazi sana ni vizur kama unasema dini ya mwenzio usiseme kinafki uwezi kudhibitisha unaongea kisa nabii wako amekwambia kaseme ivi ili apate waumini
Nitaorodhesha hapa hapa JF "uwongo" wote wa kanisa katoliki kwa faida yako mkuu ili uijue KWELI. Kaa mkao wa kula mkuu.
 
Wewe ulianza kusema hakwenda na hakufia huko ndo tunakuuliza wewe unaejua ukweli uyuoneshe wapi alifia, tupe mstari kwenye biblia maana unajinasibu kufuata ya biblia tu,sasa tupe andiko linalosema Petro alifia wapi,
Sababu unaamini biblia tu na km biblia haijasema alifia wapi basi hakufa?
Maana unaamini biblia tu na kila kitu kipo kwa biblia,
Mabaki ya Petro yamepatikana Jerusalemu, hii ina maana kuwa alifia Jerusalem. Hata kama Biblia haisemi ni wapi alipofia lakini Biblia imesema wazi kabisa kuwa Petro hakufika Roma. Hilo halina ubishi.

Paulo aliandika kila kitu alipokuwa Roma, kama Petro alikwenda Roma; iweje Paulo aandike vyote lakini asiandike kabisa habari za Petro akiwa Roma??

Iweje Petro mwenyewe asiandike kabisa waraka kuhusu Roma?? Hivi kweli inakuingia akilini, Mtume kama Petro akae Roma kwa miaka 24 AKIWA PAPA asiandike chochote kile kwa ajili ya vizazi vijavyo??

Hivi ninyi Wakatoliki mnapodanganywa akili zenu huwa hazifikirii kabisa au mmeleweshwa na mvinyo ya yule kahaba aliyenenwa katika UFUNUO 17:1-6
 
Kuzizuia haina maana kwamba hakuna watu waliowahi kuzisoma. Kuna watu wamezisoma na wanazijua vizuri. Zimezuiwa kusambazwa kwenye public.
Nani amezisoma wewe Ellen g white au [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hizo story unazoleta ni za club za gongo na chimpumu
 
ta
Wewe unaonekana ni msabato bila ubishi.Kama unamwamini Petro nadhani alikozikwa sio jambo la msingi sana.Ni kama Krismasi wasabato hawaadhimishi hii sherehe.Ila wanakubali Yesu alizaliwa japo hawana tarehe yao ya kuzaliwa.
Hahaha, tarehe alisahau Mama E. G. White kuwaambia.
 
Musa na Eliya ambao Petro aliwaona wakiwa na Bwana Yesu kule mlimani ni Musa yupi?

Ule muujiza wa harusi ya kana watu wale walipitisha maombi yao kwa nani kabla ya Bwana Yesu kuufanya ule muujiza?

Mimi adui yangu siyo "Wakatoliki", adui yangu ni "Ibilisi" anayelitumia kanisa Katoliki kufundisha UWONGO? Mimi napingana na uwongo unaofundishwa na Kanisa Katoliki lakini sipingani na waumini wa Kikatoliki. Lengo letu sisi ni waumini hawa wanaodanganywa wafunguke macho na waione KWELI.

Naomba nikuulize swali, hivi Kanisa Katoliki linapowafundisha waumini wake kusali na kumwomba Mama Mariamu badala ya kusali na kumwomba MUNGU; hiyo wewe unaona ni sawa kweli?

YESU KRISTO alifundisha nini kuhusu kusali na alisema tukisali tumwombe nani??

Musa alikuwa mtu pekee ambaye aliongea na MUNGU uso kwa uso ingawa hakumwona MUNGU lakini aliisikia sauti yake mubashara kabisa, tena alikaa mlimani akiwa anaongea na MUNGU kwa siku arobaini, lakini haijawahi kutokea wana wa Israeli wakasali na kumwomba Musa awaombee kwa MUNGU. Sasa inakuwaje leo hii Kanisa Katoliki linawafundisha waumini wake kuwaomba "wafu" wawaombee kwa MUNGU kwa kisingizio kuwa hao wafu ni watakatifu, Je! ni kweli hao wafu ni watakatifu?? Hata kama hao wafu ni watakatifu, Je! ni nani ambaye anajukumu la kuwaombea wanadamu kwa MUNGU? Siyo YESU KRISTO PEKEE??

Wewe huoni kama uwongo huu wa Kanisa Katoliki unawafanya waumini wa kanisa hili kumkosea BABA MUNGU na BWANA YESU kwa kwenda kinyume na mafundisho yake? Wewe huoni kama kanisa katoliki linawaabudu sana wafu linaowaita watakatifu, linamwabudu sana Mama Maria, linaabudu sana sanamu na kuacha kumwabudu MUNGU BABA??

Tukiwa kama WAKRISTO tukiona ndugu zetu wanapotea, Je! hatuna haki na wajibu wa kuwasahihisha? Je! NENO la MUNGU linasema nini katika kukemea maovu?

Hayo yote wewe unaona ni sawa tu yaendelee kufanyika wakati NENO la MUNGU limeyakataza kabisa, au unataka nikuandikie hapa mstari kwa mstari kutoka kwenye Biblia ndiyo uamini? Mimi sitaandika mistari ya kwenye Biblia, ila nakuomba uchukue Biblia yako, ukae chini uisome na utajua kuwa Kanisa Katoliki linafundisha "UPOTOVU" wa kiwango cha juu sana.
 
Musa na Eliya ambao Petro aliwaona wakiwa na Bwana Yesu kule mlimani ni Musa yupi?

Ule muujiza wa harusi ya kana watu wale walipitisha maombi yao kwa nani kabla ya Bwana Yesu kuufanya ule muujiza?
Acha kuniuliza maswali ya kitoto wewe. Tatizo hii JF sasa hivi imejaa vitoto ambavyo haviwezi kusoma na kuelewa hoja zinazozungumziwa.

Sikia dogo chukua Biblia yako na uisome vizuri kisha utapata majibu yote uliyoniuliza. Ukiona kuna mahali kwenye Biblia umeambiwa sali na umwombe Mama Maria, sawa fanya hivyo. Na ukiona kuna mahali Biblia yako inakuambia uwaombe wafu wakuombee, pia ni sawa fanya hivyo.
 
Back
Top Bottom