Uchaguzi 2020 Kachero Mbobevu Bernard Membe atua nchini, adai ukata umepelekea kusuasua kwa Kampeni za Vyama vya Upinzani nchini

Uchaguzi 2020 Kachero Mbobevu Bernard Membe atua nchini, adai ukata umepelekea kusuasua kwa Kampeni za Vyama vya Upinzani nchini

Hizi kauli za huyu mwamba ni kama anampigia kampeni Magufuli hivi? au
 
Labda Tanzania ya ubeligiji
Jiandaeni kisaikolojia maana Lissu ndiyo rais wako wa awamu ya sita.
photo%20266%2012-18-0.jpg
 
Typical of Membe! Hakuna mpangilio wa maneno. Hakuna maneno yenye mvuto. Hakuna muelekeo wa kiongozi.
Hapo ACT ipate kura ya nani? Anayewapa kura ni Maalim kule Z'bar, basi!
Mbona unaweweseka sana juu ya wapinzani?
 
Kwani Membe ni CHADEMA? CHADEMA wanaendelea na kampeni kwa speed huku Lissu akimtandika spanner Magufuli,hiyo michango hao CHADEMA wanajazia tu kwenye kapu lao kama CCM wanavyowakamua wafanyabiashara kujazia kapu lao tens mwaka huu wamewakamua watumishi was umma kupitia form za kuomba kuteuliwa na CCM.
Umempatia jibu zuri sana labda atakuelewa mkuu
 
Chadema mfano imepata ruzuku mabilioni na michango ya kila mwezi ya wabunge madiwani ilipeleka wapi? Haikujua kuna uchaguzi ?
Yaani cdm kweli imewashika sehemu mbaya sana, huu uzi unahusika na mgombea wa ACT wazalendo, wewe unaijumlisha cdm?
 
Kwanini picha ya zitto,kwanini wasiweke picha ya mgombea urais ili kumtambulisha kwa wapiga kura au anaomba kwa ajili ya kampeni za jimboni kwake?
Hili nalo ni jambo la msingi sana, ila inawezekana labda ni kutokana na ugeni wa mgombea wa ACT mh Membe kwenye chama ndiyo maana ikawekwa picha ya Zitto
 
BERNARD Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, mazingira magumu ya Siasa kwa sasa, yamesababisha marafiki na wafanyabiashara kushindwa kuwasaidia. Na kwamba, kusuasua kwa kampeni hasa vyama vya upinzani nchini, kunatokana na ukweli kwamba, wagombea wengi wana ukata kwani hawana msaada tofauti na chaguzi zilizopita.

“Mnapokuwa katika mbio za urais, unatakiwa ukae ujipange kifedha na uwe na timu za kampemi, vyama vyote vyenye wagombea, wana ukata wa fedha sababu vyanzo vyetu vinavyokubalika kisheria, wafanyabiasha wanaotoa msaada wote wamekimbia, hatuna fedha,”

“Sababu nyingine, tunazuiliwa muingiza fedha, ukitaka kuingiza ama kutoa fedha, unakataliwa. Nikiwa rais, nitaboresha mfumo wa fedha kuiondoa changamoto hiyo,”

Akielezea sababu za kushindwa kuendelea na kampeni za urais kwa mujibu wa ratiba yake, amesema waliamua kusitisha kwa kuwa baadhi ya wagombea wa ubunge na udiwani kwenye chama chake waliwekewa pingamizi.

“Kilichotokea, baada ya kuteuliwa mgombea wa urais, sisi wabunge wetu zaidi ya 40 waliwekewa pingamizi.

Sasa akili inakutaka utafute changamoto ya tatizo kwanza. Huwezi kukurupuka peke yako, unawaacha wabunge na madiwani wamewekea pingamizi,” amesema Membe.

Akizungumzia safari yake ya Dubai Membe amesema, alikwenda kwa kuwa, ni ratiba yake ya kawaida kwa maana ndani ya mwaka mmoja anapaswa kwenda mara nne kutokana na shughuli zake binafsi.

“Kuna malalamiko kwanini ameenda Dubai kipindi hiki, huwa naenda Dubai mara nne kwa mwaka, kuna kampuni mimi ni mwanachama, sasa sikwenda mara mbili sasa nimeenda, lakini pia nimekwenda kucheki afya yangu,”

Mwanahalisi
ccm haiwez kupinduliwa
 
Kuna malalamiko kwanini ameenda Dubai kipindi hiki, huwa naenda Dubai mara nne kwa mwaka, kuna kampuni mimi ni mwanachama, sasa sikwenda mara mbili sasa nimeenda, lakini pia nimekwenda kucheki afya yangu,”
kucheki afya tu ni dubai,halafu anataka urais
 
Sasa hapo si ndio ingekua nafasi nzuri ya kumtambulisha mgeni wao
Hili nalo ni jambo la msingi sana, ila inawezekana labda ni kutokana na ugeni wa mgombea wa ACT mh Membe kwenye chama ndiyo maana ikawekwa picha ya Zitto
 
Atuambie kikao chake na wale waarabu wa libya na huyu muuza magari shinyanga kilihusu nini?
Je wamemruhusu kuchota sehemu ya ile pesa ya ghadaffi?

Aisha mulikwa huko muda ni shahidi mzuri
 
Kwa kinywa chake, nazid kumshusha thamani siku had siku. Bora angekua anakaa kimya.

1. Ufadhili wa wafanya biashara.
Kwani ikulu kuna biashara gan ambayo itamuwezesha kulipa fadhila.kumbuka wafanya biashara hawana pesa za kuchezea hovyo !!anachotoa jua utakirudisha tu.

2. Hawaruhusiwi kuingiza fedha.
Hiz ndio zile wanaficha account za nje ya nchi au ndio uadhil wa mataifa ya nje? Kama ni ufadhil, ana mpango wa kuzirudisha vp akipewa madaraka?

Kachero mbabaishaji bwana!
Aisee haya ni maswali makubwa sana ya kujiuliza
 
Jiandaeni kisaikolojia maana Lissu ndiyo rais wako wa awamu ya sita. View attachment 1570758
Jiandae kisaikolojia weye na huyo mtu maana baada ya uchaguzi inabidi aingie mahakamani kujibu yale madudu aliyoyakimbia muda wote huko ubeligiji......andaeni namba nyingi za mpesa kuchangia gharama za kamanda utopolo akihenya mahakamani
 
Jiandae kisaikolojia weye na huyo mtu maana baada ya uchaguzi inabidi aingie mahakamani kujibu yale madudu aliyoyakimbia muda wote huko ubeligiji......andaeni namba nyingi za mpesa kuchangia gharama za kamanda utopolo akihenya mahakamani
Nakuona kama wewe ni mgeni wa mh Lissu, huyo ndiye mwamba wa mambo ya kisheria hababaishwi na lolote kinalo andaliwa juu yake na maccm.

Lissu ni mpango au zawadi ya kutoka kwa Mungu ili aje kuwakomboa watanzania.
 
Back
Top Bottom