Imetokea leo mchana maeneo ya kituo cha bandari kurasini.. kuna jamaa ana ofisi yake (frame) ya kuziba pancha na kuongeza upepo ni jirani yetu kabisa na ofisi yetu ndogo (branch) ambayo hua napita siku moja kila wiki. Huyu jamaa ni mkimya sana sijawahi kuzoeana nae ila salamu tu na nimewahi kumuomba chenji mara kadhaa.
Sasa basi asubuhi ile nafika tu pale ofisini nje nilikuta watu wanne wanaongea wanajadili kua jamaa hajafungua ofisi siku ya pili, simu yake haipatikani na wana wasiwasi yumo mule ndan mana amekua akilala ndani ya ile frame yake kwa wiki kadhaa baada ya kukorofishana na mke wake.
Nilitoa salamu, nikasikiliza mawili matatu ya wale jamaa nikaingia ndani.. kijana wa pale ofisini akaanza kunipa mkasa mzima coz yeye anashinda pale daily.. akanieleza yule jamaa alikua ni mlevi sana ila mawiki kadhaa alizidisha ulevi wa kupindukia na chanzo anasema alikua na ugomvi na mke wake hadi kupelekea kuhama kwake akaanza kulala mule ofisini. Hii ishu walikua wanajua watu wachache sana mana jamaa ni mkimya mno.
Basi kama mnavojua protocol za kibongo kuchelewesha mambo, jamaa baada ya kushauriana pale walimfata mwenye nyumba anaekaa nyuma ya zile frame kumshirikisha juu ya hofu yao kua jamaa yumo mule ndani, mwenye nyumba akaenda kwa mjumbe kaandikiwa barua wakaenda polisi ili waje nao pale wabomoe kuingia .. hizi taratibu zote zilichukua masaa mengi yan mpaka polisi wanakuja pale ni saa 8 mchana, hili nalo lilinikera sana!
Walimkuta kweli jamaa kajikunyata sakafuni mule ndan anatoka mapovu ila bado anapumua ndio kumpandisha gar kumuwahisha hospital ya bandari ambapo haikuchukua round akaaga uhai.
Watu wanamlaumu mke wake jamaa kufa kwa style ile kidhalili japo wote hatujui ugomvi wao ni wa nn, mwenye nyumba kapagawa anawaomba wapangaj wote wasiseme kua jamaa alikua analala pale kuepuka usumbufu wa upelelezi.
Mchana huo huo nikapokea taarifa ya mjomba wangu kapata ajali mbaya sana ya gari mkoani na kufariki hapo hapo, eeh Mungu tunaomba mwisho mwema [emoji2969]
Haya maisha jamani, kila mtu ana mzigo wake anaotembea nao kila siku na yeye pekee ndio anajua yanayomsibu..hakuna mwalimu bora zaidi ya muda na yote tunayopitia ni sehemu ya mafunzo.