Kafulila: 2008 SYNOVATE walisema tatizo namba moja la Watanzania ni maji

Kafulila: 2008 SYNOVATE walisema tatizo namba moja la Watanzania ni maji

Sorry, Mimi sio Kafulila.

Maji mwaka wa kumi unamaana gani?

Umeshavuta bomba ila maji hayatoki?

Au hakuna mabomba?

Fafanua Mzee,
Kafulila umekuja na ID mpya. Baada ya kuona watu wamekushtukia na kukupotezea. Maana kila saa ulikuwa unahangaika kupandisha nyuzi zako zote za nyuma ila ukazidiwa na Gen Z wa Kenya na issue ya Mpina. Fanya kazi acha uchawa.
 
Ulijaribu kupandisha nyuzi zako baada ya kusahaulika. Naona umeamua kuleta nyuzi mpya.
Acha uongo wako hapa ndugu yangu.mbona mimi ninamuandika sana Mheshimiwa Kafulila na wala siyo kwamba ninalipwa au kuwahi kuonana naye? Fahamu ya kuwa Mheshimiwa Kafulila anakubalika na kupendwa na watanzania kutokana na uchapakazi wake, uzalendo wake na upeo wake mkubwa alio nao.najuwa CHADEMA mnaumia sana na mnatamani sana angekuwa ndani ya chama Chenu ili awasaidie kwenye hoja mbalimbali
 
Kigambona gani haina maji bro?
Sio kigambona, ni kigamboni mjimwema, kibugumo, geza, mawezi, ungindoni na kwingine koote huko ni mwendo wa visima tu, raisi walimuingiza chaka alikuja kuzindua mradi haijakamilika, ye anazindua wakati hata bomba chini zilikuwa hazijatandazwa, kifupi mpaka leo yale maji aliyozindua hakuna kitu.
 
View attachment 3027483
Katika Ukurasa wake wa (X) zamani tweeter Mkurugenzi wa PPP-Cetre Tanzania Bw David Kafulila ameandika haya,

Kampuni maarufu duniani yenye kuaminika zaidi ya Steadman / SYNOVATe miaka ya 2008 iliwahi kubaini tatizo kubwa la Watanzania kwa wakati huo lilikuwa ni maji safi na salama.

Kafulila anasema tangu Rais Samia ameingia madarakani bajeti ya maji ni kubwa na inatekelezwa kabla ya wakati mara zote miezi minne kabla ya mwisho wa kipindi cha bajeti.

Kafulila anasema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitekeleza kati ya 75% hadi 92% kwa kipindi chake chote Cha miaka mitatu,

Leo, chini ya Rais Samia na kwa miaka hii mitatu upatikanaji wa Maji vijiji ni 80% kutoka 70.1% mwaka 2020.

Hata hivyo, Upatikanaji wa Maji mijini umeongezeka kutoka 85% mwaka 2020 mpaka 90% leo,

Ndio maana Tanzania inasema Mama Samia mitano tena inamuhusu.
Ukweli ni huu,
Rais Samaia anejitahidi sana kwenye Sekta ya maji,mengine ni mambo ya kawaida katika Uongozi.
 
Wapumbavu nyie,Yani miaka Zaidi ya 60 ya uhuru tunazungumzia maji? Kwa utajiri WA nchi HII mambo ya maji,barabara na umeme vingetakiwa viwe tangu miaka ya 90 au at least 2000
CCM wamedhoofisha nchi
Ni wapumbavu haswa! Dodoma mjini mabomba yapo tu hayatoi maji watu wanatumia maji ya visima.
 
Mama Samia anapiga kazi sana hakika mitano inamuhusu tu
Kwa hakika anastahili mitano mingine pamoja na kumpelekea Bungeni vijana wengine akili kubwa aina ya Mheshimiwa David Kafulila.
 
Back
Top Bottom