Umasikini mbaya kuliko wote ni ule wa fikra.Halafu kibaya zaidi ni kuwa sisi wenyewe watanzania hatujui matatizo yetu Hadi aje mzungu mkoloni huyo wa SYNOVATe
ndiye atufanyie utafiti aseme shida kubwa mko.nayo ni maji ndio Serikali ianze kufanyia kazi
HIi Nchi tuwarudishie tu Wakoloni waendelee tu kututawala Sababu ndio wanajua hasa matatizo tuliyonayo kuliko Hivyo vichwa vitupu vilivyoko serikalini akiwemo Kafulila
Hii ndiyo changamoto inayojenga na kuimarisha msingi wa umasikini wa Tanzania na Africa ya weusi (waarabu na makaburu ni tofauti, kwa wale tuliofika kwao na tuna akili tuliona na kupata uzoefu).
Viongozi wetu na watumishi wa uma wanatakiwa kuelewa kwamba, tafiti za kweli na suluhu ya matatizo yetu itapatikana kwa wananchi wenyewe.
Sera ya elimu lazima ibadilishwe kuondoa elements za ile ya kikoloni.
Hizi elimu za kukariri ni changamoto.
Tunatakiwa pia kuhakikisha watoto na vizazi vijavyo, kuanzia gen z, kutokubaliana na ujinga, uwe kwa wenyewe au kutoka kwenye mamlaka za kiserikali, hivyo wataweza kushindana na kujenga taifa lao kufaidi duniani.
Hata hivyo, tunatakiwa kuwaanda na kuwadhibiti wasifanye fujo kama Kenya.