Tetesi: Kafulila kuwa mmoja wa wakuu wa wilaya wapya watakaoteuliwa hivi karibuni

Tetesi: Kafulila kuwa mmoja wa wakuu wa wilaya wapya watakaoteuliwa hivi karibuni

Chama ndio kinaimarika mkuu!

Kwa kuzirudisha oil chafu kwenye injini na kuwapa uongozi. Sawa lakini naona kuna walakini. Hebu fikiri, kuna watu wamesotea bench miaka nenda miaka rudi. Hawajathubutu kusema nahama, hao oil chafu walichoka kusubiri wakahama. Wakakitukana chama kwa nguvu zao zote. Leo wamerudi, wakawakuta wale wa kusotea wapo pale pale. Wamepewa u dc wadhani wanajisikiaje? Ni swali tu wala sio uchochezi wala ushauri. ni swali tu. Kwani hamshauriki
 
Siasa bhana acha tu
Mkewe ni mbunge wa chadema Viti maalum atajiuzulu hiyo nafasi au
Nyumba itakuwa na upinzani baba CCM na Mama Chadema itawezekana hilo kweli?
Au jamaa kaanza kuhisi mkewe anaibiwa anavyohuzulia vikao vya bunge na majukumu mengine ya kibunge? Ila hapa mama kapewa mtihani akitaka ndoa isiyumbe akubali kujihuzulu ubunge ili sense na mumewe uko haendako maana ndoa haiwezi kuwa sawa mama awe mbunge chadema afu baba kada ccm afu apewe ukuu wa wilaya
Ndani patakuwa hapakaliki na ndoa itakufa hapa Jesca kafulila ajitathmini tu
Akijiuzulu mama anaweza kupewa hata u-DED
 
Makufuli is suffering from Allodoxaphobia that is the fear of opinions.
 
Kwa kuzirudisha oil chafu kwenye injini na kuwapa uongozi. Sawa lakini naona kuna walakini. Hebu fikiri, kuna watu wamesotea bench miaka nenda miaka rudi. Hawajathubutu kusema nahama, hao oil chafu walichoka kusubiri wakahama. Wakakitukana chama kwa nguvu zao zote. Leo wamerudi, wakawakuta wale wa kusotea wapo pale pale. Wamepewa u dc wadhani wanajisikiaje? Ni swali tu wala sio uchochezi wala ushauri. ni swali tu. Kwani hamshauriki
Sasa mkuu mtu kama le mutuz pamoja na ukweli kuwa amekisotea chama unaweza kumpa cheo kipi? Na watu aina ya le mutuz ndani ya chama ndio wako wengi lakini CCM mpya inahitaji watu aina ya Polepole, NW Mavunde na huyu Kafulila maana hawa wanasema na kutenda!!!
 
Ni dhahiri shairi kabisa kuwa kuna mipango thabiti iliandaliwa na ccm katika kuhakikisha watu hawa wanaungana nao ili kupunguza nguvu ya upinzani lakini kwa bahati mbaya, ndiyo kabisa upinzani unazidi kuimarika na wala hautetereki kwa namna yoyote!
Ni wazi kuwa kuna nguvu ya ushawishi ilitumika ili kuwanasa, na wapo wengine wanaendelea kishawishika hivyo ni suala la muda tu.
Tumeshuhudia Sofia Simba akirejeshwa ccm, hilo siyo jambo la bahati mbaya! Ni mipango ilipangwa...
Hawa vijana waliohamia ccm , Laurence Masha, Katambi pamoja na kafulila kwa kuangalia sababu walizozitoa hakika huwezi kukubaliana na hoja zao, na hata endapo ungewaangalia usoni wakati wakitoa hoja zao ungegundua kulikuwa na ushawishi flani ndani yao.
Yamkini watu wameshaanza kuhisi kuwa pengine watateuliwa kuwa wakuu wa wilaya, lakini Ngosha naye huwa hatabiriki vizuri sana!
Bila shaka huwa anapita kwenye mitandao na kupitia mijadala mbalimbali na kuona upepo ulipo na hapo anafanya kitu tofauti kabisa...
Hawa watu wana nafasi ndogo sana ya kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya hivi karibuni...
 
Mpendazoe tangu arudi ccm amepewa nafasi gani!

Ova
 
ni sawa tu, maana si kwamba mtu anaetoka upinzani hawezi kuwa kiongozi mzuri.
 
Kafulila Mkuu wa wilaya ya Hai, kwa kazi maalumu, Katambi Mkuu wa wilaya ya Arumeru kazi maalumu, Marsha hana umuhimu wowote kwa kuwa yeye ni ccm damu asitarajie uteuzi wowote. Kitila kugombea ubunge jimbo la Nyalandu, Mwigamba hana impact kwenye siasa , atasugua benchi kama Machali , sawa na msando.
 
Back
Top Bottom