Kafulila: Kwa miaka mitatu Rais Samia amekopa nje TZS 12.5T sawa US$ 5BL lakini amelizalishia Taifa TZS 47.5T sawa na US$19BL

Safi sana
 


Ameingia March 2023 deni la taifa $31.4 billion.


Source ☝️

Hadi December 2023 deni limefika $41.8 billion. Chini ya miaka mitatu amekopa zaidi ya $10.4 billion kiasi ambacho Magufuli kakopa kwa miaka 6 walau hela ilionekana ilichofanyia.

Hizo data last updated January 2024 sasa hivi BoT wakitoa new update atakuwa keshapita $12 billion za kukopa yeye mwenyewe kwa miaka mitatu tu.
 
Hakuna nyumbu wa CHADEMA anayeweza kupangua hoja hizo nzito za Mheshimiwa Kafulila. watakachoweza nyumbu ni kutukana matusi tu. Ngoja nimwite Erythrocyte

Erythrocyte njoo huku usikilize hoja.
Kafulila alikuwa ababeba mafaili dk slaa we ndo unajivunia Leo kuwa naye
 
Kafulila kuzungumzia deni la nje tu ,
 
Uongo mweupe tu wa michawa hii.
Nyie kuleni kwa kamba zenu msitupoteze maboya huku.
 
Kafulila kuzungumzia deni la nje tu ,
Deni la nje sio deni pekee la serikali ni misleading keshakopa $10.4 billion hiko ndio kiasi cha deni ambacho utakikuta DMO wizara ya fedha na ndipo BoT walipopata hizo takwimu zao.

Ukitaka kukopa tena nje au ndani uwezi kusema nimekopa $5 billion tu na ndani 5.4 billion hiko sio kigezo cha kupima debt sustainability wanataka kujua unadaiwa kiasi gani in total na mpaka sasa atakuwa keshavuka $11 billion.

Kufanya selection ya deni ni misleading statement.

Mtangulizi alikuwa na wastani wa $1.67 billion kwa mwaka, maza mpaka wastani wake wa kukopa ni $3.67 billion kwa mwaka.
 
Hoja yako ni ipi!?

Rudia kusoma kilichoandikwa uelewe na uje na hoja

"Rais Samia amekopa nje TZS 12.5T sawa US$ 5BL lakini amelizalishia Taifa TZS 47.5T sawa na US$19BL"​


..kama Maza ana mapesa yote hayo kwanini halipi deni lote ili nchi isidaiwe?

..au kwanini asitusamehe kodi na tozo walau mwaka mmoja?

..nadhani Kafulila ana data lakini hajui kutafsiri kinachoelezwa ktk data.
 
..kama Maza ana mapesa yote hayo kwanini halipi deni lote ili nchi isidaiwe?

..au kwanini asitusamehe kodi na tozo walau mwaka mmoja?

..nadhani Kafulila ana data lakini hajui kutafsiri kinachoelezwa ktk data.
Nia yako ni ipi hapo?
 
Kamishina wa PPP Mhe David Kafulila anasema "Wakati Rais Samia anaingia madarakani Uchumi wa Tanzania ulikuwa US$ 66BL Leo ni US$ 85BL sawa na ongezeko la US$19 wakati deni la nje ni US$ 5BL tu.

View attachment 2945755

Kura hazipatika JamiiForums ila zinatoka hukoooo mkoani, hizi Takwimu zinamufaishaje mtu wa Kantalamba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…