The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Bahati nzuri mimi niliusikiliza huo mjadala wa TL na wenzake huko Club House (nitaweka link hapa)..Wasalaam wana wa Mungu.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Zacharia Kafulila, amekosoa kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A Lissu kuhusu hoja ya kesi ya kukamatwa kwa Ndege na zingine mashauli yake kushughulikiwa kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya kibiashara kama ICSID- international Center For Settlement of Investment Disputes.
====
Akikosoa kauli hiyo, David Zacharia Kafulila amenukuliwa kwenye mtandao wa tweeter akiandika haya " Sitaki kujadili suala la kesi, naomba nijadili suala moja tu la uelewa kuhusu ICSID na Uanachama wake kwani Tundu A Lissu amepotosha katika hilo na huenda akawafanya wasiofahamu kuamini kwamba Tanzania ni mwanachama wa ICSID kwa Sababu ya Udhaifu wa Mahakama na Serikali ya Tanzania katika kusimamia Uhuru wa Mahakama.
Tundu A Lissu alinukuliwa kupitia ClubHouse akieleza kuwa " Lazma ieleweke kuwa sababu ya mashauri haya ya mikataba baina yetu na kampuni za nje kushughulikiwa kwenye mabaraza haya ya usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kama ICSID inatokana na tabia ya Serikali yetu ikiwa chini ya JPM na hata Samia kuingilia mambo ya mahakama na hivyo mahakama kukosa uhuru. Hivyo mahakama zetu haziaminiki, serikali yetu haiaminiki, hatuaminiki kwasababu ya rushwa za majaji na kuingiliwa na Ikulu. ndio sababu mashauri haya yanamuliwa ICSID "
Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.
David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 kumuuliza Tundu A. Lissu kuwa nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuoneaha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?
Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja ya hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?
" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"
View attachment 2433362View attachment 2433363
Lakini ni bahati mbaya kuwa Kafulila hata hajamwelewa Tundu Kiasi...!!
JIBU KWA SWALI LA KAFULILA NI HILI:
Ni kweli USA na CHINA ni wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania na nchi zingine 165 duniani...
Lakini ni ukweli pia kuwa, CHINA na USA mahakama zao haziingiliwi na serikali zao kama ilivyo kwa mahakama za nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania...
Aidha mikataba ya kimataifa (International bilateral agreements), mwekezaji mwenye mgogoro na serikali husika, ana uhuru akiona inafaa (hasa kwa kigezo cha uhuru wa mahakama ktk nchi husika) kusuluhishwa na mahakama za ndani au kwenda straight huko ICSID...
Kwa kigezo hiki, ndiyo Lissu akasema, kwa Tanzania ambapo mahakama zinafanya kazi kwa kuangalia interests za mtawala (serikali), hakuna mwekezaji aweza kuziamini mahakama zetu hata huyo Jaji au hakimu akampa haki mwekezaji ku - seize mali za serikali kama inavyofanyika huko ICSID...
Kwa lugha rahisi, ni kuwa, TL alimaanisha hakimu au Jaji wa mahakama hawezi kuhukumu against serikali...!!