Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Bahati nzuri mimi niliusikiliza huo mjadala wa TL na wenzake huko Club House (nitaweka link hapa)..

Lakini ni bahati mbaya kuwa Kafulila hata hajamwelewa Tundu Kiasi...!!

JIBU KWA SWALI LA KAFULILA NI HILI:

Ni kweli USA na CHINA ni wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania na nchi zingine 165 duniani...

Lakini ni ukweli pia kuwa, CHINA na USA mahakama zao haziingiliwi na serikali zao kama ilivyo kwa mahakama za nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania...

Aidha mikataba ya kimataifa (International bilateral agreements), mwekezaji mwenye mgogoro na serikali husika, ana uhuru akiona inafaa (hasa kwa kigezo cha uhuru wa mahakama ktk nchi husika) kusuluhishwa na mahakama za ndani au kwenda straight huko ICSID...

Kwa kigezo hiki, ndiyo Lissu akasema, kwa Tanzania ambapo mahakama zinafanya kazi kwa kuangalia interests za mtawala (serikali), hakuna mwekezaji aweza kuziamini mahakama zetu hata huyo Jaji au hakimu akampa haki mwekezaji ku - seize mali za serikali kama inavyofanyika huko ICSID...

Kwa lugha rahisi, ni kuwa, TL alimaanisha hakimu au Jaji wa mahakama hawezi kuhukumu against serikali...!!
 
Zipo Kesi kibao Tanzania tumebwagwa na wawekezaji humu humu ndani,
 
Kimsingi mahakama zetu zingeaminiwa na wawekezaji wa kimataifa, wasingelazimisha arbitration ifanyike katika mahakama za kimataifa.

Kwa hivyo, sioni alipokosea Tundu Lissu.
 
BIT ni bilateral investment treaties maana yake ni kwamba serikali A na B wanawekeana mkataba kwamba mwananchi wa A akiweza B asijeakadhulumiwa and B na mwananchi wa B akiweza A asijeakadhulumiwa. Kama atadhulumiwa mali zake anahaki ya kwenda kwenye arbitration. Viena ,The Hague,London,Singapore and Washington DC Magufuli aliamua not to renew same of the expired BIT but he forgot that most of the BITs have a sunset clause that can take up to 10 years all in all the country was doomed to fail in its endeavor to rob investors
 
Nchi ambayo haina BIT mwekezaji akienda huko anashauriwa kuwa na MIGA
Unachanganya mambo. Suala la arbitration linawekwa kwenye mkataba na taasisi itakayokubalika na pande zote mbili. Bila kipengele hicho wawekezaji hawatii saini.

Amandla...
mwekezaji akienda huko anashauriwa kiwa na MIGA
 
Umeandika hadithi isiyokuwa na content.

Unadhani kwa nini mataifa, hasa mataifa ambayo wala hayakuwa waanzilishi wa mahakama hii, huamua kuwa wanachama wa hizi mahakama za biashara?

Kwa nchi za Africa na Asia, kama hujui, ni kwamba sababu kubwa ya mataifa kujiunga na taasisi hizi ni kujenga confidence kwa wawekezaji kuwa hamwezi kuwadhulumu kwa kutumia mahakama zenu za ndani zinazoamriwa kutoa hukumu kwa matakwa ya watawala.

Mfano mmojawapo ni kwamba sisi hapo awali hatukuwa wanachama wa taasisi hii. Mkapa alipoingia madarakani, uchumi ukiwa umedorora kabisa, misaada na mikopo kutoka taasisi za fedha tumezuiwa kupewa, Rais Mkapa akaanza kufanya jitihada kubwa kuwapata wawekezaji. Sekta iliyoonekana ingeweza kuwavutia wawekezaji wa nje, ni sekta ya madini. Kwa sababu Tanzania ilikuwa na miundombinu duni kabisa, wataalam walishauri kuwa ni lazima yapatikane makapuni makubwa yenye mitaji mikubwa ndiyo yanayoweza kuwekeza kwenye sekta ya madini, makampuni yatakayokuwa na uwezo wa kujenga miundombinu yao kama umeme, maji na barabara.

Kampuni iliyoonekana kuwa na uwezo huo, kwenye top list ilikuwa Barrick Gold. Serikali ilipoiomba Barrick Gold kuja kuwekeza Tanzania, kwa kumtumia Andrew Young, rafiki wa Hayati Mwalimu Nyerere, Barrick waligoma, wakisema kuwa nchi haina investment security code, tena ikiwa na record mbaya kabisa ya kutaifisha mali za makampuni na watu binafsi mwaka 1967.

Serikali ilijitetea sana kuwa utaifishaji hautatokea, bado Barrick hawakuridhika, wakagoma kuwekeza Tanzania. Serikali ikaiomba World Bank isaidie kuishawishi Barrick. World Bank ikaiambia Serikali ya Tanzania kuwa ili kuwapa confidence Barrick, ni lazima nchi iwe mwanachama wa ICSID na WTO ili nchi ikikiuka, Barrick wawe na uwezo wa kuishtaki. Serikali ya Tanzania ikajiunga. Walivyowaendea Barrick, Barrick bado waligoma kwa maelezo kuwa Tanzania haina mali ya kufidia gharama iliyopo nje ya nchi ambayo wataichukua kama Tanzania itaenda kinyume na haki. Serikali ikalazimika kukopa dola mioni 400, na kuziweka kama bond. Baada ya hapo ndiyo Barrick wakaja kuwekeza Tanzania.

Kama hujarlewa mpaka hapo, sina la kukusaidia.
 
Yan huyu Tumbili badala ya kushauri serikali ilipe deni anakimbilia kum attack Lissu ili akumbukwe tena kwenye uteuzi, Chawa pro max pumbavu kweli
Sidhani kama anaweza kumteka Rais Samia kwa kauli za kinafiki kama hizi.
 
Naongezea serikali ikakubali Bima ya MIGA
 
Hivi Watanzania wanajua kwamba nchi yao ina kesi ngapi za namna hii??ambazo zitasababisha mali nyingi kukamatwa??na kwa nini waandishi wa habari hawataki kujituma na kwenda kwenye mtatandao wa hizi kesi na kuandika habari zote ili kuwaelimisha Watanzania??Au kuwaweka gizani ndio strategy ya serikali??Kwani kodi zao ndio zinatumika kulipa mambo kama haya
 
Symbion walipwa bila kushinda kesi lakini Watanzania waliambiwa nchi imeshindwa kesi
 
Bahati nzuri mimi niliusikiliza huo mjadala wa TL na wenzake huko Club House (nitaweka link hapa)..

Lakini ni bahati mbaya kuwa Kafulila hata hajamwelewa Tundu...!!

JIBU KWA SWALI LA KAFULILA NI HILI:

Ni kweli USA na CHINA ni wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania na nchi zingine 165 duniani...

Lakini ni ukweli pia kuwa, CHINA na USA mahakama zao haziingiliwi na serikali zao kama ilivyo kwa mahakama za nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania...

Aidha mikataba ya kimataifa (International bilateral agreements), mwekezaji mwenye mgogoro na serikali husika, ana uhuru akiona inafaa (hasa kwa kigezo cha uhuru wa mahakama ktk nchi husika) kusuluhishwa na mahakama za ndani au kwenda straight huko ICSID...

Kwa kigezo hiki, ndiyo Lissu akasema, kwa Tanzania ambapo mahakama zinafanya kazi kwa kuangalia interests za mtawala (serikali), hakuna mwekezaji aweza kuziamini mahakama zetu hata huyo Jaji au hakimu akampa haki mwekezaji ku - seize mali za serikali kama inavyofanyika huko ICSID...

Kwa lugha rahisi, ni kuwa, TL alimaanisha hakimu au Jaji wa mahakama hawezi kuhukumu against serikali...!!
Zipo Kesi kibao Tanzania tumebwagwa na wawekezaji humu humu ndani,

Ni kweli...

Na pale iliposhindwa serikali, hukataa kutekeleza hukumu hiyo...
 
Kafulila endelea na kuwakosoa Hawa Wamarekani
 
Nchi ambayo haina BIT mwekezaji akienda huko anashauriwa kuwa na MIGA

mwekezaji akienda huko anashauriwa kiwa na MIGA
Mkataba wowote una kipengele cha nini kitafanyika pakitokea disputes. Ili kuepuka kukimbilia Mahakamani, mikataba inasema hatua ya kwanza ya kuresolve disputes ni arbitration na taasisi itakayosimamia. Mara nyingi kwenye mikataba ya ujenzi ya hapa nyumbani taasisi inayotajwa ni NCC. Kwenye mikataba ya kimataifa mara nyingi taasisi inakuwa ICC. Ila kama dispute ni kati ya mwekezaji na serikali, taasisi inayohusika ni ICSID. Sina uhakika kama inakuwepo kwenye mkataba ila nadhani mwekezaji mgeni yeyote ambae anaona hajatendewa haki na serikali mwenyeji ambayo ni signatory ana haki ya kupeleka mashtaka ICSID.

Amandla...
 
Kipengele kinakuwa Diplomatic mwekezaji anakwenda kwenye ubalozi wake Tanzania balozi anajaribu kuwasiliana na wizara ya mambo ya nje.Wizara yetu ya mambo ya nje ilikuwa ya ajabu sana kwani nchi nyingi zilijaribu kuwasiliana nao lakini wakawa na dharau .Baada ya miezi sita mwekezaji anaambiwa na nchi yake aende The Hague akatafute haki yake usilaumu wawekezaji wengi ni wazalendo sana na wanajua ufedhuli unaofanyika Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…