Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Sasa kama Mahakama za Tanzania zinaaminika, kwanini Huyo aliyetushtaki hakwenda Mahakama Kuu ya Tanzania.

Tuache hayo. Lakini Moja ya sababu za kuanzishwa kutuo hiki Cha ICSID pamoja na vingine, Moja ni kutokana na Ukiritimba wa Mahakama za ndani, Uhuru. Wenye shaka wa Mahakama za ndani, kuspeed up usikilizwaji na uamuzi wa mashauri, uwepo wa Sheria zinazoilinda serikali hata inapokuwa negligent pamoja Specialisation

Haya yote huweza kuyapata kwa uhakika katika Mahakama za ndani. Embu jiulize wakati wa Katili Magufuli ni Jaji yupi Tanzania angeweza akasema serikali imekosea kivunja mkataba wa Beberu?

Lakini pia kwa mujibu wa Sheria za ndani hata kama ukiishinda serikali ni vigumu sana kukulipa. Kamuulize Vhlambia.

Itoshe tu kusema kwamba Kafulila amefulia huko nje, anajua jina la Lissu ni kete inayoweza kimfanya Raisi akamkimbuka, Lakini Hana hoja.

Lissu is right.
 
Migogoro yote ya kibiashara za kimataifa zinatatuliwa na ICSID
 
Wasalaam wana wa Mungu.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Zacharia Kafulila, amekosoa kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A Lissu kuhusu...
Lissu ni mtu mwenye akili sana ila anazitumia kuliumiza Taifa
 
Kama hoja ni mbona hata US nao ni wanachama?

..Nchi zenye mahakama safi kama USA zimejiunga na ICSD / MIGA ili wawekezaji wake waweze kushtaki nchi zenye mahakama za hovyo kama Tanzania.

..kama USA ingekuwa sio mwanachama wa ICSD basi wawekezaji / wafanyabiashara wake wangelazimika kupeleka mashauri yao ktk mahakama [ zenye rushwa, zinazoingiliwa] za ndani ktk nchi ambazo wamewekeza.

..MIGA / ICSD imeanzishwa kama chombo kinachoaminika na wawekezaji kulinda mitaji na biashara dhidi ya utaifishaji na uvunjwaji mikataba kiholela. Pia ilionekana mahakama kutokana na rushwa na kuingiliwa na serikali hazina uhuru wa kuamua kwa haki migogoro ya uwekezaji.
 
..hapa chini ni maelezo ya Wakili Sungusia kuhusu mahakama na sheria za Tanzania.

..yaani hata ukiishinda serikali ya Tanzania mahakamani suala la kufidiwa ni mpaka wahusika wajisikie kufanya hivyo.

" Serikali imetunga sheria nyingi za kujilinda na malalamiko yanayoletwa na wananchi katika Mahakama za Tanzania. Serikali inafanya biashara lakini imejiwekea mazingira hapa ndani kwamba ukifanya biashara na Serikali ikakiuka makubaliano ukaishinda huwezi kufungua kesi bila kuomba ruhusa na kutoa notisi ya siku 90, na hata ukishinda kesi huwezi kukamata baiskeli hata ya Mwenyekiti wa Kitongoji au Kijiji, yaani huwezi kukamata mali yoyote ya Serikali au ya Serikali za Mitaa wala taasisi zozote za Serikali au Mashirika yanayofanya kazi kwa niaba ya serikali..." -- Wakili Sungusia
 
Anyway Kafulila ana hoja , ila hutupo kumtetea rais na serikali hiyo ni KAZI ya msemaji wa serikali,

..kafulila hana hoja.

..Marekani yuko kwenye Icsd / Miga ili makampuni ya Kimarekani yaweze kuzishitaki serikali ambazo mahakama zake zimejaa rushwa na mizengwe.

..Icsd / Miga iliundwa ili ku-deal na nchi ambazo mahakama zake haziko huru, na zina historia au tabia ya kutaifisha mali za wawekezaji toka nje.

..Marekani yuko pale kwa nia ya kulinda mitaji ya makampuni yao yanayowekeza ktk nchi mbalimbali, na sio kwasababu mahakama zao hazina uwezo au zimejaa rushwa.
 
kavimbiwa Asali huyo Mbuzi.

ukiitwa Mbuzi jiulize mara 2

kwanza mbuzi ktokana na hajielewi mbuzi anatumika zaidi kwenye makafara.

Mbuzi unaweza kumuweka apo ale majani, akayaacha majani mazuri. akaenda mbaali kwanza akale majani mpya, labda umfunge kamba.

Mbuzi ndio mnyama pekee anaweza akakutolea macho kwa kukuangalia utadhani anakufahamu siku nyingi.

Sasa na Mbuzi ingine inakuja kujibu hoja ikiwa imelegeza macho na kuchezesha taya huku ikiongea upuuzi kwa kutuona na sisi ni mbuzi kama yeye
 
Watu wenye akili za kawaida sometimes sio rahisi kuwaelewa watu wenye akili nyingi.

Lisu hajawahi kuwa na akili. Kama unanibishia, akigombea uenyekiti wa chama chenu, utaniambia kama atashinda.
 
Nauliza tu
Upinzani upo au tuanzishe vyama mbadala.
Chadema Mpo kimya yote yanatokea mnayabariki kimtindo
Mmezibwa midomo au
What’s the point ya kuwa na safari na Mikutano ya nje huku mkijua haiwasaidii zaidi ya kupiga maphotooo
 
Kafulila hawezi kujibizana na Lisu!
 
Jaji mkuu mstaafu Chande aliwahi kumlalamikia mwendazake kuhusu vimemo vya kuwalazimisha mahakimu jinsi ya kutoa hukumu, na tumekuwa tukishuhudia mienendo ya kesi isiyoridhisha.
 
Kwani suala ni uanachama au kesi kupelekwa ICSID? Kesi ngapi zinazohusu serikali za Marekani na Singapore zimefunguliwa ICSID? Ni sababu gani kesi zinazotuhusu sisi na wageni zinapelekwa ICSID na sio kwenye Mahakama yetu ya Biashara?

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…