Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Kafulila: Lissu acha kuzipaka matope Mahakama za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa?

Mbona mmetaka ziwafukuza akina Halima mmegonga Mwamba?

Eti Mnataka Rais atoe maelekezo mahakamani hili halipo.

Mahakama zetu ni huru sana.

Kwa taarifa yako hakuna mahakama Tanzania, bali kuna majengo ya mahakama yanayoendeshwa na wanaccm. Kesi ya wabunge 19 inaendeshwa mwaka wa pili huu, wakati kenya hapo kesi ya uchaguzi wa urais haikuvuka hata mwezi. Sasa hapo kuna mahakama au uchafu?
 
Unataka Wafanywaje akina Halima Mkuu?

Hiyo kesi ilipaswa kuwa imekwisha kwenye mahakama huru. Kesi ya urais hapo Kenya imeisha ndani ya muda mfupi kwakuwa mahakama za Kenya wangalau zina uhuru wa kutosha. Hapa ni nini kinaendelea kwenye hiyo kesi ya Covid19?
 
Kitendo Cha mahakama kutumika na CCM kuwakinga kina Halima Mdee ni dharau.
 
Lissu Hana akili?. Definition ya akili ni Nini? Kapata division 1 0 level and A level, kapata hons bachelor na kapata distinction Warwick. Kama hana akili na kapata vyote hivi je, wewe umepata Nini?.

Usiwe mwepesi wa kutamka maneno Kama huna uhakika. Angekuwa Hana akili asinge limwa risasi na serikali dhalimu na mwishowe dhalimu akadondoka yeye.

Akili haipimwi kwa namna ambayo unaisema. Wapo wengi tu ambao wamemzidi kwa mbaali Tundu. Kuna vigezo vingine vingi tu vinavyoangaliwa.
Kwa sasa huwezi ukanielewa, mpaka mtakapofanya uchaguzi wenu wa Mwenyekiti ndiyo utanielewa. Maana nasikia Mbowe kasha sema basi.
 
Kwahiyo unaomba Lissu akusamhe??

Asiposamehe, asifikiri anamkomoa JPM au yeyote. Anajikomoa yeye. Maana unaposamehe katika maisha haya, unakuwa unajitendea wema mwenyewe. Vinginevyo chuki zikizidi ndizo zitakazo muua, licha ya kuwa alipona risasi za Dodoma.
 
Wasalaam wana wa Mungu.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Zacharia Kafulila, amekosoa kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A Lissu kuhusu hoja ya kesi ya kukamatwa kwa Ndege na zingine mashauli yake kushughulikiwa kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya kibiashara kama ICSID- international Center For Settlement of Investment Disputes.

====

Akikosoa kauli hiyo, David Zacharia Kafulila amenukuliwa kwenye mtandao wa tweeter akiandika haya " Sitaki kujadili suala la kesi, naomba nijadili suala moja tu la uelewa kuhusu ICSID na Uanachama wake kwani Tundu A Lissu amepotosha katika hilo na huenda akawafanya wasiofahamu kuamini kwamba Tanzania ni mwanachama wa ICSID kwa Sababu ya Udhaifu wa Mahakama na Serikali ya Tanzania katika kusimamia Uhuru wa Mahakama.

Tundu A Lissu alinukuliwa kupitia ClubHouse akieleza kuwa " Lazma ieleweke kuwa sababu ya mashauri haya ya mikataba baina yetu na kampuni za nje kushughulikiwa kwenye mabaraza haya ya usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kama ICSID inatokana na tabia ya Serikali yetu ikiwa chini ya JPM na hata Samia kuingilia mambo ya mahakama na hivyo mahakama kukosa uhuru. Hivyo mahakama zetu haziaminiki, serikali yetu haiaminiki, hatuaminiki kwasababu ya rushwa za majaji na kuingiliwa na Ikulu. ndio sababu mashauri haya yanamuliwa ICSID "

Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.

David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 kumuuliza Tundu A. Lissu kuwa nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuoneaha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?

Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja ya hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?

" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"

View attachment 2433362View attachment 2433363
Kafulila anafanya kazi nzuri Sana kwa sasa,
 
Huyu tumbili naye anahangaika ili akumbukwe kwenye teuzi, na akiangaliakesi inayomhusu mkewe imekaa vibaya anahangaika sana kujinusuru. Kafulila angefuata mfano wa Ali Hapi wa kwenda kulima tu.
Hahaa tumbili anawapigia gitaa waliomwita tumbili,waafrika wako tayari kuaibika kisa maslahi wacha tudharauliwe.
 
Unaongea nini ndugu? Mbona unachoeleza ndicho alichodadavua Lissu tena kwa undani zaidi?Au hujasikia clip yake? Au ni chuki zako tu kwake? Wewe ni wa kumfundisha sheria Lissu kweli?
Ya kuwa tunapelekwa kwenye arbitration ni kwa sababu ya wawekezaji kuogopa sheria za nchi husika. Sasa mbona kuna kesi za Saudia Arabia, Egypt, Italy, Spain, Hungry na other EU states ambazo kama ukubaliani na maamuzi ya mahakama zao unaweza kukataa rufa mpaka mahakama ya EU Brussel na bado zimepelekwa ICSID.

Ni hivi arbitration mara nyingi hasa kwa nchi za wenzetu huwa kwenye maelewano ya mkataba ukitokea mzozo namna utakavyoamuliwa.

Ebu kwanza google arbitrator chair huwa ni nani? normal judge au industry expert.

Lissu Nguli wa sheria kwako wewe.

Mimi najifunza misingi ya sheria kwa watu walioanzisha mijadala ya justice na concept zao zinatumiwa kwenye utungwaji wa sheria na kutoa haki mpaka leo. Sasa wewe katika hawa ushamsoma nani?

  1. Plato na maelezo yake ya distributive justice.
  2. Aristotle corrective justice
  3. Thomas Aquinas as social harmony
  4. Karl Max
  5. Chaim Perelman
  6. Jeremy Bentham
  7. John Stuart Mill
  8. John Rawls
  9. Robert Nozick
  10. Rudolph von Jhering
  11. Roscoe Pound
  12. Wesley Hohfeld
Or who exactly perspective of Justice is more attuned to your beliefs.

Lissu ni mwanasheria bora kwa viwango vyako sio kila mtu.
 
Wewe ndio unalisha watu matango pori. Hiyo sio private entity ni entity inayotmbulika under international dispute resolution ndio maana kabla ya Magufuli kuingia Investment Act iliitambua hiyo mahakama, na Tanzania ni mwanachama.
Arbitration sio public hearing kama mahakama unazozijua wewe, ni private hearing wanaoingia ni involved parties only.

Hakuna raia wala vyombo vya habari.

Like seriously haya mambo sio lazima ata uwe mwanasheria kuyajua kwenye masomo ya biashara na management degrees ni mandatory kufundishwa modules za ‘business law’, contract law or ‘dispute resolution process (which covers different ADR and their legal implication). Sasa katika hizo modules kama ukusoma zote basi walau ata moja ni mandatory nchi za wenzetu.

Arbitration ni ADR (alternative dispute resolution) its private sio mahakama kama tulizozizoea na inaendeshwa na industry expert husika in normal circumstances wote mnatakiwa mumuafiki.

Yaani ata hilo watanzania atuelewi na kila siku tunashitakiwa huko.
 
Asiposamehe, asifikiri anamkomoa JPM au yeyote. Anajikomoa yeye. Maana unaposamehe katika maisha haya, unakuwa unajitendea wema mwenyewe. Vinginevyo chuki zikizidi ndizo zitakazo muua, licha ya kuwa alipona risasi za Dodoma.
Umeshawahi kupigwa risasi?
 
Umeshawahi kupigwa risasi?

Lkn haina uhusiano wa yeye kusamehe. Vinginevyo maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Akiamua kujifungia kwenye gereza la chuki na kisasi, uamuzi unabakia mikononi mwa Tundu.
 
Lkn haina uhusiano wa yeye kusamehe. Vinginevyo maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Akiamua kujifungia kwenye gereza la chuki na kisasi, uamuzi unabakia mikononi mwa Tundu.
Wewe ndiyo ulimpiga lissu risasi so unamuomba akusamehe???
 
Wasalaam wana wa Mungu.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Zacharia Kafulila, amekosoa kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A Lissu kuhusu hoja ya kesi ya kukamatwa kwa Ndege na zingine mashauli yake kushughulikiwa kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya kibiashara kama ICSID- international Center For Settlement of Investment Disputes.

====

Akikosoa kauli hiyo, David Zacharia Kafulila amenukuliwa kwenye mtandao wa tweeter akiandika haya " Sitaki kujadili suala la kesi, naomba nijadili suala moja tu la uelewa kuhusu ICSID na Uanachama wake kwani Tundu A Lissu amepotosha katika hilo na huenda akawafanya wasiofahamu kuamini kwamba Tanzania ni mwanachama wa ICSID kwa Sababu ya Udhaifu wa Mahakama na Serikali ya Tanzania katika kusimamia Uhuru wa Mahakama.

Tundu A Lissu alinukuliwa kupitia ClubHouse akieleza kuwa " Lazma ieleweke kuwa sababu ya mashauri haya ya mikataba baina yetu na kampuni za nje kushughulikiwa kwenye mabaraza haya ya usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kama ICSID inatokana na tabia ya Serikali yetu ikiwa chini ya JPM na hata Samia kuingilia mambo ya mahakama na hivyo mahakama kukosa uhuru. Hivyo mahakama zetu haziaminiki, serikali yetu haiaminiki, hatuaminiki kwasababu ya rushwa za majaji na kuingiliwa na Ikulu. ndio sababu mashauri haya yanamuliwa ICSID "

Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.

David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 kumuuliza Tundu A. Lissu kuwa nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuoneaha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?

Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja ya hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?

" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"

View attachment 2433362View attachment 2433363
Sasa tujibaki kwenye logic ya kawaida.... Kati ya Tundu lissu na kafulila ni yupi mzalendo wa kweli. ...

Mzalendo wa kweli atabaki kuwa Tundu lissu , kwa maana ya kwamba anatufunulia Yale ambayo watesi wetu hawataki tuyajue kuusu maslai mapana ya Taifa letu Tanzania
Ila haya wakina kafulila wapuuzi tuu, watafuta teuzi. . Wapi subjective kwenye Kila kitu badala ya kuwasaidia wananchi wa tz ambao wengi wao ni maskini, na fukara wa fikra wao wanafuraia kuwapitosha.......
Kiufupi Lissu ni kiongozi Bora ila watesi wake ndio wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom