Wasalaam wana wa Mungu.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu, David Zacharia Kafulila, amekosoa kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu A Lissu kuhusu hoja ya kesi ya kukamatwa kwa Ndege na zingine mashauli yake kushughulikiwa kwenye Mabaraza ya Usuluhishi ya kibiashara kama ICSID- international Center For Settlement of Investment Disputes.
====
Akikosoa kauli hiyo, David Zacharia Kafulila amenukuliwa kwenye mtandao wa tweeter akiandika haya " Sitaki kujadili suala la kesi, naomba nijadili suala moja tu la uelewa kuhusu ICSID na Uanachama wake kwani Tundu A Lissu amepotosha katika hilo na huenda akawafanya wasiofahamu kuamini kwamba Tanzania ni mwanachama wa ICSID kwa Sababu ya Udhaifu wa Mahakama na Serikali ya Tanzania katika kusimamia Uhuru wa Mahakama.
Tundu A Lissu alinukuliwa kupitia
ClubHouse akieleza kuwa "
Lazma ieleweke kuwa sababu ya mashauri haya ya mikataba baina yetu na kampuni za nje kushughulikiwa kwenye mabaraza haya ya usuluhishi wa migogoro ya biashara na uwekezaji kama ICSID inatokana na tabia ya Serikali yetu ikiwa chini ya JPM na hata Samia kuingilia mambo ya mahakama na hivyo mahakama kukosa uhuru. Hivyo mahakama zetu haziaminiki, serikali yetu haiaminiki, hatuaminiki kwasababu ya rushwa za majaji na kuingiliwa na Ikulu. ndio sababu mashauri haya yanamuliwa ICSID "
Tundu A. Lissu ambae ni M/kiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea wa Urais wa JMT aliyepata kura kiduchu sana katika Uchaguzi Mkuu uliyopita wa 2020, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Siasa pekee ambaye familia yake yote ni Raia wa Marekani ameonekana mara zote kuwa upande wa mataifa ya nje kuliko taifa lake.
David Zacharia Kafulila anatoa mfano wa nchi kubwa kama Marekani na Uchina zikiwa nchi wanachama wa ICSID kama ilivyo kwa Tanzania pamoja na nchi nyingine zaidi ya 166 kumuuliza Tundu A. Lissu kuwa nchi zote hizi Mahakama zao zinaingiliwa kama ilivyo kwa Tanzania ama ni utaratibu tu wa hiari wa kiusuluhishi uliowekwa Duniani katika kuoneaha imani kwa wawekezaji hasa wa nje?
Hoja ya David Zacharia Kafulila kwa Tundu A. Lissu ni kwamba kama Tanzania Mahakama zake siyo huru ndiyo sababu kesi za migogogro ya kibiashara zinafanyikia nje kwenye tume hii ya ICSID. Je, Marekani na Uchina ambazo nazo kesi zao za migogogro ya kibiashara zinafanyikia huko huko ICSID tulikopelekwa sisi kwa hoja ya hiyo ya Lissu anataka tuamini pia kuwa Mahakama za mataifa haya pia haziko huru?
" Lissu acha kuzipaka matope Mahakamani za Tanzania, unataka kutuambia US & China ambao nao ni wanachama wa ICSID Mahakama zao zinaingiliwa ?"
View attachment 2433362View attachment 2433363