Kafulila: Serikali haiwezi kujenga kila kitu, punguzeni kuzaliana, tumieni uzazi wa mpango

Kafulila: Serikali haiwezi kujenga kila kitu, punguzeni kuzaliana, tumieni uzazi wa mpango

China waliweka mpango wa uzazi wa mtoto mmoja wakiwa taifa fukara ili kufikia malengo yao ya maendeleo ya sasa, kwa sasa wameshafikia malengo yao ya maendeleo na kuwa taifa tajiri wamebadilisha sera kulingana na mahitaji ya wakati huu.
Je, ni kweli one child policy pekee ndiyo ilisababisha maendeleo makubwa ya kiuchumi China? Au Kuna mengine, na kama yapo basi population plan bila economic reforms, industrialization, technology driven & productivity ni ngonjera tu.
 
Haikuwa one child policy pekee iliyoleta maendeleo China. Maendeleo popote duniani huchangiwa na mambo mengi ikiwemo idadi sahihi ya watu au mpango bora wa uzazi kwa raia.
 
Haikuwa one child policy pekee iliyoleta maendeleo China. Maendeleo popote duniani huchangiwa na mambo mengi ikiwemo idadi sahihi ya watu au mpango bora wa uzazi kwa raia.
 
Huku kijijini kwetu, watu ni wachache sana; kwa sasa tusipozaa, kuna uwezekano huko mbeleni kijiji kikatawaliwa na miti tu.​
 
We mpiga gwaride, Elimu yetu haikubaliki nchi za nje sijui utanielimisha kitu gani zaidi ya upuuzi.
Huo mpango wa uzazi umewashinda China wakautupilia mbali, kweli sisi tutauweza? Na jiulize kwa sababu gani China hawautaki tena. Nenda ukafanye research.
Usijitoe akili. Unajua vizuri hizo pesa za miradi zinaishia wapi, wala tusipotezeane muda. Acheni visingizio vya kizushi.
Akaangalie madhara kule Japan na South Korea.
 
China waliweka mpango wa uzazi wa mtoto mmoja wakiwa taifa fukara ili kufikia malengo yao ya maendeleo ya sasa, kwa sasa wameshafikia malengo yao ya maendeleo na kuwa taifa tajiri wamebadilisha sera kulingana na mahitaji ya wakati huu.
Hatari Sana
 
Tunaposema tuwe na strong internal market, huwa mnawadha titawajaza warundi au wanyama humo?

Bado kwa Tanzania tunahitaji population yetu iende angalau watu milioni 150.

Ndio angalau kuwaza uzazi wa mpango
 
Internal market inategemea zaidi hali ya watu kiuchumi kuliko idadi ya watu. Australia, Canada, Sweden na Norway ni internal markets kubwa sana kuliko Tanzania.
 
Internal market inategemea zaidi Hali ya watu kiuchumi kuliko idadi ya watu. Australia, Canada, Sweden na Norway ni internal markets kubwa sana kuliko Tanzania.
Soko la ndani kule Canada ni dhaifu.
Asilimia 75 Hadi 85 ya bidhaa zinazozalishwa zinakwenda Marekani.

Wapo milioni 41 na wakati Marekani wapo zaidi ya milioni 300.

Hata tukiichukua Norway na kuilinganisha na China, nadhani utaona ipi yenye robust and strong internal market.

Ukiangalia sababu ni idadi ya watu na kuwa na middle income wengi
 
Linganisha na Tanzania,
Halafu tunapozungumzia over/under population ya nchi kigezo ni "population density". Wastani wa idadi ya watu kwa eneo Marekani ina watu wachache kuliko Tanzania.
 
Linganisha na Tanzania,
Halafu tunapozungumzia over/under population ya nchi kigezo ni "population density". Wastani wa idadi ya watu kwa eneo Marekani ina watu wachache kuliko Tanzania.
Na Norway ina watu wengi kuliko Tanzania, ukiangalia population density yao.
 
Na Norway ina watu wengi kuliko Tanzania, ukiangalia population density yao.
Unaelewa unachouliza kweli?!
Soko la ndani la Norway yenye watu milioni 5 na population density ndogo kuliko Tanzania ni kubwa mara nyingi sana kuliko soko la ndani la Tanzania lenye watu milioni 70 na population density kubwa.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, ametoa angalizo la kiuchumi kuhusu mipaka na uwezo wa kifedha wa serikali, akisisitiza kuwa nchi haiwezi kuendelea kubeba mzigo wa kujenga kila mradi wa kibiashara huku ikikabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu linalohitaji uwekezaji wa haraka katika elimu ya ufundi na maarifa.

Akiongoza mhadhara, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, alieleza kwa mantiki kuwa mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi si anasa, bali ni dharura ya kiutawala inayosaidia kuondoa urasimu na kuelekeza rasilimali kwenye maeneo yenye tija zaidi kwa jamii.

“Serikali haiwezi kuwa na bajeti ya kutosha kujenga barabara kuu, masoko na vituo vya mabasi, kisha ikagharamia hadi ujenzi wa vyoo ndani ya stendi hizo na kubakiwa na uwezo wa kuwapatia elimu bora watoto wa familia masikini,” alisema Kafulila.

Alibainisha kuwa njia mbadala ya kimkakati ni kuziachia kampuni na sekta binafsi kujenga na kuendesha miradi yote ya kibiashara, ili fedha zinazookolewa zielekezwe kwenye ujenzi wa hospitali, ununuzi wa dawa na utoaji wa elimu bora.Mkurugenzi mtendaji huyo alianika takwimu zinazoonyesha kuwa kasi ya ongezeko la watu nchini imefikia asilimia 3.4, kiwango ambacho ni cha juu ukilinganisha na wastani wa bara la Afrika ambayo ni asilimia mbili.

“Ongezeko la idadi ya watu duniani limefikia asilimia moja huku India ikifikia asilimia 0.8, na kwamba China ambako idadi ya watu inaendelea kupungua,” alibainisha. Alionya kuwa iwapo kasi hii ya ongezeko la watu ambao wengi wao wanatoka katika kaya masikini haitadhibitiwa kupitia elimu ya uzazi wa mpango, itaendelea kuwa mzigo mzito wa kibajeti ya Taifa katika utoaji wa huduma za msingi.
Hatujawai kupata ufafanuzi unaofuta alichoibua PolePole kuwa miradi ya PPPC inaongezwa cha juu sana hadi inapoteza maana kuliko serkali kujisimamia!
Dhana nzuri, utekelezaji unageuka kiota cha ufisadi!
Kuhusu idadi ya watu kila serkali inapowekwa iwe na mrengo ule ule.
Mzee Magu alijitahidi kuhamasisha kuzaliana iwezekanavyo!(mambo ya kila mtoto huja na riziki yake!)
Ila naamin dhana ya kuzaliana sana ni hatari sana kama mifumo ya uzalishaji imedumaa(mf Tz) na ni tija kama mifumo imeseti kia kiumbe kufanya kazi(mf China)
Watoto wengi leo ni zao la starehe za ngono iwe ndan au ya ndoa.
Nashauri sasa tuhamishie kampeni kwa wanaume wenye mbegu(zaid ya vasectomy, kondom na withdrawal) mana kampeni kwa wanawake, mbinu zote zimefeli kwa sabab hawamiliki kanuni za mchezo!
Nashauri pia ufanyike utafiti kwanini kuna ongezeko la mabinti kupenda sana ngono mapema kuliko zamani!!! Hadi wavulana wanalazimishwa na vibinti!
Ikibidi itengenezwe sheria ya kutoa adhabu kali kwa binti anayebeba mimba (Nadhan Znz ipo).
Kijamii mama Gwajima nusuru jamii ulopewa dhamana kwa kuunda Kamati ya maadili ngazi ya kila kitongoji ya wazee na watu wenye maadili.
Badala ya sheria rasmi na urasmu wake itumie Equity doctrine(sijui kiswahili chake)
Unakuta boda anasambaza ukimwi na sheria za ushahid hazina pa kumfix vizuri.
Au binti mdogo anadanga kushirikiana na mama yake!
Au changudoa anagawa UTI ovyo!
Wazee na vijukuu!
Watumishi wa umma na wake za watu.
Hata kama tuna upungufu wa wazee wenye moral authority kukemea hadi wengine wanakuwa machawa wa vijana, lakin kuna haja ya kuwekeza katika kusimamiana ngazi ya chini kabsa kulingana na mila na desturi za pahala bila kuzisigina sheria za juu yake.
 
Iceland ina watu laki nne tu na ina uchumi sawa na nusu ya uchumi wa Tanzania.
 
Soko la ndani kule Canada ni dhaifu.
Asilimia 75 Hadi 85 ya bidhaa zinazozalishwa zinakwenda Marekani.

Wapo milioni 41 na wakati Marekani wapo zaidi ya milioni 300.

Hata tukiichukua Norway na kuilinganisha na China, nadhani utaona ipi yenye robust and strong internal market.

Ukiangalia sababu ni idadi ya watu na kuwa na middle income wengi
Iceland ina watu laki nne tu na ina uchumi sawa na nusu ya uchumi wa Tanzania. It's more about quality of people and not big number.
 
Watu ndiyo uchumi aache ujinga
Watu wengi bila elimu,
Watu wengi bila maarifa.
Watu wengi bila uchumi mbovu.
Watu wengi bila ukuaji wa uchumi.
Watu wengi bila ongezeko la uchumi.
Ukuaji wa uchumi lzm uendane na ukuaji wa uchumi na maarifa.
 
Iceland ina watu laki nne tu na ina uchumi sawa na nusu ya uchumi wa Tanzania. It's more about quality of people and not big number.
Big number ndio iliyoifanya china kuwa world manufacturing economy.

Ndio iliyoifanya India kuoneka ndio ruler of global south

Ndio iliyoitengenezea Nigeria kuwa Africa first economy.

Bado soko la ndani la Iceland halitoshelezi Bali wapo kwenye strategic location ila Bado kwa idadi ndogo ya population hawawezi kuja kuwa western Europe giant au Scandinavian giant economy.

Iceland hii yenye Nominal GDP kati ya 35 billion to 57 billion na Tanzania yenye 80 billion au Kuna nyingine?
 
Back
Top Bottom