Kafulila: Serikali haiwezi kujenga kila kitu, punguzeni kuzaliana, tumieni uzazi wa mpango

Na kuanzia sasa kuzaa hasa maeneo ya miji mikubwa iwe kwa gharama ya milioni 5.
Hakuna cha bure wala nini....
Ila mama mazazi atakaezaa kwa hiyo ghrama maana yake yeye na mme wake wana uwezo wa kulea watoto, kwahiyo ghrama za hospitali za mtoto mpaka afike miaka 16 ziwe za nafuu karibu ya bure, endapo mtoto ahahakikiwe kuwa yuko bado katika masomo ya shule na mwisho wa gharama nafuu iwe baada ya kumaliza shule ya msingi....
Maana yake huyo mtoto lazima atakuwa anahudumiwa vizuri na familia yake awe mwananchi bora....

Imefikia sasa wabongo wajue kuzaa na kulea ni gharama yao, sio ya serikali na hata shule ziweke aina ya gharama ya kutoza wazazi ambao hawana ushahidi wa kulipa kodi kama mfanyakazi au mfanyabiashara...
 
Ukweli gani? Tanzania Ina mapori ambayo hayajawai guswa yapo tu.

Then njoo Tanzania tuna kila aina ya rasilimali ambazo zikitumiwa ipasavyo kila mtu atafaidika na kupata maisha yaliyo Bora.

Changamoto kubwa haya Mafisadi hayaoni tatizo la nchi hii ni ufisadi, badala yake hutafuta wa kumrushia lawama ili yaonekane wao siyo shida. Kumbe shida kubwa ni wao walioko hapo.
Mkuu,

Unaelewa population increase ya nchi kama yetu ikoje? Unaelewa ni asilimia ngapi?

Unaelewa rate ya population increase ni ngapi? Unaelewa population yetu ina double kila baada ya miaka mingapi?

Unaelewa kwa kuzaliana kwa sasa, kufikia mwaka 2050 tutakuwa watu wangapi?

Unaele2a Tanzania population ina double kila miaka mingapi sasa?

Unaelewa kuwa kuwa na mapori mengi na rasilimali nyingi si hoja, kwa sababu unaweza ukawa na mapori na rasilimali ambazo huwezi kuzitumia, huna elimu, hayo mapori yote ukayakata ukabaki na jangwa na watu kibao ambao hata kulima hawawezi kwa sababu wamegeuza nchi yao kuwa jangwa?

Unaelewa overpopulation si suala la ardhi wala mapori, ni suala la watu kuweza kutumia hiyo ardhi na resources effectively?

Unaelewa kuwa nchi inaweza kuwa ndogo, ina watu wengi, na haiko overpopulated, kwa sababu watu wake wanaweza kutumia teknolojia vizuri, halafu nchi inaweza kuwa kubwa, haina watu wengi, ikawa overpopulated kwa sababu watu wake hawawezi kutumia teknolojia kuitumia hiyo ardhi effectively?

Do you even know what overpopulation is?

Naona Watanzania wengi hata hawajui overpopulation ni nini, wakipita huko kati na kuona mapori wanaona nchi bado inahitaji watu zaidi mapori mengi tu.
 
Big number ndio iliyoifanya china kuwa world manufacturing economy.

Ndio iliyoifanya India kuoneka ndio ruler of global south

Ndio iliyoitengenezea Nigeria kuwa Africa first economy.

Bado soko la ndani la Iceland halitoshelezi Bali wapo kwenye strategic location ila Bado kwa idadi ndogo ya population hawawezi kuja kuwa western Europe giant au Scandinavian giant economy.

Iceland hii yenye Nominal GDP kati ya 35 billion to 57 billion na Tanzania yenye 80 billion au Kuna nyingine?
Yote uliyoandika hapa sio kweli.
 
Asitupangie uzazi. Huu ni mtego wa wazungu. Tusikubali kuingia. Wao kizazi kimepungua kiasi cha kutisha wameanza kuhofia tutawazidi idadi sasa wanataka nasi tuache kuzaa. Kumbuka huko nyuma sababu moja ya wao kuwa na nguvu za kututawala ni wao kuwa wengi kuliko sisi. Tuzae tu. Karne zijazo ni zamu yetu.
Mkuu,

Ukiwazidi kizazi kwa kuzaana tu bila mpango, halafu ukafa mpaka ukafutika kwa njaa na UKIMWI ndiyo utakuwa umefanya nini sasa?

Yani unaamini kabisa kuwa Africa watu wajinga wakiongezeka kwa kasi ya sasa ndiyo tutawashinda hao unaowaita wazungu?
 
Populat

Soma kuhusu "Demographic Transition Model"
Utafiti unaonyesha kwamba kulazimisha ukomo wa uzazi kwa familia maskini (kwa mfano, kupitia shinikizo,
kulazimisha watu au sera za misaada zenye masharti makali) mara nyingi huleta matokeo yasiyotarajiwa.
Kwa familia maskini watoto ni nguvu kazi.
Kuzizimisha kuwa na watoto wachache bila kubadilisha hali hizi za msingi za kiuchumi ni kuongeza umaskini.
Maendeleo ya kiuchumi kwa kawaida husababisha kupungua kwa viwango vya uzazi, organically.
Nchi zote tajiri zilipunguza uzazi si kwa shinikizo kama tunavyofanya.
Tujikite kwenye maendeleo ya kiuchumi uzazi holela unapungua.
 
Acha ujinga, Waafrika kuwa wengi kama siafu na kuwazidi idadi wazungu wala haina athari yoyote chanya kwa bara la Africa zaidi ya kukimbilka huko kwao wazungu na kuwajazia nzi tu.
Soma kuhusu "Demographic Transition Model"
Utafiti unaonyesha kwamba kulazimisha ukomo wa uzazi kwa familia maskini (kwa mfano, kupitia shinikizo,
kulazimisha watu au sera za misaada zenye masharti makali) mara nyingi huleta matokeo yasiyotarajiwa.
Kwa familia maskini watoto ni nguvu kazi.
Kuzizimisha kuwa na watoto wachache bila kubadilisha hali hizi za msingi za kiuchumi ni kuongeza umaskini.
Maendeleo ya kiuchumi kwa kawaida husababisha kupungua kwa viwango vya uzazi, organically.
Nchi zote tajiri zilipunguza uzazi si kwa shinikizo kama tunavyofanya.
Tujikite kwenye maendeleo ya kiuchumi uzazi holela unapungua.
 
Populat

Soma kuhusu "Demographic Transition Model"
Utafiti unaonyesha kwamba kulazimisha ukomo wa uzazi kwa familia maskini (kwa mfano, kupitia shinikizo,
kulazimisha watu au sera za misaada zenye masharti makali) mara nyingi huleta matokeo yasiyotarajiwa.
Kwa familia maskini watoto ni nguvu kazi.
Kuzizimisha kuwa na watoto wachache bila kubadilisha hali hizi za msingi za kiuchumi ni kuongeza umaskini.
Maendeleo ya kiuchumi kwa kawaida husababisha kupungua kwa viwango vya uzazi, organically.
Nchi zote tajiri zilipunguza uzazi si kwa shinikizo kama tunavyofanya.
Tujikite kwenye maendeleo ya kiuchumi uzazi holela unapungua.

Kabla ya mimi kusoma chochote unachopendekeza, wewe nisome mimi kwanza, kwa utulivu, kwa ufahamu. Soma unielewe. Usiweke kasumba zako ukazipitisha kuwa ndiyo mawazo yangu wakati mimi sijaweka hoja hizo, hayo ni mawazo yako kuwa ninafikiri hivyo tu.

Mfano.

Hakuna popote niliposema yeyote alazimishwe ukomo wa uzazi.

As a libertarian and a defender of human rights, I am against that.

Unasoma unachotaka kusoma wewe, si nilichoandika mini.

Nikikuambia unipe sentensi moja niliposema watu walazimishwe kutozaa, au wapangiwe idadi ya watoto wa kuzaa, hutapata hiyo sentensi.

This is a strawman argument logical fallacy.

Unapinga hoja ambayo mimi sijaitoa, kwa kusema ndiyo hoja yangu.

Mimi ni mtu ninayeelewa na kuheshimu haki za binadamu, na haki za watu kujiamulia mambo yao, haki za kuamua kuzaa watoto, zote ni haki za binadamu.

Hata hujaelewa hoja yangu.

Unapinga hoja ya serikali/jamii kuweka ukomo wa uzazi, kulazimisha watu wasizae, wakati hiyo si hoja yangu.

Hujanielewa.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, ametoa angalizo la kiuchumi kuhusu mipaka na uwezo wa kifedha wa serikali, akisisitiza kuwa nchi haiwezi kuendelea kubeba mzigo wa kujenga kila mradi wa kibiashara huku ikikabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu linalohitaji uwekezaji wa haraka katika elimu ya ufundi na maarifa.

Akiongoza mhadhara, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, alieleza kwa mantiki kuwa mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi si anasa, bali ni dharura ya kiutawala inayosaidia kuondoa urasimu na kuelekeza rasilimali kwenye maeneo yenye tija zaidi kwa jamii.

“Serikali haiwezi kuwa na bajeti ya kutosha kujenga barabara kuu, masoko na vituo vya mabasi, kisha ikagharamia hadi ujenzi wa vyoo ndani ya stendi hizo na kubakiwa na uwezo wa kuwapatia elimu bora watoto wa familia masikini,” alisema Kafulila.

Alibainisha kuwa njia mbadala ya kimkakati ni kuziachia kampuni na sekta binafsi kujenga na kuendesha miradi yote ya kibiashara, ili fedha zinazookolewa zielekezwe kwenye ujenzi wa hospitali, ununuzi wa dawa na utoaji wa elimu bora.Mkurugenzi mtendaji huyo alianika takwimu zinazoonyesha kuwa kasi ya ongezeko la watu nchini imefikia asilimia 3.4, kiwango ambacho ni cha juu ukilinganisha na wastani wa bara la Afrika ambayo ni asilimia mbili.

“Ongezeko la idadi ya watu duniani limefikia asilimia moja huku India ikifikia asilimia 0.8, na kwamba China ambako idadi ya watu inaendelea kupungua,” alibainisha. Alionya kuwa iwapo kasi hii ya ongezeko la watu ambao wengi wao wanatoka katika kaya masikini haitadhibitiwa kupitia elimu ya uzazi wa mpango, itaendelea kuwa mzigo mzito wa kibajeti ya Taifa katika utoaji wa huduma za msingi.
Unapojenga kituo cha mavazi bila maliwato, mchoro ulisanifiwa na mhandisi au mwanasiasa? Watu wazae wakiweza, ila wake gharama za maisha pia.
 
Safi sana
 
Hakuna kikubwa unachosema hapa cha ajabu. Overpopulation ni jambo baya kwa nchi zote masikini na tajiri ila underpopulation ni tatizo kidogo kwa nchi zenye maendeleo kama China ila sio tatizo kabisa kwa nchi masikini kama Tanzania( hata hivyo Tanzania haina underpopulation).

Pia overpopulation ni suala linalohusu zaidi uwezo wa raia ku optimize rasimali zao, nchi nyingi kama Tanzania uwezo wa ku optimize rasimali zao ni mdogo sana hali inayofanya kuwa na idadi kubwa ya watu tatizo kubwa sawa na overpopulation.
Sir Einstein, overpopulation inaweza kuwa changamoto, lakini je, overcorruption haipo kwenye equation? Au hiyo sehemu tumeamua kuiacha kwa makusudi?.
 
Fungua uzi wa over corruption tujadili.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, ametoa angalizo la kiuchumi kuhusu mipaka na uwezo wa kifedha wa serikali, akisisitiza kuwa nchi haiwezi kuendelea kubeba mzigo wa kujenga kila mradi wa kibiashara huku ikikabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu linalohitaji uwekezaji wa haraka katika elimu ya ufundi na maarifa.

Akiongoza mhadhara, Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, alieleza kwa mantiki kuwa mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi si anasa, bali ni dharura ya kiutawala inayosaidia kuondoa urasimu na kuelekeza rasilimali kwenye maeneo yenye tija zaidi kwa jamii.

“Serikali haiwezi kuwa na bajeti ya kutosha kujenga barabara kuu, masoko na vituo vya mabasi, kisha ikagharamia hadi ujenzi wa vyoo ndani ya stendi hizo na kubakiwa na uwezo wa kuwapatia elimu bora watoto wa familia masikini,” alisema Kafulila.

Alibainisha kuwa njia mbadala ya kimkakati ni kuziachia kampuni na sekta binafsi kujenga na kuendesha miradi yote ya kibiashara, ili fedha zinazookolewa zielekezwe kwenye ujenzi wa hospitali, ununuzi wa dawa na utoaji wa elimu bora.Mkurugenzi mtendaji huyo alianika takwimu zinazoonyesha kuwa kasi ya ongezeko la watu nchini imefikia asilimia 3.4, kiwango ambacho ni cha juu ukilinganisha na wastani wa bara la Afrika ambayo ni asilimia mbili.

“Ongezeko la idadi ya watu duniani limefikia asilimia moja huku India ikifikia asilimia 0.8, na kwamba China ambako idadi ya watu inaendelea kupungua,” alibainisha. Alionya kuwa iwapo kasi hii ya ongezeko la watu ambao wengi wao wanatoka katika kaya masikini haitadhibitiwa kupitia elimu ya uzazi wa mpango, itaendelea kuwa mzigo mzito wa kibajeti ya Taifa katika utoaji wa huduma za msingi.
Kama haiwezi iwaachie wenye mabasi wajenge stand zao
 
Back
Top Bottom